Nikiomba tena ajira niiteni mbwa nimekaa paleee

Nikiomba tena ajira niiteni mbwa nimekaa paleee

Japo yawezekana ni simulizi tu ya kubuni lakini ndio hali halisi hasa ya vijana wengi nchini kwetu..huwezi amini kuna vijana wanatumiwa pesa na wenzao wa vijijini ambao waliwaacha njiani kwenye elimu.
 
Iyo simulizi inaualusia mkubwa sana, labda serikali ingalikuwa ni mtu moja mwenye utashi na siyo kikundi cha watu basi ingelisikia mengi mazuri inayoshauriwa, serikali yetu imeshaambiwa ipitie upya mfumo mzima wa elimu yetu, kwani siyo rafiki na mazingira ya sasa...Wahitimu wengi wanapomaliza Vyuo wengi utegemea ajira serikalini, kwa maana ya kwamba ndiko mfumo wa elimu ya Tanzania iliko, lkn km Serikali angalikuwa ni mtu moja basis naamini angeliweza kufanya kitu, zaidi kusimamia aya yanayosemwa na wadau hasa asasi za kirahia...
 
Japo yawezekana ni simulizi tu ya kubuni lakini ndio hali halisi hasa ya vijana wengi nchini kwetu..huwezi amini kuna vijana wanatumiwa pesa na wenzao wa vijijini ambao waliwaacha njiani kwenye elimu.
Kwanini iwe simulizi mkuu na kuna mstari umesema kuwa hiyo ndio hali halisi?

Mkuu hali ni mbaya mno mtaani
 
Nunua Mirunda na mabati chakavu gonga banda hapo mtaani mtafute dingilai mwepesi akukope eneo weka banda hapo nenda kwa mafundi geti kaombe rangi ilobaki piga chapa kibao TUITION TUITION AU LYKIZO TIME TUITION TUITION in 6 months period utakuja hapa unaimba mapambio
Yeah msimu wa likizo unawadia huu ndio msimu wa kupiga hela kwa vijana
 
Nashauri tu mtoto wako akimaliza form 4 mpeleke diploma elimu ya advance haina faida hata kidogo peleka diploma akapige kozi anayoitaka akimaliza achague either aende kazini au aendelee kusoma bachelor au asome bachelor huku akitumia cheti cha diploma ku apply kazi easy kama hivyo.

N.b
Wazazi mjue kuwa kitu anachofanya mwenye degree hata diploma anaweza kukifanya pia na mshahara wamepishana pesa ndogo sana tena naweza kusema diploma wanafunga na pesa ndefu sana kwa mwezi kuliko bachelor .
 
NIKIOMBA AJIRA TENA NIITE MBWA NIMEKAA PALE.

Anaandika Mo Mlimwengu.

Asubuhi ya alfajiri nikiwa tayari nimepanda basi la Happy Nation ambalo linang’aa kutokana na upya wake. Nilipendezwa na gari hilo kutokana na kuwa na sehemu ya kuchajia simu yangu. Nikiwa kwenye siti ambayo pembeni nilikaa na msichana mrembo ambaye sura yake ilikua ina rangi adimu nyeusi yenye mng’ao na huku umbile lake limepangwa likapangika na nyuma alikuwa ana kifurushi cha kutosha. Kukaa naye karibu nilifurahia maana pua zangu zilikuwa zinapokea harufu nzuri ya marashi aliyokuwa kayatumia.

Tukiwa kwenye kituo cha basi na gari limeishaanza kupiga honi kwa ajili ya kuanza safari, alipita machinga mmoja anauza earphone ikabidi nizinunue maana bei yake ilikuwa inauzwa elfu nne. Yule machinga hakuwa na chenji maana nilitoa noti ya elfu kumi yule mlimbwende niliyekaa naye pembeni aliweza kunisaidia hiyo elfu nne nikipata chenji safarini nitamrudishia. Uzuri wake ulinogeshwa na roho yake nzuri.Yule dada alikuwa ana moyo mweupe. Nilichukua earphone zile na kuweka kwenye simu yangu janja na kuzipachika kwenye masikio yangu. Chombo kikaanza safari ya kutoka Dodoma na kuelekea kijijini kwetu Kamachumu baada ya safari ya miaka mitatu ya kuhitimu shahada yangu ya kwanza.

Nikiwa ndani ya gari nilitumia muda mwingi kuwa busy sana na simu pamoja na muda mwingi niliutumia kuangalia nje maana nilikaa siti ya dirishani. Yule mlimbwende aliyekuwa pembeni yangu nilikuwa namuonea aibu maana ilikuwa nikitaka kumpiga jicho na kutana na jicho lake. Ilinifanya nitengeneze hofu kidogo kumkabili uzuri wake ulinifanya nimuogope kimoyomoyo nikajisemea wakubwa wanafaidi. Hivyo kuwa kwangu dirishani kulinifanya muda mwingi nipende kuangalia nje na kufurahisha macho yangu kuona namna Tanzania yangu ilivyo kubwa na ina maeneo mengi ambayo watu hawaishi.Nilifurahia namna tulivyo na uoto wa asili wa kuvutia kwenye maeneo mengi kwenye mikoa ambayo tulikuwa tunapita.

Nikiwa ndani ya gari nilitumia muda mwingi kuwaza namna nitakavyofika nyumbani na kukutana na marafiki zangu ambao tulisoma wote kipindi cha primary na secondary. Raha zaidi na kilichokuwa kinafanya nione gari halikimbii ni rafiki yangu wa kike Koku ambaye tulikuwa na ahadi ya kuoana pale nitakapokuwa nimehitimu shule na kupata kazi. Koku nilimpenda sana naye alinipenda sana nilikuwa nimewamiss sana wazazi wangu lakini Koku nilimmiss zaidi. Niliamini mapenzi yetu yalikuwa yananoga zaidi ya Romeo na Julieth. Ilikuwa safari ya masaa 17 kufika nyumbani ilinifanya nipate tafakari mpya ndani ya gari ya kuanza maisha mapya baada ya kupata elimu yangu.

Nilifika saa tano usiku baadae nikachukua bodaboda ambayo iliweza kunifikisha nyumbani. Bodaboda ni kijana mwenzangu ambaye tulisoma wote shule ya msingi ila yeye hakuweza kuendelea na masomo kutokana na ufaulu wake kuwa mdogo. Alifurahi kuniona na alikuwa akiniamini sana kutokana na namna darasani nilikuwa vizuri aliamini ni suala la muda tu nitapata kazi nzuri ambayo ingeendana na elimu yangu. Ni wale watu ambao akibishana na watu juu ya jambo fulani lazima akupigie simu anaamini kila jambo unalijua. Tukiwa njiani aliweza kunipa story mbalimbali za kijijini. Kuniambia watu ambao wameoa na ambao wameishafariki na vilevile alinipa taarifa nzuri ya kwamba nyumba yake ndio anakaribia kupaua hivyo ikiwezekana kesho yake atanipelekea nipaone. Nilifurahi sana alikua ana story nyingi na zote anataka nizijue is wakati mwingine kutokana na upepo nilikuwa simsikii ila naishia kusema ndio maana huwa hawakawii kusema unaringa.

Nilizoea maisha ya kijijini na kila muda ulivyokuwa unazidi nilianza kupotezana na marafiki zangu ambao tulimaliza wote chuo. Walikuwa wananitumia baadhi ya post za ajira nyingine nilikuwa ninaapply napata lakini nashindwa nauli ya kwenda kufanya interview. Ilifika muda nikaanza kukosa hata vocha yule rafiki yangu bodaboda akawa ananisadia hela ya vocha. Alinipenda sana na muda mwingi alipenda kuongozana na mimi na pale kijijini nilikua maarufu kutokana na mimi kuwa miongoni mwa vijana ambao walikuwa wamesoma hadi kufika vyuo vikuu hivyo jamii ya pale iliniheshimu sana. Kadri muda ulivyokuwa unazidi ndivyo na mimi maisha yangu yalikuwa yanazidi kuwa magumu kwangu na heshima kwa watu inazidi kushuka. Habari mbaya ni pale ambapo Koku aliniandikia barua ya kuniomba msamaha kwamba kapata mwanaume wa kumuoa hawezi kuendelea kubaki nyumbani tena ni bora aolewe kutokana na msukumo wa maisha yake. Kwenye barua Koku alimalizia na kusema Mlimwengu bado nakupenda ila maisha hayajataka iwe hivyo. Misuli ilinitoka mwili mzima huku jasho likichuruzika taratibu na macho yalinitoka kama mjusi umebanwa mlangoni. Nilikuwa sina cha kuzuia zaidi ya kutaka kutoa machozi ambayo hayakutoka kwa hasira nilichana ile barua. Niliishia kusema wanawake wote ni mbwa nikasahau kwamba mama yangu naye ni mwanamke. Niliyachukia maisha na mimi nikajichukia hapo ilikuwa imeishapita miaka miwili nihitimu chuo. Nilishaomba ajira serikalini na taasisi binafsi lakini sikuwa nimepata sehemu yeyote.

Nikiwa nimekaa chini ya mti nikazidi kukumbuka maneno ya mjomba wangu ambaye aliniambia Mlimwengu wewe soma shule ukishamaliza nitafute. Na alikua akinisisitiza kwamba mjomba ni mama kwahiyo alipenda kusema kwamba mim ni mama yako. Lakini sasa ni zaidi ya miaka miwili yule mjomba wangu nikipiga simu hapokei na anamuambia mama kwamba mimi ni mvivu.
Simu yangu janja ilibidi niuze na zile nguo zangu ambazo nilikuwa nikivaa kijijini naonekana mtanashati zote zimeishapauka. Maskini Mlimwengu mimi nakumbuka lile boom la chuo na siwezi kulipata tena. Mlimwengu nikaanza kutafuta namna ya kupotezea mawazo kwa kunywa pombe ya kienyeji pale kijijini. Kilichoniuma zaidi mzee wangu akaanza kuwaambia majirani kwamba ana mashaka na mimi haiwezekani niseme nina degree wakati nyumbani nimekuwa tegemezi. Baba aliamini huenda nilienda mjini kuzurura ila chuo sijasoma na kumbuka graduation sikufanya kutokana na kukosa nauli ya kwenda kufanya sherehe. Iliniuma sana kuona wazazi wangu wenyewe wanashindwa kuniamini. Nilianza kuwa mlevi wa kupindukia na hapo ndipo ugomvi na familia yangu ukawa mkubwa na mzee wangu akanifukuza pale nyumban kwamba kazi ni kumaliza chakula na kujaza choo. Maskini msomi mimi nilianza kuchukia dhana ya elimu na nikiona wanafunzi wamevaa sare nawaonea huruma. Ilikuwa nikilewa naongea kiingereza kitupu. Yule mama muuza gongo alikuwa mjane hivyo ikafanya nianze kuwa kibenten chake. Baada ya mzee wangu kusikia kwamba naishi na yule mama muuza. Mzee wangu alikuja kumfokea kwamba aachane na mimi. Kijiji kizima walihisi nimerogwa siyo Mlimwengu waliyekuwa wanamjua.

Yule mama muuza alinipenda sana ikawa hadi ananinunulia nguo. Kwa umri alikuwa kanizidi sana maana alikuwa na watoto wawili na wote walikuwa wanasoma sekondari . Hivyo kwake tuliishi wawili kama mke na mume kutokana na watoto wake kusoma shule za boarding. Hakuna siku ambayo niliiona ngumu kwangu pale nilipokutana na Koku na mume wake wamekuja kijijini kusalimia. Koku licha ya kuwa kashazaa ila alikuwa mzuri sana. Kutokana na mume wake kuwa na maisha mazuri kulimfanya Koku azidi kunawiri. Koku siku moja alinitafuta na alikuwa kashaambiwa story zangu kijiji chetu huwa hakina siri. Wengi walijua atafurahia kumbe alisikitika sana. Ilimfanya anitafute na aliniachia elfu hamsini lakini wakati anaondoka aliniambia wewe siyo Mlimwengu ninayemjua badilika.

Maisha kwangu yalizidi kuwa magumu sana na faraja yangu kubwa ilikuwa kwa mama muuza. Ni mwanamke ambaye alikuwa ananisikiliza peke yake. Nilikuwa nikitaka hela namuomba nauli ya kwenda mkoani au wilayani ananipatia akijua ananisaidia nipate kazi kumbe mimi ile hela naishia kwenda kulewa kwenye vilabu vingine. Nilkuwa sijionei huruma ikawa starehe yangu ni pombe tu. Siku moja mama yangu alinifuata kilabuni alilia sana akaniomba kwamba najua wewe hujipendi basi niheshimu mimi mama yako. Mama alishindwa kuongea akaishia kulia. Niliishia kumuambia mama aache uchuro hakuna mtu aliyekufa hapa. Nilivyoona mama hanielewi niliondoka zangu nikamuacha akiwa amekaa chini. Kesho yake nilivyoamka nikakumbuka namna mama alivyokuwa anabubujikwa na machozi. Kwa sauti ya chini nilisema nabadilika nikaanza kupunguza unywaji wa pombe na kuanza kutafuta kazi kwa udi na uvumba.

Serikali ikatangaza kazi nyingi na mimi nikaapply nikiamini huu ndio wakati wangu wa kupata kazi. Nikawa nasikia semina za vijana kujiajiri ninajiuliza maswali mengi ni kweli inabidi tujiajiri lakini lazima mazingira rafiki ya kujiajiri bado hayajatengenezwa. Kiukweli kilichonikatisha tamaa zaidi ni kuona ajira zote nimekosa. Kwa akili zangu timamu Mlimwengu mimi nikiomba tena ajira niiteni mbwa nimekaa pale na nilikuwa nimeomba sensa ninajua nayo sitapata hivi kama mna mawasiliano nao waambieni wafute majina yangu. Sitaki tena ajira yeyote. Nitaishi kwa kudra za Mungu maana nimeshindwa kuishi inavyostahili.
so sad but too early to give up bro
 
Nimekosa tena ajira ya ualimu kipindi ambacho naiihitaji mno, Pdf zima limejaa certificate na diploma sisi bachelor sjui tukale wapi?

Kungekuwa kuna namna ya kuibadilisha degree kuwa certificate ningefanya hivo ili mradi nizame ajirani.

Nimeamua kuachana kabisa na huu ujinga wa kuifikiria ajira , ngoja nipambane na mtaa kama sjawahi kwenda shule.

Naota ndoto hazina rangi ngoja niamke nizipake.
Pole sana
 
Nimekosa tena ajira ya ualimu kipindi ambacho naiihitaji mno, Pdf zima limejaa certificate na diploma sisi bachelor sjui tukale wapi?

Kungekuwa kuna namna ya kuibadilisha degree kuwa certificate ningefanya hivo ili mradi nizame ajirani.

Nimeamua kuachana kabisa na huu ujinga wa kuifikiria ajira , ngoja nipambane na mtaa kama sjawahi kwenda shule.

Naota ndoto hazina rangi ngoja niamke nizipake.
Nimeamua kuachana kabisa na huu ujinga wa kuifikiria ajira , ngoja nipambane na mtaa kama sjawahi kwenda shule.
[emoji1534]
 
Ajira nimeziomba sana ila kupata ndo mtihani.nishaamua kujiajiri kuuza mboga za majani maisha yanaenda.stress zimeisha.na kaz za sensa nazo bado kimya
 
Nimekosa tena ajira ya ualimu kipindi ambacho naiihitaji mno, Pdf zima limejaa certificate na diploma sisi bachelor sjui tukale wapi?

Kungekuwa kuna namna ya kuibadilisha degree kuwa certificate ningefanya hivo ili mradi nizame ajirani.

Nimeamua kuachana kabisa na huu ujinga wa kuifikiria ajira , ngoja nipambane na mtaa kama sjawahi kwenda shule.

Naota ndoto hazina rangi ngoja niamke nizipake.
Sijawahi ona mwanachuo wa degree anakwenda kufanya field mashuleni au vyuoni.
Hivyo ndo vipimo vya kuweza kujua wewe mwalimu mtarajiwa unaupeo gani wa kufundisha.
Tulikuwa tunaambiwa wenye degree wenyewe ni kwenda moja kwa moja kufundisha secondari na vyuoni au kuwa maafisaelemu wa mikoa.
Kwa experience ipi mliyonanyo kwa elimu ya leo ambayo hata mitaala haieleweki. Labda nyinyi mliopitia huko. Wewe ungesoma diploma ukaenda kufundisha ukagain experience then ukaenda kusoma ukiwa na ajira yako tayari.
 
Back
Top Bottom