Mara nyingi mtu anayefikiria dhumuni na maana ya maisha na kifo ni eidha ni masikini, ana msongo wa mawazo, shida na changamoto nyingi za maisha na upweke.
Lakini kamwe huwezi kukuta mtu mwenye maisha safi akifikiria kifo sababu muda wote atakuwa busy na kazi na kuenjoy maisha yake, matokeo yake anasahau hata kama kuna kifo.
Kufa kila mtu atakufa tu, hivyo hakuna cha kuogopa. Bali cha msingi ni nini unakiacha nyuma? Unawaachia nini kizazi na vizazi vyako? Unaacha picha gani familia yako? Kwa watoto, wajukuu na vitukuu vyako?
Kuna Familia za matajiri, zenyewe ni matajiri tu kwa mamia ya miaka kazi ni kurithishana na kuendeleza, sababu waliotangulia walitambua umuhimu wa kuacha kitu kwa ajili ya wanaokuja nao waendeleze na sio kuwa wabinafsi na kujijari mwenyewe tu kama wengi wenu humu mnaosema ("kula bata maisha mafupi haya utakufa tu mara sijui tumia pesa ikuzoee" ubinafsi wa hali ya juu)
Sasa imagine babu yako angewarithisha na angewaachia utajiri wa company za migodi na viwanda vya kufulia vyuma na kuchimba mafuta, je ungekuwa unahangaika sasa hivi? big NO.
Kifo ni inevitable.
Mimi najua kufa nitakufa tu lakini siwezi kujiachia kufanya kila uchafu na kila starehe kisa sababu nitakufa tu, hapana.
Bali nitafanya kila ninachokiweza sio kwa ajili yangu tu bali na vizazi vyangu vijavyo waje kuendeleza, sitaki kuona wanangu na wajukuu zangu wanakuwa watu wasio na umuhimu wowote popote pale au waishi kama sio chochote kazi kufuata mkumbo hapana hicho kitu sitoruhusu. labda nife sasa hivi hapa. Lakini Point ni kuacha kitu kikubwa au chochote bora nyuma kwa ajili ya vizazi vyako vitakavyo warahisishia maisha na kuwaletea fursa.
Kama babu wa babu zenu wangekuwa wapambanaji basi bila shaka msingekuwepo kwenye huu uzi.
Wengine wangekuwa maCEO, wanasiasa wakubwa, wakiwemo wa mchongo na connection mkikimbizana na mama samia, wengine mngekuwa mnagombania urithi na wengine mngekuwa nje mkisoma kwenye vyuo vikubwa kama Harvard na Oxford kwa pesa za babu au sababu babu ni mtu mkubwa mtu wa watu mwenye watu wake.
Lakini hapana mpo hapa sababu babu zenu walikuwa kama nyinyi tu. Au unadhani MO, Bakhresa na watoto wao wanafikiria kifo? big NO.
Hell, hata mimi nisingekuwepo kwenye huu uzi.
Break the cycle.