Nilichogundua, waimbaji wengi wa injili wa sasa hawana Yesu, ni biashara zaidi

Nilichogundua, waimbaji wengi wa injili wa sasa hawana Yesu, ni biashara zaidi

Hakika pamoja na mapungufu yao, lakini wengi wametubariki na nyimbo zao na shuhuda zipo zaidi ya maelfu kwa maelfu kuwa hawa hawa baadhi ya waimbaji injili ambao leo tunawanyooshea vidole, wakati wa majuto na kukosa tumaini nyimbo zao ziliturejeshea tabasamu na kutusogeza karibu na Muumba.

Kuna baadhi ya watu ambao walitaka hata kujidhuru na kujitoa uhai wao, lakini kupitia nyimbo za dini katika wakati mgumu wakakumbushwa kuwa yupo awezae yote na kwake hakuna kinachoshindikana basi wakaiona nuru na kupata tumaini jipya.

Hivyo waimba nyimbo za injili wot tuwaombee, tuwatie Moyo na tuwakumbushe kuwa hakuna aliye mkamilifu hata wanapokosea basi watubu na warejee katika mstari ulionyooka maana karama zao na vipaji vyao ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa ajili ya kulitangaza neno lake. Amen

Tubarikiwe sote na tuwe na jumapili njema🙏🏿
Uko sawa ila suala ni THE MOTIVE BEHIND. Nini kimewasukuma kuimba? Money or service? Na hizi nyimbo nyingi wala hazipiti kwenye vyombo vya kuhariri kuona kama zinaendana na kweli za kibiblia au Teolojia. Mtu anaandika tu wimbo in an unsupervised manner. Hii ni hatari kubwa.
 
Back
Top Bottom