Niko polisi imepigwa filimbi ya kushusha bendera watu wote wakasimama! Hii maana yake nini?

Niko polisi imepigwa filimbi ya kushusha bendera watu wote wakasimama! Hii maana yake nini?

Unasimama for motherland, ni alama ya taifa hio
Nitasimama leo
Kesho
Na kesho kutwa.

This is motherland.
Kama ulifundishwa na umesahau rudi shule, au omba madogo wa darasa hilo wakupige msasa.
Ni protocol...bendera ya Taifa ni alama ya Taifa,heshima kwa bendera ni heshima kwa Taifa lako. Ni sheria kusimama wakati bendera inashushwa,kupandishwa au kama inapita mbele yako.
HUU UTARATIBU ULILETWA NA NANI?
 
Utaratibu wa kishezi na utumwa hauna maana wala mantiki yeyote, unatii benders kushushwa halafu rasilimali za taifa zinaibiwa na kifaidisha familia za watu wachache.

Unafiki na uzandiki umetamalaki hamna uzalendo hapo.
 
Habari za jioni wakuu!
Niko polisi hapa kituo ambacho kipo karibu na soko! Imepigwa filimbi na watu wote wamesimama mpaka jamaa kamaliza kushusha bendera akapiga tena filimbi ndiyo watu wakaendelea na mishe!

Hivi huu si utumwa?
Maana yake nini kwa kizazi cha leo?
Mimi yote hayo yakiendelea nilikuwa nimekaa tu naperuzi!
Naweza kushtakiwa kwa kosa gani?
Nauliza maana nahitaji kujifunza zaidi, nikiwa shule ya msingi tuliwahi kufundishwa hili ila nimesahau maana yake!
Wengine tupo mbali na hicho kituo ilipopigwa flilimbi. Ebu ingia hapo kituoni uwaeleze hii habari halafu utupe majibu badala ya kutuuliza ambao hatupo hapo.
 
Kuna siku isio na jina utajichanganya TU Ndio utajua ni HARAMU au HALALI

UTII wa bendera ya nchi na wimbo wa Taifa unafundishwa kuanzia shule ya Msingi sasa sijui mwenzetu umesomea Kenya au ulaya
Yeye anaona ni ujanja kutosimama, siku akidakwa akawekwa lupango kwa kosa la kipuuzi kama hilo ataishia kutukana na kulalamika.

Ujuaji mwingi huponza.
 
Siku nyingine wewe jifanye Chizi bendera ikiwa inashushwa nenda kazuie isishushwe yaan usisimame anzisha vagi nenda kazuie Askari asishushe bendera hapo ndio utaelewa kwanini kwenye zile jezi zao wanavaaga filimbi upande wa KUSHOTO na utajua pamoja na kwamba wanazivaa zile filimbi Ila hawazipulizi ovyo ovyo usipokua kwa tukio maalumu tu
 
Habari za jioni wakuu!
Niko polisi hapa kituo ambacho kipo karibu na soko! Imepigwa filimbi na watu wote wamesimama mpaka jamaa kamaliza kushusha bendera akapiga tena filimbi ndiyo watu wakaendelea na mishe!

Hivi huu si utumwa?
Maana yake nini kwa kizazi cha leo?
Mimi yote hayo yakiendelea nilikuwa nimekaa tu naperuzi!
Naweza kushtakiwa kwa kosa gani?
Nauliza maana nahitaji kujifunza zaidi, nikiwa shule ya msingi tuliwahi kufundishwa hili ila nimesahau maana yake!
Usijaribu ukiwa LUGALO hosptari utajuta
Mm nilikuwa nimesahau hayo mambo
Nilikuwa pale LUGALO HOSPTARI kama miaka 10 nyuma hivi eeeh mm nikawa natembea na zangu sina habari
 
Siku Moja yalinikuta morogoro!sikuisikia hiyo filimbi!
Baaada muda nikawekwa chini ya ulinzi,nikatiii.pona pona yangu ilikuwa vitambulisho vyangu,[emoji23] tukaishia kupeana mikono.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Habari za jioni wakuu!
Niko polisi hapa kituo ambacho kipo karibu na soko! Imepigwa filimbi na watu wote wamesimama mpaka jamaa kamaliza kushusha bendera akapiga tena filimbi ndiyo watu wakaendelea na mishe!

Hivi huu si utumwa?
Maana yake nini kwa kizazi cha leo?
Mimi yote hayo yakiendelea nilikuwa nimekaa tu naperuzi!
Naweza kushtakiwa kwa kosa gani?
Nauliza maana nahitaji kujifunza zaidi, nikiwa shule ya msingi tuliwahi kufundishwa hili ila nimesahau maana yake!
Aisee, hata hilo hujui?
 
Siku Moja yalinikuta morogoro!sikuisikia hiyo filimbi!
Baaada muda nikawekwa chini ya ulinzi,nikatiii.pona pona yangu ilikuwa vitambulisho vyangu,[emoji23] tukaishia kupeana mikono.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Ulikuwa kambi ipi ya jeshi hapo Morogoro?
 
Siku nyingine ukisikia sauti ya filimbi ni mda wa kuchimba dawa...mtafute polisi yeyote mwambie akuelekeze choo kilipo
 
Enzi za shule pale Bwiru Boys tulikuwa tunawadunda watu kama nyie.tuko palade filimbi ya kupandisha au kuishusha bendera inapigwa wewe unaendeleza mbaliga zako sawa ngoja ishuke na ipigwe nyingine ya mwisho uone kama hatujakulalua.
 
Hizo ni Alama ya uhuru wa nchi lazima iheshimiwe kwa bahati mbaya kwa tz watu hawajui maana ya kuwa huru maana waliupata uhuru kwenye sahani nyeupe
Hofu ni siku ukiwa kiongozi utadharau mambo mengi sna ya kitaifa
 
Back
Top Bottom