Nikiona binadamu anazikwa nachanganyikiwa mno

Nikiona binadamu anazikwa nachanganyikiwa mno

Roho haifi kinachokufa ni mwili uharibikao
Shetani amewadanga kuwa eti "roho haifi". Udanganyifu ule ule alioufanya Bustanini kwa kumwambia Eva kuwa; "ukila matunda ya mti huu hautakufa hakika bali utakuwa kama MUNGU".
Udanganyifu huu wa Shetani ndiyo unaendelea mpaka leo. Inasikitisha sana!
Soma kitabu cha Nabii Ezekieli ile aya ya 18 ndiyo utajua kuwa roho inakufa au haifi.

MUNGU hasemi uwongo hata siku moja. Tumwamini MUNGU na NENO lake maana NENO lake ni KWELI tupu.
 
Unajuaje Mungu yupo, na kwamba habari za kuwapo kwa Mungu si hadithi za uongo tu tunazohadithiana watu kwa kuwa hatuna majibu?
Ni bora kuamini kuwa Mungu yupo kuliko kutokuamini halafu mwisho wa siku unakutana na Mungu.
 
Shetani amewadanga kuwa eti "roho haifi". Udanganyifu ule ule alioufanya Bustanini kwa kumwambia Eva kuwa; "ukila matunda ya mti huu hautakufa hakika bali utakuwa kama MUNGU".
Udanganyifu huu wa Shetani ndiyo unaendelea mpaka leo. Inasikitisha sana!
Soma kitabu cha Nabii Ezekieli ile aya ya 18 ndiyo utajua kuwa roho inakufa au haifi.

MUNGU hasemi uwongo hata siku moja. Tumwamini MUNGU na NENO lake maana NENO lake ni KWELI tupu.
Unajua umechukulia hili kwa mlango wa imani moja tuu.. Dunia haina imani moja hivyo ni vema ukazisoma na tafsiri zingine juu ya kifo na roho pia
 
"kifo ni mawaidha tosha"

Sisi si kitu kabisa,ukitafakari kifo kwa umakini kabisa, kuna vitu unaweza kuacha kufanya, tuishi vyema, tutendeane mema, tupendane wazee, tuthaminiane, sote tutakufa.
 
Hakuna upweke mbaya na wa kuogofya sana kama upweke wa makaburini chini ya kifusi cha mchanga kilichisindiliwa vema hasa waombolezaji wanapoondoka makaburini na kukuacha peke yako. Hiyo ni trela tu.

Mchezo kamili ni pale kiza kinapoingia na kumbuka makaburini hakuwekwi taa labda iwe kipindi cha mbalamwezi
Siri ya kifo ni siri ya kuogofya sana maana hata my wako hawezi kulala nawe pale makaburini atabaki na walio hai wengine na hisia zake juu yako zihamie huko kwa wengine[emoji24][emoji24][emoji24]
Cha kuumiza zaidi ni kwamba haya yote unayaona kama video kwenye luninga na huna la kufanya[emoji24][emoji25]
Hapo kwenye ".....kama luninga" umetudanganya. Hakuna aliyewahi kufa akaja kutusimulia inavyokuwa. Tusubiri kuexpeerience wenyewe kuliko kudanganyana!
 
Usiogope kufa, ogopa kufa ukiwa na dhambi.
Iogope "dhambi" zaidi kuliko "kifo" maana kifo kimeletwa na dhambi.

Zishike Amri zote za MUNGU na Injili ya YESU KRISTO nawe utakuwa na amani moyoni mwako hata siku ya kufa ikifika hutakuwa na hofu yoyote maana utakuwa na uhakika wa kufufuliwa na kuishi tena katika Ufalme wa MUNGU milele na milele.

Mwenye masikio na asikie!
Ameeeeen
 
Hapo kwenye ".....kama luninga" umetudanganya. Hakuna aliyewahi kufa akaja kutusimulia inavyokuwa. Tusubiri kuexpeerience wenyewe kuliko kudanganyana!
Sikuandika ili uamini lakini bali nimeandika ninachokijua
 
ASHUKURIWE MUNGU aliefanya uwezo mkubwa wa mwanadmu kusahau mambo yatuhuzunishayoo... hakika alifanya jambo kubwa sana. Mtu akishazikwa kuna uzito huwa unapungua wa simanzi unaotufanya tuweze kusonga mbele
 
Hakuna upweke mbaya na wa kuogofya sana kama upweke wa makaburini chini ya kifusi cha mchanga kilichisindiliwa vema hasa waombolezaji wanapoondoka makaburini na kukuacha peke yako. Hiyo ni trela tu.

Mchezo kamili ni pale kiza kinapoingia na kumbuka makaburini hakuwekwi taa labda iwe kipindi cha mbalamwezi
Siri ya kifo ni siri ya kuogofya sana maana hata my wako hawezi kulala nawe pale makaburini atabaki na walio hai wengine na hisia zake juu yako zihamie huko kwa wengine[emoji24][emoji24][emoji24]
Cha kuumiza zaidi ni kwamba haya yote unayaona kama video kwenye luninga na huna la kufanya[emoji24][emoji25]
Naona tunaendelea kutishana sasa kaka mshana kila mara nawambia siri ya mtungi aijuaye kata

Mtu akishakufa mwili auelewi kitu chochote ndio mana wenzetu wahindi wanauchoma moto

Tuzungumzie roho hapo sawa walakini roho nayo aikai humo chini kaburini
 
In short hakuna anayejua mtu akifa anaenda wapi au wakati anakufa anakumbana na nini!! Kwasababu hakuna aliyekufa na akarud kutuambia hayo mambo yote, kila mtu anatakiwa kuwa na imani juu ya anachoamini na sio kuketeana story mpya au kutishana

Ishi maisha yako kufa kupo tu
 
Back
Top Bottom