Nilidhani ukiingia mbuga ya wanyama Unaona wanyama kirahisi kumbe napo tabu tupu

Tour guide alituingiza chaka akaenda kusimama pahala kumbe wajamaa upande wa pili kuna familia kuubwa hatukuona.Walikuja wangu wangu si kitoto.

Tembo mmoja alikuwa mkubwa sana si kawaida mrefu haswa kigari kileee
 
Wanasema ukiwa Mtz bei ni rahisi lakin hawakupi fursa ya kukuzungusha inavyotakiwa... wanakuwa wanakubagua dizaini huna hela huwez kuwasumbua kumaliza mafuta kukuzungusha... Waweke instuction hapo mtu ajue utaratibu wa kuzungushwa na gari bei gani na vitu vingine mbalimbali maana wengi tunajua kiingilio tu
 
Tour guide alituingiza chaka akaenda kusimama pahala kumbe wajamaa upande wa pili kuna familia kuubwa hatukuona.Walikuja wangu wangu si kitoto.

Tembo mmoja alikuwa mkubwa sana si kawaida mrefu haswa kigari kileee
Hah hah tembo ni wanyama wakubwa sana, sasa tembo ambao wanaaminika kuwa ni wakubwa zaidi wapo Katavi, mkuu hao tembo mmoja akisimama utadhani ni zile nyumba/kibanda cha chumba kimoja na hata Twiga wa Katavi ni wakubwa kulinganisha na vitwiga vya Serengeti/Mikumi au Ruaha. Inaaminika wanyama wakubwa kwa maumbo wapo mbuga mbili tu Katavi na pori la selous.
 
Selous sina mashaka nako mana niliishi sana miaka ya 90 huko.Ila kisa cha Tarangire kilikuwa cha kusisimua sana.
 
Selous sina mashaka nako mana niliishi sana miaka ya 90 huko.Ila kisa cha Tarangire kilikuwa cha kusisimua sana.
Halafu maporini tofauti na watu wanavyodhani ni burudani tu kuna hatari sana, ukileta masikhara unaweza kuwa kitoweo cha wanyama wakali wakati wowote, ukiwa mbugani lazima uwe mwangalifu, mimi ninachokifanya kabla sijaenda maporini kwanza ni usalama wa gari ninaloenda nalo na pia silali kwenye vihema na ikifika tu saa 12 sitoki nje ya lodge kwani wanyama huja hadi karibu kabisa na hizo lodge kwa hiyo kulala kwenye mahema kwangu ni big NO!
 
Kile eneo linasifika kwa aina ya wanayama wa aina fulani, kwahio tembelea mbuga zote ingawa chui si rahisi kuonekana hata kama wapo ni myama mwenye aibu hivyo hujificha....
 
Kuna jeraha analo mtu wa karibu sana kwa family hii ni baada ya kushutukizwa ghafla na ujio wa Simba aliyeachwa na wenzake mida ya jioni 1996 Selous huko, ule ulikuwa mtafutano si wa Dunia hii😀😀😀

Mgonjwa aliyekuwa amebebwa kupelekwa Hospitali 1995 akiwa hoi alipona baada ya wananchi kukutana uso kwa uso na Kiboko , wakamtupa mgonjwa chini wakasepa , mgonjwa akaona isiwe taabu akafungua mafuta naye mbio kali.

Porini kule hapana aisee, ulikuwa ukichelewa mida ya jioni kukutana na Mbweha au kikundi cha mbwa mwitu ujue kukimbia si kitoto.

Selous hapana kwa kweli kule...kuna visa vizuri japo vilinitia uoga sana mida mingine, nilipokuja kuhama nilishukuru sana.
 
Simba milia???[emoji13][emoji13][emoji13] Tanzania hii??
 
Pitia Kwa kampuni sahihi za kitalii,, siyo unakaa siku mbili unatarajia uone kila kitu ndugu! Unadhani hao wanyama wanakuwa wamepewa taarifa kwamba unaenda? Baadhi ya wanyama Kama chui Kwa mfano,, mnaweza kumaliza hata mwezi bila kumuona! Na siyo kwamba yupo mbali au hawapo!

Next time jipange kukaa mbugani angalau Kwa siku tano, na usitumie vikampuni uchwara eti!
 
Si wanasema kwenye mahema hawaleti soo?
 
Na kwenyewe chenga? bora kuangalia hawa wanaorushwa kwenye luninga...
 
Nenda mikumi na serengeti
 
Nenda Burigi - Chato utawaona wanyama wa aina zote!
 
Huko Ngorongoro creater wanapoishi wamasai jamii za simba wamepewa koo za kimasai
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…