Nilichojifunza kusafiria Pikipiki safari ndefu

Nilichojifunza kusafiria Pikipiki safari ndefu

Mie Juma mosi iliyopita nimetoka Dodoma saa 7 na SunLG kitako cha mbuzi hadi Kondoa 160KM kwa rami,nikatoka kondoa to Kateshi 95 KM rough road nilifika saa 7 usiku hiko Kateshi.Mafuta nilitumia 30K.

Kesho yake nikatoka Kateshi saa 4 asubuhi-Singida Mjini 90KM kwa mafuta ya 10K,nikampuzika kidogo kisha nikaanza safari ya Singida -Dodoma 240KM kwa mafuta ya 20K.

So,kwa ujumla safari nzima nilitembea 590KM kwa mafuta ya 60K,ambapo nilitumia masaa 13.

KAKA KAMA WEWE ULITOKA DAR TO SHY 990KM kwa masaa 12 hongera.
Yap hapa mwenyewe unaona kuwa Kuna sehemu ulipita zilikuwa hazina rami....Mimi niliteleza kwenye mkeka mwanzo Hadi mwisho
 
Mwaka Jana nilijaribu kwenda masafa marefu na piki piki ilikuwa BOXER 125 nilienda shinyanga nilitumia masaa zaidi ya 12 maana nilitoka dar es salaam alfajiri nikafika shinyanga jioni kwenye saa 1 hivi kasoro...! Boxer kidogo barabarani ilikuwa inayumba Nategemea kwenda Shinyanga kwa pikipiki aina ya Boxer, CC 125
View attachment 3135103
Mwaka huu hivi karibuni nikaamua kubadilisha usafiri nikatumia Tvs hizi toleo jibya wanaziita TVS HLX 5G hizi pikipiki nilikuwa sizielewi ila kwakweli mfumo wake ni mzuri japo kwa mbali ukikosea kuzipanga gia vizuri Ina mtetemo ila ni kwa mbali sana...na gia ukizipatia kuingiza inatulia inakuwa kama baiskel vile...Ina kuwa nyepesi na haiyumbi au kupepesuka barabarani.
View attachment 3135112

Angalizo ukiwa unataka kutumia usafiri wa piki piki kwa masafa marefu...​
  1. Mwaga oil​
  2. Kuwa na spana za akiba.​
  3. Mafuta hayana shida sana maana shell zipo Kila Kona. Ila ukibebab kidumu Cha mafuta walau Cha lita 5 chenye mafuta ya imagance sio mbaya.​
  4. Beba balbu ya taa ya mbele.​
  5. Usithubutu kusafiri na piki piki jioni...mwisho wa kusafiri na piki piki ni saa 12 jioni. Kigiza kikianza kuingia barabara kubwa inakuwa hatari sana...madereva wasio na akili Wana washa headlight itakavyo kufanya upoteze uelekeo.View attachment 3135121hivyo ni Bora ukathitisha safari Giza likiingia.​
  6. Vaa sulualu zaidi ya Moja barabarani Kuna bari sana. Vaa hata jinzi Tatu.​
  7. Vaa masharti ya mikono mirefu hata mawili pamoja na jaketi zito la ngozi.​
  8. Vaa viatu haswa mabuti yatakayo kufanya uibane suluali.​
  9. Badilisha oil Yako mwanzo wa safari...!​
  10. Usilazimishe ku over take mabasi​
  11. Nenda mwendo wa kawaida tu speed 80...ila kama uoni wako ni mzuri unaweza kwenda zaidi ya speed hiyo ila kwa uangalifu mkubwa.View attachment 3135133kwakweli sijutii kabisa kusafiria Pikipiki nilikuwa naogopa sana kutumia pikipiki zenye cc mdogo ila sio hatari kama Wanavyo dai...nili enjoy sana safari za pikipiki.​
Wengi wanaoponda usafiri wa pikipiki ni wanaume/wavulana wa dar.Wa mikoani anaanzaje kuponda huo usafiri ikiwa wa baiskeli tu ni kawaida kutumia km 80?
 
Nakuunga mkono, kuna watumiaji wa piki piki wako makundi matano 5.
1. Kundi la kwanza ni The Poor & the destitutes.
Hili ndilo kundi kubwa. Kufuatia hali ya umasikini, watu wengi haswa vijijini wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea ambapo hawana usafiri mwingine
Wowote tegemeo zaidi
pikipiki hawa ni wale wanao lazimika kutumia usafiri wa piki piki kama usafiri, tuu, wanatumia kusafiri mbali kwa sababu ya shida tuu, dharura na hakuna usafiri mwingine affordable.

2. The Mishe Mishe Men. Kuna watu wa mishe mishe za mambo yao fulani fulani za kukwepa mandata mabararani, hivyo hutumia piki piki kupitia njia za panya road ili wasidakwe.
3. The Hurry Men. Kuna watumiaji wa pikipiki hutumia ili kuwahi sehemu, usually maeneo ya mijini yenye foleni kila kona, usafiri wa pikipiki ndio usafiri pekee wa kuwahi.
4. The Ordinary Preference
Kuna watu usafiri wa pikipiki kwao ni preference, kuna usafiri mwingine mwingi, public transport, daladala, uba na bolt, taxi, magari, mabasi, treni na ndege lakini wanachagua kutumia usafiri wa pikipiki just for preference.
5. The Hobby Group both the rich and the ordinary.
Hili ni kundi la watumiaji wa piki piki kwa hobby, usually wanaendesha wenyewe, hawa wanatumia pikipiki as hobby, hawa wanakwenda na pikipiki popote kwasababu wanapenda and it is fun kwao. Ukifanya kitu unachokipenda na una enjoy, huchoki, na mapenzi yakizidi unakuwa blinded unacheza michezo ya hatari bila kugopo.

Kundi hili lina bike.loves wa kawaida na the rich and the famous. Hili ndilo kundi langu.

Nilikuwa namiliki piki piki 5 kwa matumizi mbalimbali.
1. Batavus ya 50 cc ya kuendea dukani hapo jirani.
2. Honda VT 250cc ya kuendea kazini daily
3. Beta 350 off road ya kuchezea michezo ya piki piki pale Kawe kila Jumapili.
4. Buel 1,200 cc for fun ride, hii ni racing bike, the only one in Tanzania by then, niliinulia US and it costed me a hell.
5. Harley Davidson 1.800 cc custom made for long safari.
Hii Harley bongo ni tuu na wazungu. Hii ndio ilinifanya vibaya na ikaripotiwa humu Pascal Mayalla apata ajali..... na nilipopona nikatoa shikrani humu Waraka wa Pascal Mayalla - Asanteni Sana!

P
Harley sio mchezo aisee. Wale jamaa wana pikipiki haswa.
 
ACHA UONGO

Utoke Dar to Shinyanga Kwa Boxer utumie saa 12?
Mwongo mkubwa huyu... Dar - Shinyanga ni kilometa ngapi? Tena anasema kwa mwendo wa kawaida... Hizi ni stori za kijiweni za wanabodaboda,
Kuna mmoja alisema alitoka Dar - Mwanza kwa bodaboda.... ACHENI kutufanya wajinga.
Angesema alikuwa na Honda ya kuanzia cc 250 (mf. Baja) na kuendelea, labda angeeleweka
 
Mwongo mkubwa huyu... Dar - Shinyanga ni kilometa ngapi? Tena anasema kwa mwendo wa kawaida... Hizi ni stori za kijiweni za wanabodaboda,
Kuna mmoja alisema alitoka Dar - Mwanza kwa bodaboda.... ACHENI kutufanya wajinga.
Angesema alikuwa na Honda ya kuanzia cc 250 (mf. Baja) na kuendelea, labda angeeleweka
Unapinga nini sasa? Mimi nilitoka Mwanza To Tarime kwa Tvs 150 na spidi niliweka 80 hakuna basi ambalo lilinitangulia mbele nilipitwa na Ford 1 tu.Nilitumia masaa 4 tu kumbuka hiyo ni km 338
Na mwendo huu wa 80kph naona ni mzuri hata route ya Dar unapiga tu kama wewe ni mzoefu barabarani na unajua kuendesha pikipiki vizuri.Usipingane na mtoa mada katika hilo.
 
Back
Top Bottom