Si tulishakubaliana kuwa ni ngumu kusema chochote kuhusu kupendwa Kwa JPM Kwa kuangalia namna anavyojaza nyomi mana wananchi wanamfwata Kwa mengi.Wakuu,
Niko hapa Korogwe ambapo Kesho tutakuwa na kampeni ya mkoa kwa mgombea wa CCM ndugu Magufuli.
Wananchi wamejitokeza kwa wingi sana kumsalimia barabarani. Watu ni wengi mno. Nimeamini kuwa kiongozi anayeshughulika na matatizo ya watu, atapendwa na kuheshimiwa.
UPDATES
20/10/2020 0805
Uwanja umefurika watu na babu Seya anatumbuiza hapa.
Kuingia uwanjani ni lazima unawishwe na vitakasa mikono (sanitizer) na upimwe joto la mwili. CCM inajali na inachukua hatua zote za kiafya kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya
0830
Helikopta ya CCM inaamsha popo uwanjani hapa
0835
Humphrey Polepole anaongea
0850
Wagommbea Ubunge wanaeleza Utekelezaji wa ilani ya CCM, kumuombea kura Magufuli, wait wenyewe na madiwani wa CCM
0950
Magufuli anawasili uwanjani
Hongera sana Magufuli na karibu Tanga
Amani
View attachment 1605139
Video (Dkt. Magufuli akiwa Mkata) [emoji1484]
View attachment 1605611
1) Wananchi wengi pamoja na watoto/wanafunzi wa shule za Msingi hawana uwezo wa kuingia kwenye show za wasanii wetu. Hivyo mikutano ya JPM inatoa fursa adhimu Kwa wananchi kuwaona wasanii wakubwa stejini bila kiingilio chochote.
2) Wapo ambao wanakwenda kumshangaa JPM Kwa vile ni Rais. Hawa ni wengi Sana pia na ninwa vyama vyote.
3) Wapo ambao wanaenda mikutano Kwa kuwa wamelazimishwa na viongozi wao wa chama. Hawa ni wale wenye uniform za chama, wanaoletewa kwa usafiri wa kwenda na kurudi na wanalipwa Posho ya kuhudhulia mkutano wa Kampeni.
4) Wapo ambao wametishwa na Maboss zao kuwa wasipoenda watakiona cha mtemakuni. Au Kwa Sababu za kinafki inabd waende kuwalidhisha Maboss zao.
5)Wapo wasanii wenyewe na wacheza shoo wao. Kundi hili hawapungui watu 200 kwenye kila mkutano.
6) Wapi viongozi wa chama na Serikali pamoja na walinz wake. Hawa pia ni Zaid ya 200.
Hivyo ndugu yangu ni ngumu Sana kujua kama wanaomfwata wanampenda au lah. Ili tujue wanaompenda Kwa dhati. Aache kutembea na wasanii ndio atajua Hali ipoje. Akishindwa Hilo asubiri tu Hadi tarehe 28/10/2020 atajua ukweli.