PostGE2025 Nilichokishuhudia kwenye maandamano: Serikali ya Tanzania imeshindwa vita

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Aiseee watu mna kipaji Cha kuandika.
 
Wanapropaganda za analogy wakati tupo 2025
 
Too long for nothing.

Niseme tu nimeshindwa kusoma hadithi yote baada ya kutambua kuwa mwandishi ni mtunzi (mashuhuri si mzuri) wa habari.

Nilikosoma, hadithi imepangiliwa vizuri kiuwasilishaji; lakini kimantiki inayo mashimo chungunzima.. Kwa mfano, hayo anayosema aliyashuhudia yeye mwenyewe yakitokea. Siku nzima yeye kazi aliyojipa ilikuwa ni ya kushuhudia matukio? Yeye alikuwa na kinga gani iliyozuia asidhurike?

Kwa mfano, anasema serikali hawakujipanga kukabiliana na matukio; hao KMKM waliibuka tu na kufika kwenye maeneo walikosababisha mauaji ya waTanganyika?.

Kwa mfano, serikali haikujiandaa kwa vyovyote kwa kuhakikisha kuwa hapatakuwepo na mawasiliano nchi nzima, ili mauaji yafanyike gizani?

Kuna mifano ming sana inayoweza kuonyesha kuwa mleta mada kakaa tu chini na kuanza kutunga hadithi aliyopanga yeye kwa kuunganisha kiufundi wa kimaandishi tu kuonyesha sehemu zilizoonekana kuwa na udhaifu kutoka upande wa serikali.

Kabla ya kuchoshwa kwa kusoma hadithi nzima, nilikuwa nimenuia kuichambua taarifa hiyo kipengere kwa kipengere; lakini kadri nilivyoendelea kuingia ndani zaidi, nikaamua nivute andiko chini kujuwa lina urefu kiasi gani....; hapo hapo nikachoka.
 
Akili zenu zinapokuwa fupi na kushindwa kutambua haya yote yalitokana na nini hasa, hapo ndipo kunaanza kuwepo na matatizo. Wewe unaangalia huo uharibifu tu uliotokea na waliosababisha huo uharibifu; lakini hutaki kujuwa kuwa haya yote yangeepukika kirahisi sana kama hatua zingechukuliwa mapema kabisa kwa kuwepo na maelewano ya kuwepo na uchaguzi ulio huru na haki.

Ni kitu gani hasa kilichozuia hili lisiwezekane? Hutaki kujuwa!
 
Kwanza kabisa niseme, akili fupi ni wewe uliyemsikiliza Dr Fauci, akikudanyanga na wewe kukubali kudungwa chanjo feki ya uviko, wakati wafanyakazi wa pfizer na familia zao walikuwa exempted. Now your body has turned into a spike protein factory machine. Nani mwenye akili fupi hapo?

Pili, nani alikuambia mimi naikubali hii serikali haramu? Nani alikuambia nakubali propaganda za hawa wauaji? Kila siku wanaongelea mali zilizoharibika bila hata kugusia mauaji ya watoto. Baadhi yetu, tumeshang'amua kuwa uharibifu huo umefanywa na hao hao CCM mtandao, kama smoke screen.
 
Najuwa maana yako ya kuweka hii taarifa hapa; wakati hata hujui lolote juu ya swala hilo, na ukimweleza mtu anayeweza kukufundisha kama mtoto wa darasa la kwanza katika eneo hilo.

Kwa hiyo nakufahamisha kuwa hunikogi chochote na ujinga huo.
Sasa kama hukubaliani na hizo "propaganda" kwa nini unazipa nguvu kwa maoni hayo uliyoweka hapo. Unapolaumu na kulaani uharibifu uliofanyika, halafu hata hukumbuki kilichosababisha uharibifu huo, bado unataka uonekane kuwa unayo akili iliyonyooka sawasawa?
 
Ilikuwa ni katika kuleta chachu kwenye mjadala, nilikuwa na hoji, kumfanya msomaji afikirie nini hasa kilitokea siku ile.
 
Ilikuwa ni katika kuleta chachu kwenye mjadala, nilikuwa na hoji, kumfanya msomaji afikirie nini hasa kilitokea siku ile.
Maswala mazito ya namna hii siyo ya kufanyia uchunguzi kutaka kujuwa waTanzania wanasimamia wapi.
 
Mwisho wa mashetani CCM na washirika wao machawa wao unakaribia.
Uzuri wake wote wanafahamika. Kwa hali iliyofikia atafuata mmoja mmoja nyumbani kwake kusalimiwa na wananchi. Sijui kwanini walishindwa kusoma nyakati? Mbaya zaidi mwenyekiti msaidizi alisema bila woga kuwa ccm itatawala milele hahaha
 
Andiko kuntu, andiko lenye afya na uonyaji. Hongera mkuu kwa kuliona hili mapema na wengi wameshindwa kuliweka wazi ingawa mioyoni mwao wanaliona ila wanasubork matokeo. R
Tutafika tu
 
Maswala mazito ya namna hii siyo ya kufanyia uchunguzi kutaka kujuwa waTanzania wanasimamia wapi.
Hapa tunajadiliana na kuelimishana, kila mtu anaufahamu wake wa kipekee, ukihoji unapata mawazo tofauti kwa wengine. Wapo ambao wataelezea kitu kile kile vizuri zaidi na wote kufaidika na madini yatakayo tolewa.

Mfano mzuri ni hii mada, mwanzisha mada alitoa maoni yake katika ku comment kwenye mada yake nyingine, kama wewe ulivyonihoji hapa. Niliposoma na kuona umuhimu wa comment yake, nikahoji, kwa nini asiipost kama mada inayojitegemea? Kwa werevu wake, mara moja aka copy&paste comment yake na kuifanya mada. Yeye alikuwa anachangia tuu, mimi nikaona madini, na wengine wengi wamemkubali na wameisifia sana hii mada.

Kwa hiyo boss, "hatufanyi uchunguzi", nilichokifanya ni kuleta chachu tuu ili kupata elimu (education) kutoka kwa wadau mbali mbali. BTW neno "education" ni neno lililotoholoewa kutoka neno la kilatini linaloitwa "educo", likimaanisha "to draw out" from within. Kwa maana nyingine elimu siyo vile vyeti bali ni mijadala kama hii ambapo wadau wanatoa madini kutoka kwenye fahamu zao.

Comprende!
 
Kinachoendelea kwasasa nchini Tanzania ni jambo watawala hawakuwahi litegemea kama litakuja kutokea Tanzania, na wanaliogopa mno: KUTENGENEZA MAGENGE YA WANANCHI SUGU.

Watanzania waliletengenezwa na Mzee Nyerere kuwa kama kondoo, yaani Serikali iwapige kofi halafu wanageuza shavu jingine wapigwe kofi jingine. Mtanzania anaweza kuwa amemzidi nguvu za mwilini polisi, lakini hata kama polisi atamshambulia alikuwa haweza kurudisha. Ni mara nadra mno kukuta watanzania wanagombana na mamlaka.

Tokea 2017-2025 watanzania walishuhudia wenzao wengi wakitekwa hadharani bila huruma na hawakuweza kufanya lolote lile. Bahati mbaya watawala walitegemea kwamba wakiwaua kikatili wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi mkuu basi wataweza kunyamaza. Kuna siku Raisi Samia Suluhu akajitapa kabisa kwamba "Waulize Gen-Z kama kuna mtu ana ujasiri wowote wa kufanya vurugu" akiamini kabisa kwamba amewakomesha kabisa watanzania wa bara.

Hili linafanana sana na mapinduzi ya mwaka 1905-1906 nchini Urusi ambayo hayakufanikiwa. Mfalme wa Urusi badala ya kuwasikiliza watu akawa mbabe, na baada ya watu kuogopa ndiyo wakawa majasiri zaidi na makatili. Miaka tisa baadaye yani mwaka 1917 zamu ya Mfalme wa Urusi kuuwawa ikafika. Urusi walikuwa na shirika kubwa la kijasusi (The Okhrana) ambalo lilikuwa na uwezo wa kipekee kabisa lakini lilishindwa kumlinda Mfalme Nicholas Ramanov.

The Okhrana walishawashinda kabisa wana mapinduzi wa Urusi kina Lenin. Tatizo lilianza pale ambapo Urusi ilianza kushambuliwa na maadui kutoka nje kama Ujerumani, Uturuki, Marekani na Japan. Wakati wa vita ya kwanza ya dunia, wanamapinduzi wa Urusi waliamua kuungana na maadui wa Urusi ili kuipindua serikali ya Ramanov. Jambo hili halikuwa jema lakini ukatili wa serikali ya Ramanov uliwapelekea wanamapinduzi kuungana na maadui wa taifa lao, jambo ambalo liliigawa Urusi vipande-vipande.

===============================================================================
TISS + JWTZ + CCM wasipojifunza kwa kinachoendelea, siku siyo nyingi damu itamwagika sana huku bara. Ubaya zamu hii hawataumia raia peke yao, bali na watawala pia. Vitendo vilivyotokea jana na juzi vinafikirisha mno: Mosi, Watanzania wa kawaida kuamua kufukuzia gari ili kuokoa uhai wa mtu na kufanikiwa, tena dhidi ya watu wenye silaha za moto hadi mhanga akatoroka ni jambo ambalo limejenga taswira mbaya ya uasi kwa watanzania.

Pili, kitendo cha afisa mkubwa wa serikali kuwekewa vikwazo na taifa kubwa duniani na watanzania wengi kuoneshwa kufurahishwa ni jambo la kuogopesha. Marekani anawawekea vikwazo watu wengi mno, hata maafisa wa Ujasusi wa Kagame waliwahi kushikiliwa nchini Uingereza, lakini wanyarwanda wengi walikarahishwa na hicho kitendo. Tanzania imekuwa tofauti sana, maana wengi wamefurahi, hata mimi binafsi nimefurahi sana.

===============================================================
Mnawaua watanzania, mnawatesa hadharani, huku mkiwanyanyasa na kufanya maisha yao kuzidi kuwa ya kimasikini, siku wakiamua kuusi na kuungana na maadui wa nje mtalalamika na kusema wamekosa uzalendo ??? Unaweza ukahisi hili haliwezekani, lakini mifano hai imewazunguka:

1. Musseveni aliungana na Tanzania dhidi ya serikali yake ya Uganda.
2. Kagame aliungana na Tanzania na Uganda dhidi ya serikali yake ya Rwanda.
3. Kabila aliungana na Tanzania, Uganda na Rwanda dhidi ya serikali yake ya Zaire.
4. Chiume aliungana na Tanzania dhidi ya serikali yake ya Malawi.

Wahenga husema, MUOSHA HUOSHWA. Siku siyo nyingi hawa watanganyika mnaowapuuza watafanya mambo ya hatari na ajabu halafu wote tutapoteza nchi na kushuhudia mauaji makubwa mno. Ubaya zaidi, Tanzania ikiingia kwenye machafuko makubwa ya kisiasa lazima mataifa mengi ya hapa Afrika, Ulaya, Amerika na Asia yataingia kupora mali huku yakiunga mkono pande zote.

Ninyi maafisa TISS + JWTZ mnaoua na kutesa watanzania, siku inakuja mtaamka tu na kujikuta hamna chenu, serikali imeanguka na mishahara hailipwi, mkaishia kuwa masikini kama walivyokuwa KGB na Red Army baada ya kuanguka USSR. Majumba yenu ya Mbweni, Masaki na Bunju yakawa hayana faida tena kwasababu hamna MDHAMINI.

================================================
ENIWEI, shupazeni shingo lakini siku inakuja.

Tena itakuja kama MWIVI, wakati ule hamtegemei.

Ninyi watawala wa Tanzania hamko tofauti na mataifa mengine hata kidogo.

Ni suala la muda tu, sisi tuko hapa tunakunywa KAHAWA, na panapo majaliwa tutakuja kuwakumbusha.
​
 
Alama zote ziko wazi kila kuta na lango la nchi.
Kwamba utawala uliofitinika unaanguka kwa kasi ya ajabu.

Sasa tupo kwenye 'ESCALATION TRAP'.
Watawala na vyombo vya dola wakiongeza mabavu na ukatili usemayo yatatimia, na wakilegeza demokrasia ikashamiri wataondoka madarakani haraka sana kisha watashitakiwa.
Hawajui watatokaje kwenye hii ESCALATION TRAP.
Vivyo hivyo wananchi waliochoka kukandamizwa na ubadhirifu wakirudi nyuma dola itazidi kuwanyanyasa na wakiongeza kasi kupambana nayo ndivyo ukatili unavyo ongezeka toka kwa watawala wa kimabavu.
 
Asante mkuu, sichoki kukusoma kila mara nakusearch kupata update yoyote mpya.
Mungu akulinde sana.
 
Huu ni UONGO.

Nyerere alimudu nchi kwasababu:
  • Alikuwa na akili ya kujibu hoja
  • Hakuwa na tamaa na hakuwa na cha kuficha wala kuficha watu mafisadi
  • Hakuwa mtu wa kukaza fuvu. Na nduo maana alibadilisha mengi kwa njia za mazungumzo kama, Uhuru, multiparty, Muungano, Dini, etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…