Mimi nimeamua kufunguka hapa JF ili kuwafungua na wengine. Kuhusu viongozi wa dini, hilo pia ninalifahamu, ipo siku yao nitawapiga nyundo nzito pia.
Yapo mengi makubwa kuliko hata hilo la ndoa ☺️ tena hayo mazito yanafanywa na wachungaji, maaskofu, mapadri, masheikh, manabii, na mitume ni makubwa kuliko hilo ndoa lakini hakuna anaye wakemea hao ila ni vile tu wanajitahidi kuyaficha sana,, ni makanisa mengi sana yana behind the scenes ila waumini hawajui na mimi nayajua kwa sababu ni mdadisi sana,, hatuyasemi sababu yatazua mambo mengine mazito na kuwavunja moyo watu
Hata hizo ndoa mnazo sema wasanii wamevunja pia kuna siri ambazo sisi hatuzijui kwahiyo mnataka hadi mtu afie kwenye ndoa kisa ni msanii hatakiwi kukimbia mateso 🥺 Tisiwe wepesi wa kulaumu ila tuwe wadadisi wa mambo, tukiwa wadadisi wa mambo tutaweza kusaidia watu wengi sana ila kwa kuwalaumu watu bila kujua vyema chanzo cha tatizo tutapoteza watu wengi sana,, mtu akifanyiwa jambo baya ambalo halisemeki hadharani akifanya maamuzi hadharani anaonekana ni mkosaji ndg zangu kwa hali hii tunakosea sana
Wasanii wenu kuna mengi sana wanayapitia...
Kama mtu amekaa kwenye ndoa kwa miaka zaidi ya 15 then anakuja kuondoka hapa lazima kuwe na sababu ikiwemo kuchoka kuvumilia mateso
Kuachana kwa namna hii sababu kubwa ni kuchoshwa na jambo fulani alilovumilia kwa kipindi chote lkn hakuna hata uhafadhari na miaka inazidi kusonga kumbuka kila mtu yupo hapa duniani ili afurahie maisha sio kuteswa na mtu
Kwanini mtu ateseke kwa sababu akichukua hatua ataonekana yeye ndio mkosaji.. huu ni ukatili unaofanywa na wanajamii kushirikiana na mtesaji mwenyewe🥺 hili ndio jambo la kukemea sio kumkea mtu aliye amua kujipunguzia mateso