Niko na shida nahitaji kumbadilisha jina mwanangu kutoka Samia kuwa Amina, Utaratibu ukoje?

Mashamba Makubwa Nalima

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2024
Posts
4,978
Reaction score
2,411
Kiufupi baada ya kupata mtoto wangu 2021 nilimpa Jina la Samia kutokana na mafanikia ya bi mkubwa mmoja mtaani ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza pale mtaani kuwa na Master of Science in Computer Science, lakini namna alivyokuwa ghafla hizi siku za karibuni, siamini kama anaweza kuwa mfano mzuri kwa mwangu tena na najilaumu kwa kurupuka kufanya maamuzi hayo.

Ningeomba mtu mwenye uelewa wa namna za kubadilisha majina la mwanangu kutoka Samia kwenda Amina.
 

Lucas, Tlaatlaah kunatakikana mwongozo huku
 
Nenda mahakamani utaapa na kubadili jina.
Ila sidhani jina linaumba hulka ya mtu kwani Steve Nyerere angekuwa na akili nje ya uchawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…