Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi

mwaka 2001 PGM umeishia kuwa mpishi sie PGM wa mwaka 2010 tunapeta na div two zetu haukuwa serious.
 
Usikate tamaa kama bado unaishi timiza ndoto zako, mwanamuziki AY alianza na muziki na sasa amemaliza kozi yake ya urubani soon ataanza kurusha ndge yetu.
 
Habari kiongoz,kwanza usikate tamaa hii nikwasababu ya mfumo wetu wa elimu ndo umetufikisha hapo.embu pigana pigana kwa kujichanga changa ufanye plan B.ili uelekee kwenye ndoto zako
 
Mkuu samahan mhindi ajakushika kato???!![emoji16][emoji16][emoji16]
Wakati nasoma A-level, Mkwawa High School (1999-2001) ulipita uvumi kuwa tunaosoma PGM tunaandaliwa kuwa marubani lakini leo hii ninafanya kibarua kama mpishi kwa Mhindi Masaki. Kwa mshahara wa 250,000/= kwa mwezi

Aisee elimu hii ovyo sana.
 
Umenichekesha sana Mkuu maisha ya wengi ndio yapo hivyo hata waliofanya vizuri bwana Njinjo bila kujiongeza msomi anaishia kutamani pesa za mifuko ya jamii..watu na PhD zao wananyenyekea na kutukanwa wasitumbuliwe kama hawajasoma kuna tofauti na mpishi...
 
Wakati nasoma A-level, Mkwawa High School (1999-2001) ulipita uvumi kuwa tunaosoma PGM tunaandaliwa kuwa marubani lakini leo hii ninafanya kibarua kama mpishi kwa Mhindi Masaki. Kwa mshahara wa 250,000/= kwa mwezi

Aisee elimu hii ovyo sana.
JF ina kila aina ya takataka,Mpaka wapishi wa wahindi
 
Wakati nasoma A-level, Mkwawa High School (1999-2001) ulipita uvumi kuwa tunaosoma PGM tunaandaliwa kuwa marubani lakini leo hii ninafanya kibarua kama mpishi kwa Mhindi Masaki. Kwa mshahara wa 250,000/= kwa mwezi

Aisee elimu hii ovyo sana.
Ulifaulu vizuri?
 
Angalia isije ikawa wewe ndo tatizo mkuu....mi mwenyewe nilisoma accountancy niliambiwa nitakuwa mhasibu kwenye mabenki makubwa makubwa...lakini sana nilisota kupata kazi nikaibukia kwenye biashara nyingi nyingi sana kutokea chini kabisa huku accountancy yangu ikinisaidia katika utunzaji wa fedha,leo hii naweza kusema nimepitiliza hadi kwenye huo uhasibu jinsi nilivyosimama,kiasi ambacho ningekuwa kwenye hio ajira ya uhasibu sidhani kama ningefika hii level
 
Katika elimu kuna slow learner, medium na vipanga. Kila mtu lazima ajitume ili afanikiwe. Wengi huwa tunahangaika na MATOKEO bila kuangalia CHANZO. Kufeli kupo lakini ukiangalia chanzo ni kutojituma. Kuna masomo ya kusoma ukiwa na muziki pembeni na kuna masomo yanataka kujichimbia bila kelele. Inategemea wengi tupo slow learners lakini enzi zetu ilikuwa ni kusoma usiku kucha. Nashangaa kuona sasa hata youtube zipo zinafundisha, unaweza kupata e-books hata pdfdrive.com wanatoa vitabu bure mtu unakalia kuhangaika na ati Magufuli etc. Soma uangaze mbele. Watu wanadai hakuna kazi, lakini kazi zipo ila sasa lazima uwe umetusua kweli anza na form four, six, degree ya kwanza (GPA isiwe chini ya 4) na uhakikishe angalau una Masters ndipo utafute kazi.
wewe nae majivuno yamekuzidi mno, una mtazamo wa kwamba unamzidi kila mtu humu JF. UNAKOSEA
 
Katika elimu kuna slow learner, medium na vipanga. Kila mtu lazima ajitume ili afanikiwe. Wengi huwa tunahangaika na MATOKEO bila kuangalia CHANZO. Kufeli kupo lakini ukiangalia chanzo ni kutojituma. Kuna masomo ya kusoma ukiwa na muziki pembeni na kuna masomo yanataka kujichimbia bila kelele. Inategemea wengi tupo slow learners lakini enzi zetu ilikuwa ni kusoma usiku kucha. Nashangaa kuona sasa hata youtube zipo zinafundisha, unaweza kupata e-books hata pdfdrive.com wanatoa vitabu bure mtu unakalia kuhangaika na ati Magufuli etc. Soma uangaze mbele. Watu wanadai hakuna kazi, lakini kazi zipo ila sasa lazima uwe umetusua kweli anza na form four, six, degree ya kwanza (GPA isiwe chini ya 4) na uhakikishe angalau una Masters ndipo utafute kazi.
HII ULIYOIANDIKA HAPA NI NNYA,
HAINA APPLICABILITY YOYOTE KATIKA MAISHA YA WABONGO WENGI KUFIKIA UFANISI!!!
 
Back
Top Bottom