Nikiomba tena ajira niiteni mbwa nimekaa paleee

[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Maisha ya mwanaume hata raha ya kuishi huioni
 
Kama si math na physics, ama si elimu maalum, mkuu kaza kwanza mtaa sahau huku ama pata connection, mwaka 2015 hata nusu kuchukuliwa bado.
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Kwahiyo physics na mathematics ndompango mzima
 
Unapata wapi hao wanafunzi wakati ma shuleni wanaachiwa saa 11 na bado wanaitwa tena weekend na likizo
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Walimu wanafundisha non stop from morning to evening
 
Sulikuwa unalia kila siku watoe majina, Sasa majina yametoka unalia tena
 
Sasa hao wanachuo wenye degree huwa wanafanyia field wap? Kama sio shuleni mbona kama huelewi hata nini kinaendelea duniani kwa wakati huu, yani uko shallow na unajikuta unajua kila kitu,
Yani unai praise diploma over degree, ndio maana elimu yetu inakosa thamani sababu watu wanaamini diploma ndio bora kuliko degree
 
Usiikate tamaa au ukiomba usiombee degree mpendwa .kunamtu kaitimu chuo mwaka2001 ndo kapata kazi juzi kwenye tamisemi kwaiyo usikate tamaa mpendwa
 
Hii
 
Yule Mwijaku ana Masters, amejitwist kwenye uchawa kunamlipa vizuri tu.

Karibu mtaani huku ndiko kwenye matumizi ya akili na siyo vyeti.

Unapokuja mtaani vyeti vyako fungia kabatini for future use, huku walioferi darasani ndio magenius.
Degree alisoma wapi achilia mbali masters?? Nakumbuka Wakati niko Mzumbe alidisco sasa sijui alienda kusoma wapi tena..
 
History na kiswahili [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu usicheke,yauma sana sema ndio tunakaza tuu,ila ndicho kilichopo,ukisoma arts na so kingereza chance ndogo sana ila walimu wa physics na math wanamarket na wachache sana,tatizo wengi hawakufaulu vyema so wanaenda ualimu kwa kuwa hawana option
 
Tatizo tunaamini kuajiriwa mpaka serikali ,jaribu hata private huku ukijiwekeza sehemu hata ajira ikichelewa hautokua exhausted ! Tatizo kubwa linakuja ambapo unakaa macho yote yameitegemea ajira ya serikali by then wasomi wa sanaa ni wengi sana na wanaajiliwa kulingana na miaka 2015_ up to date kwa hyo nayo changamoto kwenye kuajiri kulingana na idadi na uhitaji .Endelea kuvumilia tu nafasi yako kama ipo utaajiliwa na tatizo hili huwa ni ualimu na afya maana sisi wengi wetu ni watoto wa maskini ndio huwa tunalalamika sana .
 
Private zinatofautiana nazo zina level zake,ukienda shule hasa za mission na ukapewa mkataba mbona utalipwa vizuri,wengi wetu tunaogopa zile private nzuri zenye malipo mazuri kwa sababu elimu ya sasa hivi ni voda fasta mtu anamaliza chuo hayuko competent hata kidogo kwa hyo sehemu nzuri nyingi wanatoa oral and written paper interview anaogopa hata kuattend ! Pili wakikulipa hata miezi hyo miwili mitatu unajiwekeza hata ukiwa na genge umempa mtu anakupa 2 kwa siku ukawa na uwezo wa kupata kihela cha vocha na menu utokaa kuwaza sana ajira za serikali kwa sababu serikali lazima tu itakuajiri one day.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…