Ulitumia njia gani? ukitaka kuona wanyama mbugani lazima ujipange vilivyo kwa kutoa pesa nyingi tofauti na vile tunatangaziwa kwenye vyombo vya habari, tatizo ni serikali kuwaachia watu binafsi kuongoza watalii, miaka ya nyuma watumishi wa hifadhi ndio ilikuwa kazi yao kuu sasawamebaki kufanya kazi za ulinzi wa wanyama na kuchukua tozo tu hayo mengine hayawahusu. Unapoenda hifadhini utakuta karibu hifadhi nyingi zina nyumba za kufikia wageni ambazo hutoza kati ya TZS 20,000 hadi 25,000 tatizo linakuja kupata mtu wa kukupeleka kwenda kuwaona wanyama ambao wanaweza kuonekana kwa wingi mbali na hizo nyumba za kufikia wageni, mara nyingi wanyama huwa kwa wingi mbali kama vile km 50 na kuendelea kwenye mapori kwa hiyo hapo inabidi mukodi waongoza watalii binafsi ambao wana magari yao na hutoza kati ya TZS 400,000 kwa siku ,ili kupunguza gharama inabidi muwe angalau watu 4. Kwa wale wenye pesa huenda kwenye makampuni ambayo yamejenga makambi yao ndani ya mbunga sehemu ambazo wanyama hupita na sehemu hizo ziko ndani zaidi ukiwa kwenye hizo kambi huweza kuwaona wanyama kwa karibu zaidi ukiwa kwenye kambi hizo lakini tatizo ni kuwa unapolipia malazi pekee jua mambo ya usafiri hadi huko ndani ni juu yako na hapo ndio shughuli ipo. Kwa kifupi kwenda kuona wanyama wakubwa 5 ni kazi kubwa na inahitaji mkwanja mrefu, pia kuna wakati mnaweza zurura mbugani mkaishia kuwaona tembo, nyati lakini kwa farusi rahisi sababu wanalindwa na wapo wachache sana tena wa kuwa hesabu, twiga utawaona kwa wingi lakini hawa wa jamii ya paka kama vile simba,chui hawa inakuwa ni wa kubahatisha ila msimu wa mvua nyingi ni rahisi kuwaona sehemu za miinuko kwa kuwa hawapendi kukaa majini kwa muda mrefu kwani kucha zao huoza wakikaa kwa muda mrefu kwenye maji.