Point namba moja imejibu hoja zako
Sera zangu hizi hapa na hizi ni hints amabazo zipo kwenye video A) maelezo yangu binafsi Mimi ni nani??? Nimezaliwa lini??? Nimezaliwa wapi??? Elimu yangu??? B)mambo ntakayotekeleza nikiwa Rais Mambo ntakayotekeleza nikiwa Rais wa Tanzania kwenye video nimeelezea kwa undani Viwanda vya...
www.jamiiforums.com
Robert, nimepitia hoja zako za utafanya nini, naona ya kwamba zinahitaji msasa mkubwa kwasababu zimekaa kama mtu anayetaka kujifanyia make up, nunua powder, nunua mafuta etc etc na unajua ya kwamba make up ya mwanamke huwa haidumu hata masaa 24, maana yake ni aina fulani za mikakati ambayo sio sustainable. Na bila sustainability sahau uchumi ambao ni sustainable unaokua kwa 12% annually.
Hizi sera zako nimezi copy embu dadavua kila moja kwamba itaongeza vipi uchumi ukimulika cost benefit analysis ya kila moja, maana naona ni kama umeweka tu mambo bila basis wala ku consider structure ya uchumi wa Tanzania.
Viwanda vya awali
Kuzalisha megawatts 200,000 za umeme
Kusambaza mabomba ya gesi
Kupima nchi nzima
Kuboresha elimu ya msingi
Kuwapeleka wale wote waliofeli form four veta
Kuwa na tozo (fee) moja ya utalii
Kuboresha michezo
Kuanzisha mashindano ya tennis
Kuanzisha mashindano ya diamond league
Kuondoa squatter
Huduma za dialysis bure
Kupunguza kodi
Kupunguza na kufuta tozo kwenye miamala ya benk na simu
Kutengeneza artifical ozone layer
Kuzalisha dawa Tanzania
Kutengeneza mazingira ya viwanda vya satellite, rockets na ndege
Baadhi ya wafanyakazi wa taasis za serikali kuwa na mikataba ya miaka 15