Nilifadhaika sana kupata watoto wa kike tu

Nilifadhaika sana kupata watoto wa kike tu

Mkuu, me nina watoto wawili, wote wa kiume tupu.
Shemeji yako ana mimba nyingine ya miezi 8 sasa, natarajia mwezi ujao atajifungua.

Kila muda tumekuwa watu wa kuomba mungu ili tupate mtoto wa kike maana hawa wa kiume sina ham nao tena.
Why huna hamu nao tena😀!mm nawazaga tu kumsuka, then avae madini tu yaani . .yaan ntamtoboa sikio siku ya 2
 
Mkuu, me nina watoto wawili, wote wa kiume tupu.
Shemeji yako ana mimba nyingine ya miezi 8 sasa, natarajia mwezi ujao atajifungua.

Kila muda tumekuwa watu wa kuomba mungu ili tupate mtoto wa kike maana hawa wa kiume sina ham nao tena.
Kama mna kimuhemuhe na wahka kujua jinsia ya mwanenu ajaye mbona ultra sound itawasaidia kujua mapema tu

Nendeni hospitali, nadhani gharama za kipimo haifiki elfu 20
 
Ndo ukweli huo chief.. ondoa tu hiyo mindset.. mtoto ni mtoto mkuu..
mimi mambo ya kukaa bila amani siyataki, mtoto wakike kuna umri tu akiufikisha ni balaa mzazi unakua huna amani tena mana watoto wenyewe siku hzi wanakua mapema unakuta mtoto mwili unatamanisha lkn yeye bado ana akili za kitoto so hawezi kujilinda na vishawishi hlf kibaya zaid wanapitia vishawishi vingi mno ,yani unakuta akienda dukani anatongozwa, shuleni anatongozwa, kwenye daladala anatongozwa, kwenye mafunzo ya dini anatongozwa,nyumbani anatongozwa,mtaani tu utakuta kuna njemba kama 6 hivi zinamfukuzia yeye hapo bado kwenye safar zake nyengine n.k sasa yeye hana akili ya kujilinda na vishawish vyote hivy lazma tu atanasa kwa wahuni so inakubidi wewe mzazi umsaidie lakin kwa bahati mbaya huwezi kuilinda bahari, mana unaweza ukawa unamfundisha mtoto wako vizur tu kila muda unakaa naye unampa risala ili aweze kuyaepuka majaribu lkn bahati mbaya hawa viumbe hata sijui kwanini wakikutana na wakulungwa huko njiani wakapigishwa sound basi hapo yale maneno yote ya mzazi wanasahau na kuyakubali anayombiwa na jamaa hlf sometimes unaweza kukuta unamhudumikia mwanao vizur tu hlf anaend kuliwa na muhuni hana mbele wala nyuma shabaash..., mkuu nayaongea haya kwa experience ya kutosha pia na mengine nisiyoyataka ni kma haya [emoji116][emoji116]
 
Mungu alinipa mtoto wa 1&2 wote wa kike. Nili adopt mtoto naye ni wa kike.

Marafiki na majirani walinipa pole kwa kuwa na familia yenye watoto wa kike tu. Nilikataa kuziitikia pole hizo na kuwaambia yote ni mipango ya Mungu.

Niliamua kuwapenda na kuwafundisha upendo. Nashukuru Mungu ameamua kuwa upande wangu.

Wamekuwa sehemu ya furaha kwangu kila napokutana nao nyuso zao zinapendeza kwa furaha.

Napenda watoto wa kiume, lakini sijutii kutokuwa nao kwa sasa.

Hongera kwa kuwa Mungu amekupa ulichotaka kwa muda mrefu.
 
Mtoto ni mtoto tyuuh. Nwei hongera kwa kupata mtoto wa jinsia uliyoitaka.
 
Obama anawakike tu, Bill Clinton anawakike tu. Waafrica na wahindi ndo tumebaki kuamini Watoto wakiume Ni asset.

Dunia ya saiv kwanza ukizaa wa kiume inabidi umuombee Sana. Hata James delicious Baba yake alikuwa proud alipozaliwa akasema amezaa kidume.
Nilijua tyuuh hoja ya hivi lazimaa iwepo. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mola ana maajabu yake sana,anakujaalia watoto wa kike kisha anakupa na mapenzi ya dhati kwao.

Huwa tunasema hivi unaweza kuchukia jambo kumbe lina kheri na wewe na unaweza kupenda jambo likawa na shari na wewe.

Watoto wakike ukijaaliwa ni neema kubwa sana,hasa ukiwalea katika malezi ya dini.

Nina mengi sana ya kusema juu ya fadhila/ubora wa kuruzukiwa watoto wa kike.

Nakomea hapa.
 
Back
Top Bottom