PostGE2025 Nilichokishuhudia kwenye maandamano: Serikali ya Tanzania imeshindwa vita

PostGE2025 Nilichokishuhudia kwenye maandamano: Serikali ya Tanzania imeshindwa vita

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kuna mambo watu wanafanya bila kufikiria

Mfano umeuwa watoto wangu, na wewe unakoishi napajua. Kwa kuwa unanizi nguvu na mamlaka nitamwachia Mungu kwa muda tu, lakini you will pay the price hata kama baada ya miaka 20 mbele.

Dhambi ya kuua usiifanya ukadhani watu watasahau, never.

Mwandishi ameeleza vizuri hiki ndio kinafanya vita Congo, Somalia, Sudani na Kwingineko isiishe. Yule uliyemuulia ndugu zake atakimbia muda ule ambao unamzidi nguvu, akipata upenyo analianzisha upya.

Tusiende mbali kwani Rwanda 1994 ilikuwaje? Ndugu zake Kagame waliuwawa miaka ya 70 na 80. Waliousika wamekuja kulipa Gharama 2000s iwe familia zao au wao wenyewe.

Mungu atuepushe na dhambi za kuua hazichagui, madhara ni kwa nchi nzima
Vyombo vya Usalama vimejiweka rehani maana makazi yao yanajulikana.
Ipo siku watafanyiwa surprise na wasijue wanatokaje maana hawatakuwa na uwezo kama wa Israel. Tanzania uzuri mshikamano upo kati ya raia vs serikali
 
Kizazi cha sasa kuanzi 95 hadi sasa ni kizazi ambacho akili zao wanazijuwa wenyewe akili zao ni version 2.1 adavanced na Tanzania wanatumia mfumo wa kizamani 1.0 local kuwaendeshea hawa vijana, mi mzazi wangu dingi nilikuwa namuogopa adi leo ni akija tu home nakuwa kama piliton ila mdogo angu wa 2006 kaja mtoa kamasi mpaka dingi anasema hawa watoto wa sasa wapo tofauti na kizazi kingine
Mkuu hii nukuu na mfano upo sahihi kabisa hiki kizaz kina DNA ya ajabu sana hakisikii wala kujari halafu sasa namna ya kudeal nao pia ni shida ukideal kama Unadeal na hawa 1980s umepotea kabisa..
 
Tungeenda wiki zaidi ina maana FUEL ndiyo ingeanza kupanda bei na MTEJA mkubwa angekuwa ni SERIKALI kwasababu itabidi magari yote ya jeshi vikosi vya usalama Tanzania nzima yajazwe mafuta na kuwa barabarani masaa 24. Hili lingepelekea kabisa jeshi kupewa kipaumbele hivyo magari ya raia yangebaki ndani tu.

Mara ya kwanza wangefanikiwa kwasababu ya ruzuku za hapa na pale, lakini ikiendelea itakuwa mzigo kwasababu mafuta hayo hayatumiki katika uzalishaji, na serikali itaanza kuona mzigo mzito kwasababu inatumia tu, haingizi. Kuagiza kwa waarabu haitawezekana kwa haraka maana meli za majini hutumia zaidi ya siku 10-12 ikitegemeana na spidi. Mwishowe serikali itaanza kufanya kama vita ya Kagera, manunuzi ya kukopa jambo ambalo ni hatari mno.

Huku mtaani mfumuko ambao utatokea siyo wa dunia hii. Pia kwasababu serikali imepoteza usimamazi basi kitu kiitwacho WAR-PROFITEERING/WAR PROFITEERING ambacho hakiruhusiwi kabisa wakati wa majanga ya kitaifa. Mwaka 2020 kipindi cha UVIKO-19, bei za bidhaa zilianza kufumuka na ikafika wakati watu walianza kuuza Barakoa (Masks) hadi elfu 7. Sanitizers za Detol zilifika hadi elfu 18 ndani ya usiku mmoja.

Serikali ilikuwa imedhibiti nchi basi ikafanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei wa kihuni kama huu. Mwaka huu 2025, nimeelewa na ninakiri kabisa kwamba Marehemu JPM tulimkosea mno, mimi nikiwa kinara hasahasa kwenye suala zima la UVIKO-19. Kama angeweka Lock-Down kipindi kile basi watanzania wengi mno wangepoteza maisha na uchumi wa nchi ungeporomoka ndani ya wiki tu. Lakini jambo jingine, Serikali ilikuwa haina uzoefu na CURFEWS.

Hii ndiyo CURFEW kubwa kuwahi tokea nchini Tanganyika. Hivyo vyombo vya usalama havikuwa na uzoefu wowote ule, wala miongozo ya nini kifanyike endapo jambo kama hili limetokea. Inaweza isiwe MACHAFUKO bali MAGONGJWA yakalipuka, fahamu kabisa CCM + TISS + TPDF + MINISTRY OF HEALTH + MINISTRY OF TRADE hawana uzoefu wowote ule na Watanganyika tutakufa sana.

NCHI ZA WENZETU, huwa zinaandaa miongozo ya kufuata kipindi majanga ya kitaifa (National Crisis) yametokea. Viwanda gani havitakiwi kufungwa, taasisi zipi za kifedha hazitakiwi kufungwa, masoko gani ya kifedha yanakuwa wazi, barabara zipi zinakuwa wazi na watu wanapita kukaguliwa wanapoenda kununua mahitaji pamoja na kusindikizwa na vyombo vya usalama.

Pia bidhaa gani ambazo zinapigwa marufuku kuuzwa, mfano FUEL, AMMONIUM, na COMBUSTIBLE CHEMICALS ambazo zinaweza tumika kutengeneza silaha za milipuko. Marekani walikuwa wanafanya simulations mashuleni, endapo vita vya kinyuklia vitatokea wafanyaje haraka. Hapa kwetu taasisi za kiusalama zilikuwepo tu, na kwasababu zimejikita kwenye kupambana na watanganyika hasahasa WAPINZANI, mambo nyeti kama haya hawakuwahi kuyafikiria kama yangetokea. UKWELI NI KWAMBA, tumepulizwa na upepo, uchi wetu umeonekana na dunia nzima wamefahamu kwamba kumbe Tanzania haivaaagi chupi.

NILISHUHUDIA: Bodaboda walikuwa wanalipwa Elfu 30 kwa safari ya kupeleka mahitaji kutoka MWENGE hadi MASAKI. Mkate wa Elfu 1 ukiuzwa hadi Elfu 4. Nyama robo ikifika Elfu 5 hadi 6 baadhi ya maeneo Dar Es Salaam.
=====================================================================
Watanganyika wangeendelea kukaza hata siku tano zaidi, serikali nzima ingeanguka kwasababu NJAA INGETAMALAKI na watu wangeingia mtaani kufanya vitendo ambavyo wangevijutia na wala asingekuwepo mtu wa kuwazuia. Ila kama ulivyosema TANGANYIKA huwa tunaishi kwa HURUMA ZA MUNGU TU, ila kiukweli sisi ni A POTENTIALLY FAILED STATE. Yakitokea majanga kama haya basi hakuna atakayesalimika.
​
Kwa akina mwita na masikio uliko taja fuel ilifika 7000 kwa kuuziana huko mitaani maana station nyingi hazikutoa huduma hiyo.
 
Uko sahihi kabisa kuhusu watoto wa kuanzia 95 kwenda mbele.

Iko hivi, kisayansi kizazi kimoja hutengenezwa kwa miaka 15 na baada ya hapo huwa kinaanza kuishi misingi ambayo kilijengewa. KGB wanasema ukitaka kuvuruga nchi basi anza na watoto mashuleni. Badilisha mitaala na mbinu za kielimu ambazo kizazi kinakua nayo.

Watanzania wengi ambao walisoma shule ya msingi kuanzia mwaka 1975 na kumaliza 2005 wanaendana sana kifikra na kimawazo. Elimu ilikuwa ni suala la kitaifa na siyo huria kama leo hii. Mitaala yetu ilikuwa imelalia kwenye elimu ya kijamaa (Marxist Leaning Education). Tunanyweshwa hadi sumu kwamba UBEPARI ni mfumo dhalimu wa kiuchumi, tunaimba nyimbo za kumsifu Nyerere na tunahudhuria Chipukizi-CCM.

Vizazi vyetu vilijengewa nidhamu ya woga, lakini tulifundishwa kufikiri kabla ya kutenda. Kizazi chetu sisi watu wana uelewa mkubwa wa siasa za nchi, dunia na historia, ila elimu yetu ilitunyima ujasiri na ililenga kutuzalisha kuwa wafanyakazi maofisini. Hata mtu akiishia darasa la saba alikuwa ana ufahamu mkubwa ya Uraia, Nidhamu, Stadi za Kazi na Maarifa ya Jamii.

Tofauti na wengi tunavyofikiri, Gen-Z siyo kizazi cha kwanza kufanya fujo hapa Tanganyika. Kizazi cha Millennials waliaozaliwa mwaka 1981 hadi 1986, kiliwahi kufanya vurugu kubwa za namna hii, utofauti ni kwamba hazikuwa vurugu za kisiasa. Kama utakumbuka kuanzia mwaka 1994 mashule ya bweni kulikuwa na vurugu sana na wanafunzi walishindikana kabisa. Tambaza, Mkwawa, Tosamaganga, Umbwe, Lyamungo, Lupata, Iyunga nk zilikuwa na watu wakorofi haswaaa.

Wanafunzi walikuwa wanachoma shule, wanaua makondakta na kufanya vurugu nyingine kama kutengeneza mabomu maabara (Hili lilitokea Tosamaganga, Ifunda na Mkwawa) na kukamatwa. Serikali ya Mkapa na vyombo vya usalama katika kuhakikisha hiki kizazi ambacho kinaanza kuonesha kuchukia CCM hasahasa kwenye uchaguzi wa 1995 kwa kuwaunga mkono NCCR-Mageuzi, walikuja na mkakati madhubuti kabisa wa kuvuruga elimu ya nchi.

Shule zikaanza kufungwa na kufutwa, ufaulu wa wanafunzi ukapungua kabisa wasomi wasiwe wengi, mitaala ikabadilishwa kwa kiwango cha ajabu na elimu huria ikapanuliwa jambo lililopelekea kuanguka kabisa kwa elimu nchini. Baada ya 2006 wakaja na utaratibu wa shule za kata ambao ulichangia wanafunzi wengi kukosa waalimu wa kutosha kufundisha baadhi ya masomo kwasababu walimu wazuri wote walienda shule binafsi ambazo vigogo ndiyo walipeleka watoto wao.

TATIZO LINAKUJA HAPA: Kizazi ambacho hujakiandaa kwa miaka 15, huwezi kukitawala kirahisi kwasababu hamuwezi kuwa nacho ukurasa mmoja kimawazo. Millenials walizimwa vizuri na kurudishwa kwenye mstari, serikali ikisaidiwa na wazazi ambao waliamini kabisa elimu ndiyo ufunguo wa maisha na CCM ndiyo chama kitakachowafikisha nchi ya ahadi.

Gen-Z ni tofauati kabisa. Mtoto anaweza akamaliza shule bila kujua kusoma na kuandika vizuri, hafahamu kabisa historia na nchi, hamjui Nyerere wala falsafa zake hivyo hawezi kuheshimu chochote kuhusu serikali au chama. Tofauti na Millennials, Gen-Z hawajanyweshwa ile sumu wa woga ambayo ilitolea kupitia elimu ya kijamaa.

Gen-Z wamezaliwa kipindi ambacho fursa ndogo-ndogo za kiuchumi zinapatikana kiurahisi hivyo na uchumi wa masoko umekomaa. Millennials tulitegemea ajira za maofisini, kwamba soma, faulu, omba kazi ufanukiwe maisha. Gen-Z bila woga hawachagui kabisa kazi. Tena ukizingatia wengi hawafaulu vizuri, basi huanza kutafuta hela pindi wamemaliza kidato cha nne. Bodaboda na Bajaji wengi ni Gen-Z. Wadada wa Soloon wengi ni Gen-Z. Mawinga wengi wa Kariakoo ni Gen-Z. Mafundi simu na Laptops wengi ni Gen-Z.

Kiufupi, Gen-Z kwa idadi yao wao ndiyo waendesha uchumi wa nchi. CCM ilivyovuruga elimu kwa maksudi ili kuendelea kuwatawala watanganyika kiurahisi imelata matokeo yasiyotabirika (The Plan Has Backfired). Kungekuwa hakuna mtandao basi mkakati wa CCM ungefanikiwa ila tatizo ni kwamba Gen-Z wengi wamelelewa na INTERNET, huku wazazi wao wengi wakiwa wametingwa na ugumu wa maisha na nyumbani hawapo.

=====================================================================
Watoto kama hawa ambao hawafikiri mara mbili ukishawakwaza haina kurudi tena. Gen-Z wengi hata wazazi tumewashindwa kabisa. Ukimkoromea anakujibu na kuvimba, hivyo tunaongea nao kwa kuwabembeleza siyo mabavu tu kila siku. Hawa watoto wako hivi siyo kwasababu kuna kitu wanacho la hasha. Gen-Z wa mataifa kama Uchina, Ujerumani na Urusi ambako elimu bado ni suala la kitaifa hawako hivi, wana uzalendo mkubwa mno wa kushangaza.

Ila sehemu ambako elimu ni huria kama Uingereza, Ufaransa, Marekani chamoto wanakipata kutoka kwa Gen-Z. Ndiyo maana mbali na udikteta wa Paul Kagame kutumia jeshi kutawala, ametumia elimu kuwazubaisha wanyarwanda wengi ambao ukiwasikiliza huwa hawaamini kuna dunia nyingine nje ya Rwanda, jambo ambalo siyo kweli.

Gen-Z wengi wana ujasiri mkubwa (Exceptionally Bold) ila They Lack Deep Thinking, Deep Analytical Skills, Common Sense na wanakitu wanasaikolojia tunakiita Diminished Danger/Diminished Responsibility ambapo ubongo unashindwa kuchakata hatari na kuona ni jambo la kawaida tu au kitu cha kawaida.

===============================================================
CCM haina PLAY-BOOK ya kupambana na Gen-Z. Kule Marekani magenge ya kizayuni kama AIPAC yamewashindwa kabisa Gen-Z hasa linapokuja suala la Palestina, mpaka sasa Marekani hafahamu afanyaje, mbali na kutumia teknolojia kuwadhibiti. Hapa Tanzania ambako vyombo vya usalama vilibweteka na kujiamini kupita kiasi, bila kufahamu kwamba mchwa washaanza kuvitafuna kwa ndani kimya-kimya, hawamaliza salama hata 2027.

Matatizo yote haya yalianza 1995 na kama watu wangekuwa makini na kuona mbali, basi Tanzania ingejiepusha na matatizo mengi sana. Lakini ndiyo hivyo washachelewa na meli imeanza kuzama, hapa kila mtu anahangaika kujilinda kivyake. Mle ndani CCM + TISS + TPDF, watageukana na kuchinjana kupita kiasi mambo yakakavyozidi kuwa mabaya kila mtu akitaka kukwepa lawama.

Zanzibari wanaweza kujitoa kwenye MUUNGANO, lakini mapema kabisa tutashuhudia ule Uzanziberi na Uzanzibara kwasababu adui yao wa kumrushia lawama Tanganyika a.k.a Machogo hawatakuwepo. Mwaka 1964, watu wa nje walihusika na mapinduzi lakini ukatili wote dhidi ya waarabu ulisaidiwa kuratibiwa na Wazanzibara. Hata mwaka 2001, watanganyika waliuwa wazanzibari kikatili, wakisaidiwa na Wanzanzibara.

Umeona Sudan ilivyo leo ? Wote ni waislamu lakini kuna Muislamu Muarabu na Muislamu Muafrika. Mwanzoni ilikuwa ni Waislamu dhidi ya Wakristo Weusi. Walipotengana tu, ikafahamika kwamba kumbe kuna utofauti pia baina ya Waislamu weusi na Waislamu Waarabu.

====================================================================
NOBODY is SAFE
​
Hii comment inafaa ikae kama uzi unaojitegemea pia.
 
Huu uzi watu wa nyumba kubwa wanapaswa kuchota maarifa mengi wakitumia weredi kidgo huenda mwendo wa 912 hautaingia.. ila wakikaza shingo kunauwezekano mkubwa 129 ikaja kugeuka kuwa 121 na utakuwa uzembe uliopitiliza..

Kumbuka kabla ya kufikia hapa watu walionya mno wakasema tuongee kama taifa ila haikuwa rahis maana mawazo yote yalikuwa 1029 sasa matokeo yake tumejikuta wahanga wakubwa kwenye nchi ambayo hatukuwahi kuwaza..
 
Kitendo tu cha wao kuzima internet na kisha kutumia silaha za moto kuwakabili waandamanaji ambao hawana silaha zozote, kimeonesha vyombo vyetu vya usalama vina watu wapumbavu mno, hawana waledi, ni wavivu wa kufikiri ndio maana waka opt njia ya shortcut iliyogharimu maelfu ya watu ambao ni nguvu kazi ya taifa na mbaya zaidi hata hawajali.

Ukiongeza na lile la kuruhusu mamluki kutoka nje waje wasaidie kutuliza ghasia ndio kabisa limeonesha hili taifa linaloongozwa na wajinga.
Kuna zee moja linaitwa Haj Omar Kheir, kutoka Zanzibar elimu yake ni darasa la saba.

Ndio shauri la Samia mambo ya Siasa..
Halina alili kabisa. Zerooooo
 
Whatever you call it, but it happened in almost every part of our country. Kiburi na kubeza hakusaidii kitu, ndo maana hata Rais Kwa kuliona hilo , ameamua kuachana na machawa na kuamua kubadilisha mtazamo na Sasa anaongelea maridhiano, misamaha kujenga demokrasia. Yangekuwa hayakutokea angebaki na kauli za kubeza za akina Wasira, wenye mawazo ya kale wasijue nchi na Dunia imebadilika sana.
Nachokiona bado serikali ipo kwenye denial kuanzia speech ya uapisho hadi hii ya bungeni.

Hawataki kwanza kutambua yale yalikuwa ni maandamano kwa sababu wakikubali inamaanisha waanzee kukubali kiini cha maandamano ambayo ni kupinga uchaguzi, katiba lakini pia uminyaji wa haki za binadamu uliokithiri. Kitu ambacho si rahisi maana kitabatilisha ile 97% na kitaweka sura mpya ya maridhiano kwamba yale yalitakiwa, inabidi yakelezwe. Kitu ambacho si rahisi

Kingine, njia zile zile zilizobatilisha uchaguzi ndio hizo hizo zinatumika kuhalalisha kilichofanyika kwenye maandamano kwa kumtanabaisha anaepingwa kama "victim". Na card ya uzenji na udini wanaitumia kwa nguvu pasipo kuangalia athari zake maana kama kuna vita iliyo karibu na Tanzania ni ya udini.

Siamini hawajui ila kuitumia hiyo card inaonekana wapo radhi chochote kitokee lakini power ilindwe. Kwa hiyo nachokiona struggle for power ni kubwa mno, mgawanyiko ni mkubwa mno kwa hiyo hapa njia rahisi rahisi haitolimaliza hili unless hawataki permanent solution ama la linatakiwaa kutokea tukio kubwa zaidi litakalowapa shock kubwa zaidi kiasi cha kuachia power. Kitu ambacho nacho si rahisi

Kiufupi nchi yetu imewekwa kwenye corner mbaya sana na nikitafakari ni nani wa kulinusuru hili. SIMUONI zaidi ya walioshikilia usukani waamue kulimaliza Or else. Meli inazama
 
Wanachojua ni mbinu za kizamani za kivita,
Wapasue tofauti kwa ngumi, wavute gari nk wakati wenzao wanatengeneza Drones huko
Kila mahala kwenye mjadala unahusiana na hali iliyopo na kilichotokea 29 October 2025 haya ndio nayoyasema

1. Ni kwamba jeshi letu na vyombo vyetu vimejiweka uchiiiii wa mnyama ikitokea hata kama imepigwa mechi ya kirafiki tu ya wiki moja na ka Rwanda tutapasuliwa mchana kweupe Vikosi vya adui vitakua vinapiga chai Dar na Dodoma sio tu kwasababu ya uchache wa silaha na na hayo ma logistics yani watakaochangia ushindi wa adui ni wabongo wenyewe watawataja walipo watataja kila kilochofichwa kwasababu ya chuki ambayo ipo

2. Tofauti na ile ya Iddi Amini ambapo Raia wali support nchi yao hii ya sasa raia wata support adui, Jw walipewa vyakula na kila kitu kutoka kwa wananchi safari hii watapokea usaliti ambao hawajawahi kukutana nao.

3. Vyombo si vinalala nakusema raia wakigeni wanaingia kuleta vurugu basi dua ziishie kwa hao hao raia pasitokee GenZ wakapokea raia na silaha wallah familia za askari na vyombo vingine na CCM watakiona cha mtema kuni.
 

Attachments

  • FB_IMG_1763282369940.jpg
    FB_IMG_1763282369940.jpg
    56.6 KB · Views: 15
Siku akitokea fara 1 akaanzisha kundi msituni..aiseeee!!!! Tanzania itawaka moto yoteee
Usiseme 'akitokea fara'!

Wasipokaa chini na kuridhiana kwa haki, yanayokwenda kutokea ni hayo.

Hakuna mjinga atakayekubali kuandamana kwa bango huku akisambaratishwa kwa risasi!

Hakuna atakayekubali tena hadaa za maridhiano kama safari hii mchakato huo utapita bila ya ufumbuzi wenye suluhisho la maana.

Tuombe sana Mwenyezi Mungu atuepushie hilo balaa lililopo mbele yetu linaloonekana dhahiri kutunyemelea.
 
Back
Top Bottom