PostGE2025 Nilichokishuhudia kwenye maandamano: Serikali ya Tanzania imeshindwa vita

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mkuu umeandika vizuri. Vyombo vya ulinzi vilitumia nguvu nyingi sana kuzuia waandamanaji, vikapitiliza na kuua watu wasio na hatia majumbani kwao.

Kwenye changamoto kama hiyo inategemewa kwanza riot police watumie njia za kudhibiti maandamano kama risasi za mpira, maji ya washawasha, mabomu ya machozi. Ila wao walianza moja kwa moja kwenye risasi za moto kama vile wanapambana na magaidi. Gaddafi alianza hivihivi kwa nguvu nyingi mpaka pale waandamanaji walipoanza kujibu na ikawa hakuna anayeweza kurudi nyuma tena.

Sasa raia wana chuki nyingine ya ziada, wakati mwanzoni walikuwa na chuki na utekaji, kuminywa demokrasia na ufisadi.
 
Hili mbona ni dogo sana ndugu yangu.

Kuna silaha zimepita mpaka fulani hivi zimefika Dar Es Salaam nyingi mnoo.

Kiukweli mpaka kufika 2027 dunia nzima haitaamini kwamba hawa ni watanganyika.
​
We usinambie kwamba vijana wa Gen-Z wanaletewa silaha Kwa magendo, hii mbona harufu ya uasi au civil war. Ee Mungu tuepushe na janga hili.
 
Maandamano au uporaji?
 
Kisasi lazima kilipwe, sasa watu wanafanya marking tu kujua nani anaishi wapi, hivyo ikianza utashangaa ni surprise tu machawa wote wanakuwa homeless ndani ya siku
Kuna mambo watu wanafanya bila kufikiria

Mfano umeuwa watoto wangu, na wewe unakoishi napajua. Kwa kuwa unanizi nguvu na mamlaka nitamwachia Mungu kwa muda tu, lakini you will pay the price hata kama baada ya miaka 20 mbele.

Dhambi ya kuua usiifanya ukadhani watu watasahau, never.

Mwandishi ameeleza vizuri hiki ndio kinafanya vita Congo, Somalia, Sudani na Kwingineko isiishe. Yule uliyemuulia ndugu zake atakimbia muda ule ambao unamzidi nguvu, akipata upenyo analianzisha upya.

Tusiende mbali kwani Rwanda 1994 ilikuwaje? Ndugu zake Kagame waliuwawa miaka ya 70 na 80. Waliousika wamekuja kulipa Gharama 2000s iwe familia zao au wao wenyewe.

Mungu atuepushe na dhambi za kuua hazichagui, madhara ni kwa nchi nzima
 
Maandamano au uporaji?
Whatever you call it, but it happened in almost every part of our country. Kiburi na kubeza hakusaidii kitu, ndo maana hata Rais Kwa kuliona hilo , ameamua kuachana na machawa na kuamua kubadilisha mtazamo na Sasa anaongelea maridhiano, misamaha kujenga demokrasia. Yangekuwa hayakutokea angebaki na kauli za kubeza za akina Wasira, wenye mawazo ya kale wasijue nchi na Dunia imebadilika sana.
 
Kuna wakati kama walichanganyikiwa
 
The Tanzania we grew up in, is gone and it will never come back.
Maneno haya yamenifanya nitokwe na chozi
Pascal Mayalla pitia uzi huu naamini una chakujifunza, huwaga sisi binadamu tuna dondoka na kuinuka na kwishwa kujifunza wapi tulikosea.
 
Serikali hii ikitenda HAKI sawasawa na madai ya wananchi obviously inatoka Madarakani. Je,wapo tayari kwa hilo?
 
Ila bongo nyoso tunaishi kwa neema ya Mungu tu. Machafuko ya siku tatu tu tayari njaa mtaani imeshatamalaki, je yangeendelea wiki mbili tu vita ingeisha maana hadi makachero wangekufa njaa
Tungeenda wiki zaidi ina maana FUEL ndiyo ingeanza kupanda bei na MTEJA mkubwa angekuwa ni SERIKALI kwasababu itabidi magari yote ya jeshi vikosi vya usalama Tanzania nzima yajazwe mafuta na kuwa barabarani masaa 24. Hili lingepelekea kabisa jeshi kupewa kipaumbele hivyo magari ya raia yangebaki ndani tu.

Mara ya kwanza wangefanikiwa kwasababu ya ruzuku za hapa na pale, lakini ikiendelea itakuwa mzigo kwasababu mafuta hayo hayatumiki katika uzalishaji, na serikali itaanza kuona mzigo mzito kwasababu inatumia tu, haingizi. Kuagiza kwa waarabu haitawezekana kwa haraka maana meli za majini hutumia zaidi ya siku 10-12 ikitegemeana na spidi. Mwishowe serikali itaanza kufanya kama vita ya Kagera, manunuzi ya kukopa jambo ambalo ni hatari mno.

Huku mtaani mfumuko ambao utatokea siyo wa dunia hii. Pia kwasababu serikali imepoteza usimamazi basi kitu kiitwacho WAR-PROFITEERING/WAR PROFITEERING ambacho hakiruhusiwi kabisa wakati wa majanga ya kitaifa. Mwaka 2020 kipindi cha UVIKO-19, bei za bidhaa zilianza kufumuka na ikafika wakati watu walianza kuuza Barakoa (Masks) hadi elfu 7. Sanitizers za Detol zilifika hadi elfu 18 ndani ya usiku mmoja.

Serikali ilikuwa imedhibiti nchi basi ikafanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei wa kihuni kama huu. Mwaka huu 2025, nimeelewa na ninakiri kabisa kwamba Marehemu JPM tulimkosea mno, mimi nikiwa kinara hasahasa kwenye suala zima la UVIKO-19. Kama angeweka Lock-Down kipindi kile basi watanzania wengi mno wangepoteza maisha na uchumi wa nchi ungeporomoka ndani ya wiki tu. Lakini jambo jingine, Serikali ilikuwa haina uzoefu na CURFEWS.

Hii ndiyo CURFEW kubwa kuwahi tokea nchini Tanganyika. Hivyo vyombo vya usalama havikuwa na uzoefu wowote ule, wala miongozo ya nini kifanyike endapo jambo kama hili limetokea. Inaweza isiwe MACHAFUKO bali MAGONGJWA yakalipuka, fahamu kabisa CCM + TISS + TPDF + MINISTRY OF HEALTH + MINISTRY OF TRADE hawana uzoefu wowote ule na Watanganyika tutakufa sana.

NCHI ZA WENZETU, huwa zinaandaa miongozo ya kufuata kipindi majanga ya kitaifa (National Crisis) yametokea. Viwanda gani havitakiwi kufungwa, taasisi zipi za kifedha hazitakiwi kufungwa, masoko gani ya kifedha yanakuwa wazi, barabara zipi zinakuwa wazi na watu wanapita kukaguliwa wanapoenda kununua mahitaji pamoja na kusindikizwa na vyombo vya usalama.

Pia bidhaa gani ambazo zinapigwa marufuku kuuzwa, mfano FUEL, AMMONIUM, na COMBUSTIBLE CHEMICALS ambazo zinaweza tumika kutengeneza silaha za milipuko. Marekani walikuwa wanafanya simulations mashuleni, endapo vita vya kinyuklia vitatokea wafanyaje haraka. Hapa kwetu taasisi za kiusalama zilikuwepo tu, na kwasababu zimejikita kwenye kupambana na watanganyika hasahasa WAPINZANI, mambo nyeti kama haya hawakuwahi kuyafikiria kama yangetokea. UKWELI NI KWAMBA, tumepulizwa na upepo, uchi wetu umeonekana na dunia nzima wamefahamu kwamba kumbe Tanzania haivaaagi chupi.

NILISHUHUDIA: Bodaboda walikuwa wanalipwa Elfu 30 kwa safari ya kupeleka mahitaji kutoka MWENGE hadi MASAKI. Mkate wa Elfu 1 ukiuzwa hadi Elfu 4. Nyama robo ikifika Elfu 5 hadi 6 baadhi ya maeneo Dar Es Salaam.
=====================================================================
Watanganyika wangeendelea kukaza hata siku tano zaidi, serikali nzima ingeanguka kwasababu NJAA INGETAMALAKI na watu wangeingia mtaani kufanya vitendo ambavyo wangevijutia na wala asingekuwepo mtu wa kuwazuia. Ila kama ulivyosema TANGANYIKA huwa tunaishi kwa HURUMA ZA MUNGU TU, ila kiukweli sisi ni A POTENTIALLY FAILED STATE. Yakitokea majanga kama haya basi hakuna atakayesalimika.
​
 
Asante sana MALCOM LUMUMBA.
Waliopo kwenye nafasi za kimaamuzi kwenye hili taifa, wameshapoteana na mbaya zaidi waendelea kuchochora kusiko eleweka.
 
Shida kubwa ni ile kufata watu majumbani usiku, kupiga mageti risasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…