kyagata
JF-Expert Member
- Oct 18, 2016
- 10,406
- 19,892
Ndugu zangu hamjambo?
Jamani nina mpenzi tumedumu muda sana tu na tumepitia vipindi tofauti yani ups and down.
Kuna kipindi tulikosana na mimi nikajitahidi kumuelewesha lakini akawa hataki hata kunisikia ila nikamchunguza nikagundua pia hana mtu.
Sasa nikaamua kuwashirikisha ndugu zake ili watuweke sawa lakini mwenzangu akawa kakasirika zaidi eti kwanini ndugu zake nimewaambia.
Mimi nimekua nikimjibu tu ni mapenzi yako kwako na siko tayari kukupoteza, ndugu zake wametusuhulisha lakini mwenzangu kila tukipishana kauli basi anaanza kunikumbushia kuhusu hiyo ishu ya kuwaambia ndugu zake anaenda mbali mpaka anasema mimi nimejipeleka kwao. Nashindwa kumuelewa ana tatizo gani kwani ndugu wakijua kuwa tunadate ni kosa kubwa la hadi mtu kuliweka moyoni.
Naomba mawazo yenu nifanyeje na huyu mtu jamani sababu imekua too much.