Niliacha kwenda kanisani baada ya kuona makanisa yanafungisha ndoa za jinsia moja kwa kigezo cha human rights, huku yakipinga ndoa za mitala

Hakuna kitabu cha Biblia ila kipo cha injili ambacho ndicho yesu alipewa ,Biblia ni nakala zilizochakatwa na wazungu kwa maslahi yao Binafsi fungua macho na moyo Uuone ukweli na Haki
Yesu alipewa kitabu ?

Tupe source ya taarifa zako .

N:B Source isiwe kitabu kilichokuja miaka 600 baada ya Yesu
 
Samahani mkuu sipingi unalosema ila nimeona niliweke sawa.
Ukristo haukubaliani na maovu yaani uvunjaji wa sheria za Musa (amri kumi za Mungu.) Ila ukristo unatufundisha kuwa hakuna binadamu mwenye haki aliyeweza kumpendeza Mungu kwa kutenda na kuzifuata amri kumi za Musa. Binadamu si mkamilifu ni dhaifu. Kila muda anatenda maovu iwe ni kwa maneno, mawazo au vitendo.
Hatuingii mbinguni kwa matendo isipokuwa kwa Imani ktk Yesu kristo.
Pia usisahau kuwa Imani bila matendo ni imani mfu!
Tumaini la mkristo lipo ktk Kristo.
Mkriso hajafutiwa dhambi ila akitubu na kuungama kwa mwenyezi Mungu kupitia kristo atasamehewa dhambi zake.
Yesu Kristo ktk maandiko anaitwa Mpatanishi
Mkuu ninakubaliana na wewe 90% kwa sababu umeongelea suala la kufanya toba kwa kua binadamu si mkamilifu.Sikubaliani na wewe 10% kwa kusema Yesu ni mtu pekee ambaye atafanya mimi kusamehewa na Mungu.Mitume(manabii) wote wa MWENYEZI MUNGU wakiwemo Abraham,Yesu Muhammad n.k ni wapatanishi kwa misingi ya kuleta habari za kumjua MWENYEZI MUNGU na ni hivyo tu lakini katika imani yangu mimi baada ya kumjua MWENYEZI MUNGU,toba ninamfanyia MUNGU wangu pasipo kumshirikisha mtu yoyote yule. Simshirikishi Ibrahim,Yesu, Muhammad,mtakatifu Paulo Wala yeyote yule.Toba yangu ni kwenda kwa MWENYEZI MUNGU moja kwa moja.

Rafiki yangu ukweli ni huu: mkristo na muislamu hawatokuja kukubaliana 100% kwa sababu ya tofauti za kiimani.Wewe unaamini Yesu alikufa msalabani kwa ajiri ya ondoleo la dhambi zako ilhali mimi ninaamini Yesu hakufa msalabani bali Mwenyezi Mungu alimchukua kwenda mbinguni na yule aliyesulubiwa hakuwa Yesu bali alifanana na Yesu.Kitendawili cha mzizi huu ni hiki:kabla mnaosema yeye ni Yesu kukamatwa alikwenda kusali akasemaje?Ewe baba kama inawezekana hiki kikombe kiniepuke bali mapenzi yako yatimizwe(sija nukuu ila theme inajitosheleza) hivyo basi waislamu tunatumia mstari huu kama reference kusadifu Quran kua Yesu aliepushwa na sulubu ya msalaba kama alivyoomba hivyo Mungu alimuokoa.
Ila ninyi wakristo mnatumia mstari huo hususani "bali mapenzi yako yatimizwe.."mkisadifu Yesu alikua na utayari wa kusulubiwa ili kutimiza maandiko.

Hivyo rafiki kaa ukijua hatuwezi afikiana 100% kwa sababu ya imani tofauti.Mimi nilikua mkristo ila sasa ni muislamu kwa sababu ya imani yangu na wewe ukristo ni imani yako.Hivyo kila mtu abaki na imani yake.
 
Wewe muislamu, Mimi mkristo ni imani mbili tofauti. Tushirikiane ktk kutenda mema, mengine tuzidi kujifunza.
 
Hakika kaka🤝.Hiki ni kitu huwa ninakitafuta siku zote katika jamii yetu.
Huku ukiendelea kutenda mema pia endelea kujifunza kuhusu Kristo.
Mengi utayajua kuhusu Yesu kristo ambayo hukuwah kuyajua kabla. Na ni vyema ukaanzia hukohuko kwenye Qur'an nayo pia imemuelezea Yesu vizuri tu ikionyesha ukuu wake tofauti na manabii /mitume wengine.
 
Mkuu mimi nilikua mkristo ila nimebadilisha dini na kua muislamu.Wazazi wangu wote ni wakristo na tupo jirani na kanisa ambalo nilibatizwa ila imani yangu haijawai kubali mafundisho ya kikristo.
 
Sawa, ila usichoke kuzidi kujifunza
 
Mkuu ninakubaliana na wewe 90% kwa sababu umeongelea suala la kufanya toba kwa kua binadamu si mkamilifu.Sikubaliani na wewe 10% kwa kusema Yesu ni mtu pekee ambaye atafanya mimi kusamehewa na Mungu.Mitume(manabii) wote wa MWENYEZI MUNGU wakiwemo Abraham,Yesu Muhammad n.k ni wapatanishi kwa misingi ya kuleta habari za kumjua MWENYEZI MUNGU na ni hivyo tu lakini katika imani yangu mimi baada ya kumjua MWENYEZI MUNGU,toba ninamfanyia MUNGU wangu pasipo kumshirikisha mtu yoyote yule. Simshirikishi Ibrahim,Yesu, Muhammad,mtakatifu Paulo Wala yeyote yule.Toba yangu ni kwenda kwa MWENYEZI MUNGU moja kwa moja.

Rafiki yangu ukweli ni huu: mkristo na muislamu hawatokuja kukubaliana 100% kwa sababu ya tofauti za kiimani.Wewe unaamini Yesu alikufa msalabani kwa ajiri ya ondoleo la dhambi zako ilhali mimi ninaamini Yesu hakufa msalabani bali Mwenyezi Mungu alimchukua kwenda mbinguni na yule aliyesulubiwa hakuwa Yesu bali alifanana na Yesu.Kitendawili cha mzizi huu ni hiki:kabla mnaosema yeye ni Yesu kukamatwa alikwenda kusali akasemaje?Ewe baba kama inawezekana hiki kikombe kiniepuke bali mapenzi yako yatimizwe(sija nukuu ila theme inajitosheleza) hivyo basi waislamu tunatumia mstari huu kama reference kusadifu Quran kua Yesu aliepushwa na sulubu ya msalaba kama alivyoomba hivyo Mungu alimuokoa.
Ila ninyi wakristo mnatumia mstari huo hususani "bali mapenzi yako yatimizwe.."mkisadifu Yesu alikua na utayari wa kusulubiwa ili kutimiza maandiko.

Hivyo rafiki kaa ukijua hatuwezi afikiana 100% kwa sababu ya imani tofauti.Mimi nilikua mkristo ila sasa ni muislamu kwa sababu ya imani yangu na wewe ukristo ni imani yako.Hivyo kila mtu abaki na imani yake.
hongera kwa kuujua ukweli na kuifuata dini ya haki

Allah akuongoze katika njia iliyo ya sawa
 
Wazungu waliotuletea dini, huko kwao makanisa yanageuzwa kuwa bar.

Wengi wameacha kusali, hawaendi tena makanisani, ule moto wa injili uliokuwa ukiwaka ndani yao sasa umepoa kabisa, na jivu lake limekuwa la baridi kabisa.

Huku kwetu Tanzania, wengi hawaendi kanisani labda kwasababu ya ubize na sababu nyingine.

Nikiwa mu Anglikana, nilisikitika kwa kitendo cha kanisa langu la Uingereza kufungisha ndoa mashoga, huku wakikataa mtu kuwa na wake wengi, eti ni dhambi.

Wanatetea ndoa za mashoga na kuziita eti ni kielelezo cha haki za binadamu.

Nikaona tusikwazane, tusikerane.
Mkuu una muabudu mzungu au Mungu?
 
Back
Top Bottom