Nikiona binadamu anazikwa nachanganyikiwa mno

Nikiona binadamu anazikwa nachanganyikiwa mno

Sometime huwa nawaza wale watu wazima( umri umeenda) huwa wanafikiria nini kuhusu Kifo.

Kuna Babu yangu alikua analalamika kwanini kifo kimemsahau. Alisikia mtu amefariki anahuzunika kwamba kwanini hawajakiambia kifo kimfuate, kwanini kimemsahau, au akilipe pesa kiasi Gani kimfuate upesi? Anasema kimemchukua Mke wake wakati anaona na yeye hapo macho hayaoni Bora afe tu na umri umeenda.
 
Sometime huwa nawaza wale watu wazima( umri umeenda) huwa wanafikiria nini kuhusu Kifo.
Umri unapokwenda sana unapoteza faraja mana wenzio rika lako, rafiki zako, ndugu zako, wapenzi zako asilimia kubwa wanakuwa wameshakufa unabaki na kizazi ambacho kiko tofauti na wewe, hivyo unakuwa mpweke sana hutamani tena kuwepo, ni sawa na wewe ufungiwe ndani na watoto wa miaka miwili alafu uambiwe utakaa nao hapo hapo kwa miaka kumi, do you feel what it is?
 
Hakuna upweke mbaya na wa kuogofya sana kama upweke wa makaburini chini ya kifusi cha mchanga kilichisindiliwa vema hasa waombolezaji wanapoondoka makaburini na kukuacha peke yako. Hiyo ni trela tu.

Mchezo kamili ni pale kiza kinapoingia na kumbuka makaburini hakuwekwi taa labda iwe kipindi cha mbalamwezi
Siri ya kifo ni siri ya kuogofya sana maana hata my wako hawezi kulala nawe pale makaburini atabaki na walio hai wengine na hisia zake juu yako zihamie huko kwa wengine[emoji24][emoji24][emoji24]
Cha kuumiza zaidi ni kwamba haya yote unayaona kama video kwenye luninga na huna la kufanya[emoji24][emoji25]
Exactly! It happened to me when I lost my mama, nilienda makaburini saa Saba usiku ili niprove myth busters wanao sema huwa hufufuka,niliishia kuumwa na mbu tu. RIP Mom.
 
Hakuna upweke mbaya na wa kuogofya sana kama upweke wa makaburini chini ya kifusi cha mchanga kilichisindiliwa vema hasa waombolezaji wanapoondoka makaburini na kukuacha peke yako. Hiyo ni trela tu.

Mchezo kamili ni pale kiza kinapoingia na kumbuka makaburini hakuwekwi taa labda iwe kipindi cha mbalamwezi
Siri ya kifo ni siri ya kuogofya sana maana hata my wako hawezi kulala nawe pale makaburini atabaki na walio hai wengine na hisia zake juu yako zihamie huko kwa wengine[emoji24][emoji24][emoji24]
Cha kuumiza zaidi ni kwamba haya yote unayaona kama video kwenye luninga na huna la kufanya[emoji24][emoji25]

Nilichogundua tunaogopa zaidi kifo ni sisi tulip hai tukiwaza jinsi msiba unavyokua Kwa walioachwa na kushuhudia maandalizi ya mpendwa wenu akiagwa na kuhitimisha safari yake.

Sifikirii aliyefariki anakua na Hali tunayoifikiria sisi, huenda anaanza ngwe nyingine kabisa ya maisha hata Hana Tena habari ya Mke, watoto, ndugu au jamaa amewaacha huku duniani, utaona kwamba tunaokiogopa kifo ni sie tulio hai kuliko hata wafu.

Kinachotusumbua ni Ile ntawaachaje wanangu, wataishije, Mke/ Mme wangu ataishije, nnaviachaje vitu nnavyovopenda, maisha yatakuaje na Nini litatokea baada ya kifo.
Kwa kuwa hiyo ni njia yetu sote, nimejikuta siku hizi siogopi mambo ya kifo, na alipofariki Baba ndio nikaona kumbe yeyote anaweza kufariki muda wowote!

Kitu kimoja Cha msingi, kutokugombana na watu Kwa vitu vya kupita, turaacha Kila kitu, hauendi na magari, nyumba, au pesa zozote, unazikwa kwenye eneo dogo sana. Sisemi usitafute maisha, la hasha, nnachosema harakati za maisha zisikufanye ukashindwa kuishi na kuifurahia maisha ya Sasa Kwa hofu ya maisha yajayo. Usikwaruzane na watu kama hakuna ulazima ikavuruga amani na furaha yako.

Paula Paul hakuna haja ya kuogopa sana " it couldn't have been better"
 
Alafu zile Stori za eti anakuja malaika anakutoa roho huku unaona video ya maisha yako ni uwongo mtupu na kutishana kusiko sababu.unaambiwa roho inavyotoka maumivu yake Bora uminywee pu**[emoji28] au afadhali maumivu ya kujifungua Kwa wanawake yanaanzia kwenye vidole kisha yanapanda Hadi utosini wakati roho inatoka

Wakati ukiweka zako jiko la mkaa chumbani kisha ukafunga madirisha na mlango unakufa Kama umelala,kimya kimya burudaani kabsa[emoji1] Tunatishana Sana
Is a myth, Nani kakudanganya kuwa alitolewa roho Kisha ikarudishiwa Tena then aje atuhadithie?
 
Poleni sana na majukumu.

Nikiona watu wanachimba kaburi then kumfukia binadamu mwenzangu navurugwa sana kichwani. Nafikiria mambo mengi mno... Mbaya zaidi azikwe mtu ambaye namfahamu.

Nikienda makaburuni makaburuni na kutizama namna udongo unavyotumeza, inasikitisha na kufikirisha mno.

Maisha baada ya kifo ndio swali zito sana linalonijia kichwani mwangu.

Unafukiwa, unaoza na kuwa udongo. Feeling yake unapokufa pia inatafakarisha sana.

Kweli siri ya maiti iajuaye kaburi.

Tutende mema wakati wote jamani.
Usiogope kufa, ogopa kufa ukiwa na dhambi.
Iogope "dhambi" zaidi kuliko "kifo" maana kifo kimeletwa na dhambi.

Zishike Amri zote za MUNGU na Injili ya YESU KRISTO nawe utakuwa na amani moyoni mwako hata siku ya kufa ikifika hutakuwa na hofu yoyote maana utakuwa na uhakika wa kufufuliwa na kuishi tena katika Ufalme wa MUNGU milele na milele.

Mwenye masikio na asikie!
 
Kimwili sawa lakini sio kiroho

Mhubiri9:4-5- Nilitafakari juu ya hayo yote, nikaona kwamba Mungu anaongoza ... 5. Maana, walio hai hujua ya kwamba watakufa, lakini wafu hawajui chochote.
 
Hakuna upweke mbaya na wa kuogofya sana kama upweke wa makaburini chini ya kifusi cha mchanga kilichisindiliwa vema hasa waombolezaji wanapoondoka makaburini na kukuacha peke yako. Hiyo ni trela tu.

Mchezo kamili ni pale kiza kinapoingia na kumbuka makaburini hakuwekwi taa labda iwe kipindi cha mbalamwezi
Siri ya kifo ni siri ya kuogofya sana maana hata my wako hawezi kulala nawe pale makaburini atabaki na walio hai wengine na hisia zake juu yako zihamie huko kwa wengine[emoji24][emoji24][emoji24]
Cha kuumiza zaidi ni kwamba haya yote unayaona kama video kwenye luninga na huna la kufanya[emoji24][emoji25]
Wafu hawajui kitu chochote wala hawana kumbukumbu wala ufahamu wa kitu chochote.

Ukifa umekufa, unakuwa haupo kabisa. Ni kama kipindi kile haujazaliwa wala mimba yako haijatungwa, ulikuwa haupo. Vivyo hivyo na baada ya kufa.

MUNGU alimwambia Adamu; "uu mavumbi wewe na mavumbini utarudi ulimotwaliwa".

Hii maana yake ni kwamba kabla ya Afamu kufanywa kiumbe hai alikuwa ni mavumbi yasiyokuwa na uhai. Hivyo basi mtu akifa anarudi kuwa mavumbi yasiyokuwa na uhai wala ufahamu.
 
Roho haifi kinachokufa ni mwili uharibikao
 
Wafu wa mwili sio wa roho.. Roho haifi
Nani kakudanganya kuwa Mwanadamu ana roho isiyokufa?

Ezekieli 18:20 imeandikwa hivi; "roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa".

Tena fahamu kwamba roho ya mwanafamu haiwezi kuwa hai pasipokuwa na mwili ulio hai. Ingelikuwa roho hazifi basi MUNGU asingeweka siku ya ufufuo. Angezihukumu roho bila miili. Lakini roho bila mwili hakuna uhai na ndiyo maana imetengwa siku ya ufufuo ambapo wafu wote watafufuliwa(watarudishiwa uhai) na kuhukumiwa kila mmoja kwa kadiri ya matendo yake.
 
Back
Top Bottom