Nilichojifunza kusafiria Pikipiki safari ndefu

Yap hapa mwenyewe unaona kuwa Kuna sehemu ulipita zilikuwa hazina rami....Mimi niliteleza kwenye mkeka mwanzo Hadi mwisho
 
Wengi wanaoponda usafiri wa pikipiki ni wanaume/wavulana wa dar.Wa mikoani anaanzaje kuponda huo usafiri ikiwa wa baiskeli tu ni kawaida kutumia km 80?
 
Harley sio mchezo aisee. Wale jamaa wana pikipiki haswa.
 
ACHA UONGO

Utoke Dar to Shinyanga Kwa Boxer utumie saa 12?
Mwongo mkubwa huyu... Dar - Shinyanga ni kilometa ngapi? Tena anasema kwa mwendo wa kawaida... Hizi ni stori za kijiweni za wanabodaboda,
Kuna mmoja alisema alitoka Dar - Mwanza kwa bodaboda.... ACHENI kutufanya wajinga.
Angesema alikuwa na Honda ya kuanzia cc 250 (mf. Baja) na kuendelea, labda angeeleweka
 
Unapinga nini sasa? Mimi nilitoka Mwanza To Tarime kwa Tvs 150 na spidi niliweka 80 hakuna basi ambalo lilinitangulia mbele nilipitwa na Ford 1 tu.Nilitumia masaa 4 tu kumbuka hiyo ni km 338
Na mwendo huu wa 80kph naona ni mzuri hata route ya Dar unapiga tu kama wewe ni mzoefu barabarani na unajua kuendesha pikipiki vizuri.Usipingane na mtoa mada katika hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…