Niko polisi imepigwa filimbi ya kushusha bendera watu wote wakasimama! Hii maana yake nini?

aise

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2018
Posts
5,175
Reaction score
16,488
Habari za jioni wakuu!

Niko polisi hapa kituo ambacho kipo karibu na soko! Imepigwa filimbi na watu wote wamesimama mpaka jamaa kamaliza kushusha bendera akapiga tena filimbi ndiyo watu wakaendelea na mishe!

Hivi huu si utumwa?

Maana yake nini kwa kizazi cha leo?

Mimi yote hayo yakiendelea nilikuwa nimekaa tu naperuzi!

Naweza kushtakiwa kwa kosa gani?

Nauliza maana nahitaji kujifunza zaidi, nikiwa shule ya msingi tuliwahi kufundishwa hili ila nimesahau maana yake!
 
nina kuuliza maswali matatu...
swali la kwanza, nini maana ya uzalendo?
swali la pili kati ya marekani ni tanzania unaipenda nchi gani?
Swali tatu, Ukiambiwa uishi tanzania na marekani utachagua nchi gani?
Nabashiri majibu yako.
1. sijui
2. marekani
3.marekani
kama majibu yako ni hivyo, basi ndio maana umefungua uzi wa kipuuzi namna hii ewe mtanzania usieheshimu nchi yako.
 
Kuna siku isio na jina utajichanganya TU Ndio utajua ni HARAMU au HALALI

UTII wa bendera ya nchi na wimbo wa Taifa unafundishwa kuanzia shule ya Msingi sasa sijui mwenzetu umesomea Kenya au ulaya

Na kuhusu vifungu usijali utatafutiwa pale ambapo taya ya juu na chini vikiwa havina uhusiano mdomo wa juu upo kulia wa chini upo kushoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…