Niliamua Kuitest Nissan Dualis barabarani

Niliamua Kuitest Nissan Dualis barabarani

Mtu kujisifu kukimbizana mabarabarani huko ni kituko hasa.
Tulioponea chupuchupu tukarudi duniani kwa kudra za Mungu tunakwambia ongeza mwendo tu.
Iko siku,
wenzio hata leo ukiuliza mke wangu nani ntamuuliza 'eti mwanjaa wewe unaitwaje vile? kama mzee Mwinyi.
 
Heshima kwenu wakuu.

Wiki iliyopita niliamua kuifanyia nissan dualis majaribio ya mbio barabarani.( nilikua natafuta ligi kwa udi na uvumba)

Nilitenga hela ya faini 150,000.00 kwa safari ya kutoka Dsm to Singida. Ilipigwa 100,000 nikabaki na 50,000.

Nilianza ligi na Vanguard, crown, subaru. Crown alikuwa ni mjeshi yeye anapita tuu

Ila hadi tunaingia morogoro crown na subaru tumeziacha nyuma sana.

Kufika Moro, vanguard na mimi na Nissan patrol (DFP)

Vanguard mziki ulimshinda akakaa nyuma nahisi aliogopa trafiki,

Nilifika Mbande ilibidi nikachungulie dereva wa Nisan Patrol ni nani, yule mzee anaendesha gari kama pikipiki anaovertake sehemu hatari balaa

Alikuwa anakimbia aseee, huyu ndio alinipa challenge kwakuwa alikuwa haniachi 500m.

Nissan Dualis ni mnyama sana, hata nikisema nipate gari, narudi kwa Dualisi tena.

Hongereni sana trafiki mnafanya kazi ipasavyo.

Upadates:

Dar es Salaam to Dodoma_( Masaa 5 net) mafuta yaliyotumika 3/4 tank
Kwani hiyo ajali ilitokea wapi???😳
 
Mtu kujisifu kukimbizana mabarabarani huko ni kituko hasa.
Tulioponea chupuchupu tukarudi duniani kwa kudra za Mungu tunakwambia ongeza mwendo tu.
Iko siku,
wenzio hata leo ukiuliza mke wangu nani ntamuuliza 'eti mwanjaa wewe unaitwaje vile? kama mzee Mwinyi.
Sie tumepita hapo Msamvu muda si mrefu tumekuta Dualis ipo mtaroni nikajua ni yeye
 
Mimi Dar ni either tarehe 20 au 21, mimi natokea kyela..mara nyingi moro napita night kimtindo...
Piga mdogomdogo tu unafika kilaini,sio mambio yasio na msingi wakati huwahi abiria.
Kyela-Dar siku 2.
Unazima Iringa siku inayofata unaamsha Dar mchana ushafika.
 
Back
Top Bottom