Niko hapa Korogwe ambapo Kesho tutakuwa na kampeni ya mkoa kwa mgombea wa CCM ndugu Magufuli.
Wananchi wamejitokeza kwa wingi sana kumsalimia barabarani. Watu ni wengi mno. Nimeamini kuwa kiongozi anayeshughulika na matatizo ya watu, atapendwa na kuheshimiwa.
UPDATES
20/10/2020 0805
Uwanja umefurika watu na babu Seya anatumbuiza hapa.
Kuingia uwanjani ni lazima unawishwe na vitakasa mikono (sanitizer) na upimwe joto la mwili. CCM inajali na inachukua hatua zote za kiafya kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya
0830
Helikopta ya CCM inaamsha popo uwanjani hapa
0835
Humphrey Polepole anaongea
0850
Wagommbea Ubunge wanaeleza Utekelezaji wa ilani ya CCM, kumuombea kura Magufuli, wait wenyewe na madiwani wa CCM
Ukiwalinganisha wanaotaka urais, baadhi wanaopata kushabikiwa hadi unaona huruma. Hivi kweli akili ya Lissu inaweza kuongoza nchi na ukaamini nchi itaendelea! Tutajikuta kila siku rais akitunga sheria.
Anapendwa na nani?
Yaani atese wananchi kwa miaka mitano halafu wampende?
Kuna lipi jipya na lenye maana aliwaahidi kuwafanyia wakazi wa Korogwe mwaka 2015 halafu mwisho wa siku akawafanyia?
Magufuli anapendwa sana, wana Korogwe tusifanye makosa kabisa tujitokeze kwa wingi wetu tukamchague Raisi Magufuli na wabunge wa CCM Korogwe mji na Korogwe vijijini Mungu mbariki Magufuli na umpe Maisha marefu sana.
Kabisa mama D. Yani unajua sio Kama naongea ushabiki, aisee hilo nyomi sijapatapa ona. Kwa wale makamanda wa Lissu wanaweza kupiga simu waulize hali ilikuwaje. Kumbuka Leo mapokezi tuu mkutano n kesho
Kiki na maigizo ya jamaa yenu. Mungepigwaa mlivyo na kiherehere mungekaa kimya hata musiende mahakamani? Zama zenu za kiki na maigizo na propaganda kwisha habari yenuu.