Niko njia panda msaada

Niliwaambieni.
Oa rafiki yako unayemjua siku nyingi.
Oa mtu msiezidiana Sana kiuchumi.
Oa mtu msiezidiana Sana kiumri.
Oa mwanamke anaye kuheshimu. If you can marry your childhood friend, please do. Ikibidi oa mtu wa kwenu, sio umetokea Rombo huko ndaaani ndani unakutana na pisi lakimakonde au hata kimachame unatañgaza ndoa.
Umekutana na jimwanamke Lina tako unatañgaza ndoa unadhani umeoa?
Kwanza Ile mitako hua Ni mavi tu yamejaa mle, hakuna kitu.
 
Mkuu kwanz sidhani kama uyo mwanamke, anakupenda mpaka alipofikia shukuru kwa hiyo roho ya uvumilivu ulonayo toa copy hilo kadi linatosha kuwa ushahidi mpeleke kwao kwa amani tu mwaga kila kitu hadharani na umuache hapo atakuja kukupa kesi uyo.
 
Kama unaishi kwenye nyumba yako mtimue bila kupepesa macho. Kama ni nyumba ya kupanga kimbia mwache hapo bila kumwambia chochote. Usimuonee huruma.
 
Busara hii.
Azingatie huu ushauri.
 
Ona mwenyewe kama unaweza kuvumilia hali hiyo (mtu mwingine asikuingizie mawazo yake).
Hili nalo ni Jambo la msingi.
Lakini huoni huyo mwanamke amejiandaa kutaka kuishi na mchepuko wake?

Kwanini asikie wivu mchepuko kubariki ndoa na mwanamke mwingine wakati yeye yupo kwenye ndoa na mtu mwingine?

Kwanini kadi ya clinic aandike jina la mchepuko Kama lengo kulikuwa kupata mtoto sababu mumewe hatungishi mimba?
 
Imekuaje Hadi impeleke mkeo kutafuta mtu wa kumbebesha mimba ?¿. Ebu angalia na huyo first born isije ikawa nalo ni goal la kupewa.
 
Siku ya kwenda kumpeleka kwao ambatana na fuso la vitu vyake vyote mpaka kwao
 
kua mpole ukimpleleka kwao peleka na vitoto vyote then hukohuko muite mama yake na ukooo onesha ushahidi then sepa tafuta mwingine n.b km simu ulinunua wewe mpokonye
 
Piga chini.
 
Kapime DNA huyo wa kwanza...
Alafu fukuza huyo mwanamke haraka sana,
Anza kutafuta watoto na wanawake wengine, fanya maamuzi ya kiume
 
pole sana,hili suala usisubiri kitu ni hatari sana,mpeleke kwao kwa wazazi wake,ita viongozi wa dini,limwage na uwaambie hapo ndio mwisho nae.Anza life upya,nisikilize mdogo wangu,hili ni jambo hatari sana
 
Mimi nimetoa ushauri wangu na ushauri uko based on taaluma ya "counselling". Kwamba unapomshauri mtu lengo lake siyo kumwambia aamue nini kuhusu, mfano, ndoa yake. Yeye ndiye mwenye ndoa na ndiye anayeamua. Kama lengo si hilo ushauri maana yake ni nini? Ni kwamba, mwomba ushauri kuna mambo yamemchanganya (yamechanganyikana), mshauri anatakiwa amchanganulie/ayachambue. Ni kama kusema alphabets A-Z zimechangantikana na mtu anaomba uziweke vizuri tena ili apate kuona mpangilio wake. Mimi nilichokifanya ni kuweka katika utaratibu huu: A,B,C,D, etc na kumwachia mhusika achague alphabets anazotaka. Wewe unachotaka ni mimi nimwambie "chagua C, X na Y ndizo zinazokufaa." Sasa huu siyo ushauri, bali ni kumchagulia mtu afanye nini katika shida yake. Hilo si jukumu la mshauri, jukumu la mshauri ni kutoa mwanga na kumwacha mhusika achague mwenyewe. Ukisoma counselling utapata counselling skills na utawasaidia watu wengi namna ya ku'deal' na matatizo yao na siyo kuamua wayatatue namna gani. Kwani nani huwa anakuamlia wewe namna ya kutatua matatizo yako? Huwa unayatatua wewe mwenyewe au watu wengine ndio huwa wanakutatulia matatizo yako? Kama huwa unayatatua mwenyewe, kwa nini unataka huyu ndugu umtatulie wewe tatizo lake? Linakuhusu? Umesikia pia upande wa pili unasemaje au umeamini for granted alichosema huyu ndugu? Haya ni maswali ya kujiuliza unapotoa au ombwa kutoa ushauri na usiegemee upande mmoja to the detriment of the other side. Huo ndio ujumbe wangu.
 
Pole sana Brother. Hongera pia kwa utulivu na uvumilivu.

Huyo mwanamke wako amefikia Kiwango cha juu kabisa cha dharau kwako, amekushusha kuliko unavyofikiria.

Cha kufanya kwa sasa nakushauri mpe muda ajifungue mpeleke kwao na ukishamfikisha huko hakikisha akishajifungua humhudumii tena kwa chochote.

Kwa sababu ushahidi unao mwambie tu ulikua unajua tangu siku ya kwanza ila uliona usimbugudhi , mfungukie kwa uwazi kisha achana nae kwa manai. USIJE UKAMWELEZA MTU YEYOTE SABABU YA KUACHANA NAE, HATA MAMA YAKO AU AMMA YAKE WALA MSHENGA.
 

Ukimpeleka huko kwao ndio iwe talaka yake hiyo, aishie huko huko...
 
Kuanzia hapo no 4 na 5 umepuyanga aisee,hivi unaanzaje kuishi na mwanamke wa hivyo?,hata kama unampenda
Wewe usiyepunyanga, nikuulize: je, umesikia pia upande unaolalamikiwa na kusikia unasemaje au unatoa hukumu kwa kusikia tu upande mmoja na kuamini kwamba mke wake ndiye kakosea? Kwenye ishauri wangu, nimeamua kuwa neutral, nimejaribu kuweka hivyo kumwachia mhusika aamue mwenyewe na siyo nimwambie mimi. Kama ambavyo sikumwamlia amwoe mke wake, hivyo pia siwezi kumwamlia amwache mke wake. Uamuzi ubaki kwake - aamue afanye nini (isipokuwa asiamue kumdhuru mke wake).
 
Ndugu, kama huna ushauri kaa kimya. Usimhukumu mtu. Umesikia tu maneno ya upande, ni unfair kudhani mke wake kakosea kabla ya kumsikiliza. This is unethical!
 
Ndugu, kama huna ushauri kaa kimya. Usimhukumu mtu. Umesikia tu maneno ya upande, ni unfair kudhani mke wake kakosea kabla ya kumsikiliza. This is unethical!
Mkuu yeye alisema amepata ushahidi kwenye simu yake na kila kitu kiko wazi wapi mimi nimemhukumu? huo ndio ushauri wangu toa na wa kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…