Nilichobaini kwa watu wa Njombe

Hongera sana kwa hio simulizi nzuri na uzoefu uliopata njombe
 
😂😂😂😂😂😂
Mgeni mgeni mgeni huyu mgeniiii
 
Nature ya mazingura huku mkuu.

Ila wafugaji wapo wa kawaida.

Parachichi huku ndio sehemu yake karibu sana.
Ahlaaaaa!😳😳😳😳
We mbena gani unajua kukuna nazi!?
We mzaramo mkuu umeenda kutalii tu huko,fanya urudi Chalinze Njombe hakuna nazi.
 
GoldDhahabu unasema kweli. Kuna jamaa alienda njombe kwa masuala ya posa . Aliporudi alituambia amekuta watu wa Njombe ni wachapa kazi sana. Wote waliokuwa nao waliishangaa kuona biashara zilianza kuchangamka tangia mapema asubuhi kinyume na mijimingi hapa cnini Tz. NJOMBE OYEE.

Sent from my SM-A045F using JamiiForums mobile app
 
kule ishu ya malisho ni ngumu mji umejaa milima kule sisi nguruwe ndio Kila kitu
 
Wakijitahidi vizuri kwenye lishe bora maumbo yao yanaweza kuwa makubwa. Wale nyama, samaki, maziwa na mayai kwa wingi sana.
 
You said it all bro!!
Karibu sana Njombe.
 
Zamani tulikuwa tunafuga ufugaji huria ila kutokana na ardhi nyingi kuwa imewekezwa kwa kilimo cha miti ya mbao na matunda ufugaji huo ukakosa maeneo ya kuchungia hivyo waliobakia wengi wanafuga ufugaji wa kisasa na nyasi za kulisha zinalimwa katika mashamba maalum. Siyo rahisi kujua kama watu wanafuga kwakua mifugo hairandirandi.
Ukitaka kujua wanafuga utaona viwanda vya maziwa maeneo kama Uwemba,Njombe mjini nk
Kuhusu mbolea mahitaji ni makubwa kuzidi wafugaji,mpaka sasa Wilaya inayofuga zaidi mkoani njombe ni Wanging'ombe ambako wanategemea zaidi kilimo cha kutumia wanyama kazi(ng'ombe)
 
Njombe kuna wabena pia.
Wabena ni watu poa sana ila wanaendekeza ulokole to the infinixy.
Wabena wastaarabu,hawana mambo mengi na akikupenda kakupenda.
wabena hao watu wa maana kabisa. nawapenda mnooo. lakini wabena kwao hasa sio Iringa?
 
Njombe Mjini Wabena,Wapangwa na Wakinga kiasi.
Wakinga wengi wapo Makete na Makambako.
Kuhusu vifo huenda ni suala la kibaolojia tu, hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa mali na vifo hilo suala halipo kabisa Njombe. Kwanza ukijulikana umefanya hivyo hawawezi kukuacha salama.
Labda sababu ya maradhi inaweza kunishawishi maana wengi wa wanaume miaka ya nyuma walikuwa wanaoa wanawake wengi inawezekana ndo chanzo cha magonjwa kusambaa kirahisi na kuwazoa.
 
Pole sana.
Huijui Njombe wewe.
Matajiri wa Njombe wanashinda na watu wengine kikawaida sana. Siyo ajabu kumkuta tajiri anakula supu mahali wanapokula vijana wanaoingiza elfu kumi kwa siku.
Hawana kujitutumua,mtu anapakia semi kadhaa za mbao anaenda Dar anauza halafu anarudi na pesa zake zote mfukoni kiunoni amefunga koti kama mshamba fulani kumbe amebeba mizigo.
Ila msiwakabe sasa[emoji23]
 
Kuna jambo umesahau kule njombe kila nyumba kuna mgonjwa wa HIV..... hiii ni moja ya changamoto ya mkoa huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…