Niko Kigoma, kweli sura siyo roho

Niko Kigoma, kweli sura siyo roho

Gharama za maisha ziko chini ukilinganisha na wapi? Maskini gani anaweza kulipia migebuka kwa 25000 hotelini? Nguo dukani ziko juu sana tofauti na kwingine. Kifupi,gharama za maisha Kigoma ziko juu sana isipokuwa nauli za treni daraja la tatu C
Acha uongo wewe hoteli gani kigoma wanakouza mgebuka 25000? Gharama ya nguo dukani ni kama sehemu zingine tuu t-shirt na jeans ni kati ya 18-25 ukisema kigoma maisha gharama sana na wanao ishi Arusha wasemaje ? Acha kudanganya watu
 
Kwa mara ya kwanza nimekuja Kigoma baada ya miaka 25. Nimeshangaaa sana. Kigoma si mbaya kihivo kama ilivo jina lake, na kama binafsi nilivokuwa naichukulia iko tu kama mikoa mingine Kama Sumbawanga, Lindi, Tabora au Ruvuma na Shinyanga.

Kifupi Kigoma haina sura mbaya hivyo inayoonekana. Ila pia kuna vitu ni gharama haka kamkoa
1. Juice ya muwa 1000. Kaah hiki ni kitu nimeshindwa kushangaa
2. Wali maharage elfu mbili. Nimeshtuka sana
3. Wali mgebuka elf 10 na ziwa tanganika lipo nyuma tu
So labda ukale migahawa ya kajambanani

Mji umepoa kama uji, pia nimepita anapoishi Mwijaku kaaah ni haki watu wa huku wawe na midomo sana!! Kwa bei hizi za vyakula lazma uwe tu mpigania uhuru wa chakula.
Jakaya Kikwete aliibadili Kigoma ikawa Dubai! Watanzania tuko kama vitoto vidogo, yaani mtu anakuambia ukinichagua nitapageuza hapa pawe kama Dubai, nawe kwa ujinga wako unamchagua!
 
Acha uongo wewe hoteli gani kigoma wanakouza mgebuka 25000? Gharama ya nguo dukani ni kama sehemu zingine tuu t-shirt na jeans ni kati ya 18-25 ukisema kigoma maisha gharama sana na wanao ishi Arusha wasemaje ? Acha kudanganya watu
Asante mkuu maana unaijua sana Kigoma! Nenda Mwitongo hotel, Migebuko na sato 25,000, ingia Metro bar kuhe 30,000. Kaulize t shirt/jinsi/mikanda 35,000 mpaka 40,000. Hizo ni bei za May 15, 2024 Kigoma mjini
 
Nimeishi Moshi na Arusha na pia nimetembea mikoa mingi ya Tanzania, maisha ya Kigoma yanahitaji maombi
 
Asante mkuu maana unaijua sana Kigoma! Nenda Mwitongo hotel, Migebuko na sato 25,000, ingia Metro bar kuhe 30,000. Kaulize t shirt/jinsi/mikanda 35,000 mpaka 40,000. Hizo ni bei za May 15, 2024 Kigoma mjini
Hakuna hoteli yoyote maarufu ambayo sijaingia kigoma hizo bei za chakula na nguo ni zako usidhani wewe pekee ndio umefika mwisho wa reli
 
Back
Top Bottom