Niliacha kushabikia mpira nilipobaini Mpira unageuza Watu Wachawi!

Niliacha kushabikia mpira nilipobaini Mpira unageuza Watu Wachawi!

Ila ushabiki wa mpira unataka roho ya chuma jamani, ukiwa na moyo mwepesi unaweza kufa kwa presha.

Mi nakumbuka mwaka fulani nilikuwa na rafiki yangu tukaenda kibanda umiza kuangalia mechi ya Man Utd Vs Tottenham, jamaa alikuwa shabiki sugu wa Man Utd.Ile siku Manchester ilichapwa kichapo kizote. na Tottenham jamaa akalia machozi Hadi nikamhurumia.

😂😂😂
Ni kama mambo ya Imani. Unaumi utadhani timu ya Babaako bhana
 
Mimi sio mshabiki kabisa ila nashangaa sna inakua vipi kijana wa Leo mtanashati au binti mrembo tu ana shabikia Yanga !!!!!!!
 
Tumepumzika kidog , Kwa vile hawajaisha tutaresume Kati ya October na December mana atapekechwa mwingine

😂😂
Adui WA watanzania ni watanzania wenyewe.
Mbaya zaidi mtanzania anaungana na adui kuiangamiza nchi yake.
Ubinafsi ni kitu kibaya Sana
 
Alafu nilikuwa sina bahati, kila nitakapokaa kuangalia Mpira hasa Ile ya saa nne, kipindi kile Liverpool inahali mbali, lazima ifungwe.
Sasa hivi mkuu unapitwa uhondo! Tuko tunamkimbiza Man U kwenye top 4 ni hatari! Tumeshinda game 7 mfululizo!
 
Asalamu alyekum!

Niliacha kushabikia mpira miaka 10 iliyopita Baada ya kugundua kuwa Mpira unanigeuza kuwa wanga, mchawi na mwenye Roho ya husda.

Nilikuwa Mshabiki wa Simba Kwa timu za ndani, Huko Ulimwenguni nilikuwa Mshabiki wa Liverpool. Lakini nikaja kugundua kila timu pinzani(namaanisha Yanga) ikishinda Roho inaniuma Sana, Kwa kweli Ile hali haikunivutia kama kijana mdogo enzi zile.
Haiwezekani Mafanikio ya mwingine ATI roho iniume, inafikia hatua ninaomba kabisa Wasishinde na wasiende Mbele.

Haiwezekani Yanga akishindwa ati ninafurahi, ninachekelea na Kupata Amani ya Moyo. Tayari niliona ugeni Mpya katika moyo wangu ambao nilipojitathmini niliamua kuwa ni lazima nichukue hatua ya kuondokana na Uchawi(kutofurahia Mafanikio ya wengine)
Nikaamua kuachana na kushabikia mipira, haikuwa kazi rahisi Kutokana na mazoea lakini niliweza.

Nilikuwa Huru, sio mchawi tena. Simba ashinde au Yanga ashinde kwangu ni pouwa! Ninaangalia Mpira kama burudani na sio kama Mshabiki.

Yanini Kujiumiza? Yanini kuwa Mchawi na umri huu. Kiufupi Mpira haunisumbui asilani. Ninaweza kulala Kwa raha na wala sio mtu wa kufuatilia mipira kabisa, yapo mambo ya kuninyima usingizi, yapo mambo ya kuutesa moyo wangu. Lakini Kwa Mpira nilikataa.
Yaani mwingine afanikiwe Mimi nitumie, hiyo nilikataa.

Nimemaliza,
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kwa hiyo sisi tufanyeje sasa?
 
Back
Top Bottom