FYATU
JF-Expert Member
- Dec 7, 2011
- 5,567
- 4,683
Kuhusu kutoshine kwa belle 9 siongelei clouds, lakini kiukweli na ukimuuliza mtu anayejua musiccc hasa producer aliyesomea mziki atakwambia kuwa belle 9 anajua sana tena sana.
ni kati ya wasanii wachache wanaoweza kuimba key za juu na ana sauti ya kipekee.
hata mimi nadiriki kusema Ben Pol na Diamond kwa belle 9 wanasubiri.
lakini kila mtu ana bahati yake si bongo tu hata mbele kuna watu wanakubarika kuwa wanajua kuimba sana lakini hawapigi mpunga sana kama wengine.
WORD....Mimi sio mtaalamu wa muziki ila ni msikilizaji mzuri na nadhani nina vigezo vyangu vya kuvutiwa na muziki. Nakubali kuwa Tanzania inao waimbaji wazuri wala sio Bell 9 peke yake.
Marehemu Marijani sio kwamba alikuwa na sauti inayomtoa nyoka pangoni, hata kwa ufahamu wangu mdogo wa utaalamu wa muziki hili nalitambua kupitia masikio yangu. lakini hata leo hii ninapokuwa popote pale nikiisikia sauti ya Marijani lazima nitulie nisikilize mpaka wimbo uishe. Na ninaamini hili halitokei kwangu pekee, tupo watanzania wengi.
US kuna kina dada kama Tchina Anold, Tisha Campbel...je umewahi kuwasikia hawa wadada wakiimba ? wasanii wengi maarufu tunaowajua duniani hapo kwao watasubiri, lakini jiulize kwa nini wameamua kubaki tu kama waigizaji ?
Mwisho wa siku kipaji na mafanikio ni idara mbili tofauti.