Nilichojifunza kusafiria Pikipiki safari ndefu

Nilichojifunza kusafiria Pikipiki safari ndefu

Passo cc990 inatoboa Shinyanga na popote bila kuchemsha.

Ugomvi ni gari ya cc660, hii hata Moro hutoboi!!
Kwahiyo Suzuki Jimny ni ya kutembelea town tu?

Ila pikipiki ni CC 125 mpaka 150 ambayo mleta uzi kasafiri nayo kwanini CC 660 ziwe hazina uwezo
 
So ulitembea km zaidi ya 1000 Kwa saa 12 yaani ulikuwa unamantain speed ya 90kmh muda wote WA safari
Kuna muda nilikuwa nazidi...nilitembea Hadi 100kmh njiani nilikutana na raia nahisi walikuwa wanaenda either kuchukua MKAA au walikuwa wanarudi....wale jamaa walikuwa wanne bwana walikuwa enaendesha pikipiki...kupitia wao tukawa tuna kimbizana...hao jamaa tulikimbiza pita nikupite🤣🤣🤣 Hadi Dodoma tokea CHALINZE...

Kupitia hao jamaa safari niliiona nzuri Hadi tukawa marafiki tuliokutana barabarani...!​
 
Upo sahihi ila kwenye muda apo umetupiga mkuu...

Mimi natumia zile kubwa cc 200....Km 85 adi 90 natumia Lisaa 1 [1hr] apo speed nacheza na 80 adi 100...

Kwa boxer au tvs 150 labda masaa 20...umejitahidi sana masaa 15 dar-shy na apo ujasimama kupumzika wala kupata msosi kidogo.
-----------------

Usafiri wa pikipiki ni mzuri sanaa,hasa ukiwa unaendesha kwa mapenzi yaani unapenda kitu kipo kwenye damu,utaenjoy sana.

Pia ni usafiri wa hatari sana,hasa kama una matatizo ya kiafya (pressure,msongo wa mawazo,au uoni hafifu)....ukiwa barabarani na pikipki muda wote akili iwe active.

Napenda sana zile pkpk kubwa cc 200 na kuendelea afu nyuma ufunge mzigo wa kg 10 au 15......sipendi kubeba mtu labda iwe tu dharura.
Sijawapiga ndugu yangu...nilisimama kidogo Dodoma...Kisha nikaendelea na safari Hadi mwisho...! Ninachokumbuka Dar es salaam nilitoka alfajiri​
 
Kwanini sasa cc660 ichemshe wakati pikipiki tunazunguka nazo kutwa nzima na azichemki...hapa naizungumzia cc 125 ambayo ni ndogo sana kuliko hiyo cc660...!​

Gari yenye cc660 inakuwa na piston 3 wakati yenye 990 inakuwa na piston 4.

Piston inatoa horse power ndogo sana kumudu kuvuta mzigo wa kilo mia kadhaa umbali mrefu, nadhani pikipiki hp inayozalisha inaendana na load iliyopo!
 
Kwahiyo Suzuki Jimny ni ya kutembelea town tu?

Ila pikipiki ni CC 125 mpaka 150 ambayo mleta uzi kasafiri nayo kwanini CC 660 ziwe hazina uwezo

Load ya gari na mizigo haiendani na hp inayozalishwa na gari kumudu safari ndefu.

Cc660 ni piston tatu ujue, mbili zinashuka moja inapanda kuvuta kwa muda mrefu haiwezi
 
Mwaka Jana nilijaribu kwenda masafa marefu na piki piki ilikuwa BOXER 125 nilienda shinyanga nilitumia masaa zaidi ya 12 maana nilitoka dar es salaam alfajiri nikafika shinyanga jioni kwenye saa 1 hivi kasoro...! Boxer kidogo barabarani ilikuwa inayumba Nategemea kwenda Shinyanga kwa pikipiki aina ya Boxer, CC 125
View attachment 3135103
Mwaka huu hivi karibuni nikaamua kubadilisha usafiri nikatumia Tvs hizi toleo jibya wanaziita TVS HLX 5G hizi pikipiki nilikuwa sizielewi ila kwakweli mfumo wake ni mzuri japo kwa mbali ukikosea kuzipanga gia vizuri Ina mtetemo ila ni kwa mbali sana...na gia ukizipatia kuingiza inatulia inakuwa kama baiskel vile...Ina kuwa nyepesi na haiyumbi au kupepesuka barabarani.
View attachment 3135112

Angalizo ukiwa unataka kutumia usafiri wa piki piki kwa masafa marefu...​
  1. Mwaga oil​
  2. Kuwa na spana za akiba.​
  3. Mafuta hayana shida sana maana shell zipo Kila Kona. Ila ukibebab kidumu Cha mafuta walau Cha lita 5 chenye mafuta ya imagance sio mbaya.​
  4. Beba balbu ya taa ya mbele.​
  5. Usithubutu kusafiri na piki piki jioni...mwisho wa kusafiri na piki piki ni saa 12 jioni. Kigiza kikianza kuingia barabara kubwa inakuwa hatari sana...madereva wasio na akili Wana washa headlight itakavyo kufanya upoteze uelekeo.View attachment 3135121hivyo ni Bora ukathitisha safari Giza likiingia.​
  6. Vaa sulualu zaidi ya Moja barabarani Kuna bari sana. Vaa hata jinzi Tatu.​
  7. Vaa masharti ya mikono mirefu hata mawili pamoja na jaketi zito la ngozi.​
  8. Vaa viatu haswa mabuti yatakayo kufanya uibane suluali.​
  9. Badilisha oil Yako mwanzo wa safari...!​
  10. Usilazimishe ku over take mabasi​
  11. Nenda mwendo wa kawaida tu speed 80...ila kama uoni wako ni mzuri unaweza kwenda zaidi ya speed hiyo ila kwa uangalifu mkubwa.View attachment 3135133kwakweli sijutii kabisa kusafiria Pikipiki nilikuwa naogopa sana kutumia pikipiki zenye cc mdogo ila sio hatari kama Wanavyo dai...nili enjoy sana safari za pikipiki.​
Kuna mwaka mwana JF Pascal Mayala nae alisafiri kwa pikipiki yake ya Kisasa kutoka Dar kwenda Dodoma lakini haikufika aliishia njiani,alienda kuponea India majeraha aliyoyapata
 
Back
Top Bottom