Nilichojifunza kutoka timu za Tanzania ambazo zimefuzu group stages za CAFCC na CAFCL

Nilichojifunza kutoka timu za Tanzania ambazo zimefuzu group stages za CAFCC na CAFCL

ninosi

Senior Member
Joined
Jun 30, 2022
Posts
151
Reaction score
333
Mwaka jana vijana wangu wawili walikuwa wanafanya mitihani yao ya Taifa. Mkubwa alikuwa akifanya mitihani ya kidato cha 4 na huyu wa mwisho alikuwa akifanya mitihani ya darasa la 4.

Matokeo yao yalipotoka mwaka huu yalikuwa hivi:-
1. Huyu wa darasa la 4 alifaulu kwa kupata A zote. Nyumbani hapakukalika ilikuwa kila mgeni akija anataka kumueleza matokeo yake na sisi wazazi tulisumbuliwa sana tununue zawadi. Nilichogundua furaha yake ni kwasababu ni mara yake ya kwanza kuexperience furaha hiyo.

2. Huyu wa kidato cha 4 alifaulu kwa kupata Division 1 ya point 9. Huyu alinyong'onyea sana, na hakutaka hata zawadi. Nilimkalisha chini nilimuuliza kwanini hana furaha? Akanijibu, Baba tangu nimeanza kufanya mitihani ya Taifa sikuwahi kufaulu kwa kiwango kidogo kama hichi. Nilichogundua huyu hakuwa na furaha kwa sababu ana malengo makubwa.

NILICHOJIFUNZA:
1. Ukiona timu inashangilia na kulifanya jambo kubwa kuingia group stage za michuano midogo ya CAFCC, usiwacheke au kuwazuia kwasababu wametimiza malengo yao au ndiyo experience pekee waliyoipata ambayo kujirudia tena si leo wala kesho.

2. Ukiona timu inachukulia poa kuingia group stage za michuano mikubwa ya CAFCL, usiwashangae kwasababu wana malengo makubwa na nikawaida yao kufika stage hiyo.
 
Wew una furaha Gani nyingine ikiwa hta ligi kuu huongozi pamoja na kumzidi yanga mechi.

Rage apewe heshima alikua sahihi sana.

Kuingia group stage ya 'Michuano Mikubwa' ya CAFCL in furaha tosha.

Mkuu NBC PL ni marathoni. Sasa hata nusu ya msimu haijafika upo keleleni unashangalia, hii ni akili kweli au ndo umevimbewa mihogo ya kuchemsha?!

NB: Olo ini Olo, UTOPOLO VIMBENI.
 
Kuingia group stage ya 'Michuano Mikubwa' ya CAFCL in furaha tosha.

Mkuu NBC PL ni marathoni. Sasa hata nusu ya msimu haijafika upo keleleni unashangalia, hii ni akili kweli au ndo umevimbewa mihogo ya kuchemsha?!

NB: Olo ini Olo, UTOPOLO VIMBENI.
Kwani kuachwa Point huwa inaanzaje??..unadhania huwa inakuwa ghafla point 10?😹
 
Back
Top Bottom