Nilifanya maombi maalum mara kadhaa, mtumishi hadi kuja kwangu, sadaka za kujimaliza ila bado nateseka mnyororo huu, eeh Mungu nifanye nini sasa?

Nilifanya maombi maalum mara kadhaa, mtumishi hadi kuja kwangu, sadaka za kujimaliza ila bado nateseka mnyororo huu, eeh Mungu nifanye nini sasa?

Tusali kwa Nafsi Zetu, Na Pia Tuweke Tumaini kwa Mungu, kweli Duniani Kuna Matatizo lakini kwa Sasa Hivi watu matatizo yako, ndo Mtaji, wanakugeuza Sehemu ya Kupatia Fedha.
Sari omba Mungu Binafsi Maana Mungu asikusikie wewe asikie tu maombi ya Muchungaji inamaana yeye ndo mwema sana kuliko wengine, Yeye Mchungaji ni Mwanadamu kama Mimi cha umuhimu ni Kumtumainia Mungu Pekee.
 
Mathayo 6; 26
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

Ila hao ndege wanaozungumziw wakiamka asubuhi chakwanza ni kwenda kwenye mti kuimba na kumwabudu mungu kisha wanazungukia majalala yao.

Subiri utumishi na maombi ya baba paroko anayetaka sadaka zako afungue online tv ale kwa viewers
 
ukitaka kujua shida inayokusibu nenda kwa muonaji (siyo mganga). Kama unaamini upande wa nuru, sikiliza au tafuta kitabu cha Mwl. Mwaksege au Pastor Sunbella Kyando masomo yake juu ya ndoto yapo YouTube. Kumbuka hawatafsiri ndoto bali wanakuelekeza namna ya kutafsiri ndoto.
Hao wote ni matapeli na wasaka fedha tu,bora waganga wa kienyeji kuliko hao matapeli,
Hao mbwa washampiga sana pesa aunt yangu
 
Siku nyingine uache upuuzi wa kutoa hizo sadaka kwa wahuni. Fanya kazi kwa juhudi na maarifa huku ukimwomba Mungu kivyako. Jifanyie tathmini na uweke malengo. Kuna matatizo ya kuisha ndani ya mwaka au miaka. Ukijiambia ukweli utafanikiwa. Ukiendelea kuwategemea hao matapeli wanaotumia biblia utapigika zaidi.
 
ukitaka kujua shida inayokusibu nenda kwa muonaji (siyo mganga). Kama unaamini upande wa nuru, sikiliza au tafuta kitabu cha Mwl. Mwaksege au Pastor Sunbella Kyando masomo yake juu ya ndoto yapo YouTube. Kumbuka hawatafsiri ndoto bali wanakuelekeza namna ya kutafsiri ndoto.
Wote hao ni matapeli.
 
Mkuu Pole sana kwa matatizo yanayokupata...

Uwezo ulionao ndio unasababisha hasira kwa asiyetaka kuona ukiudhihirisha uwezo wako na pengine yeye ndio anautumia kwa sasa.

Kuota uko shuleni inategemea ni level gani ya shule kwa sababu si kila kuota uko shuleni ni ishara mbaya, ila kwa kesi yako itoshe kusema tafsiri ya ndoto yako ni kuwa adui anakurudisha nyuma kiuchawi.

Matatizo ya namna hii ni muhimu kutafuta vitu kama chumvi ukavitumia kujisafisha hukubukiendelea na maombi.
 
Ahssante mkuu

Nimetumia chumvi
Full moon

Nimeaomba
Nakuombea

Mganga ndio bado tu?

Yani hata nashindwa kuelewa mkuu
 
Natafuta masters ya psychology. Nikiipata nakua nimequalify kutoa ushauri 100%
 
Kuota unarudi shule sio kurogwa! Manake ni kukwama! Kwa mfano mimi nilikuaga naota niko shule nafanya mtihani jibu nalijua ila mpaka karatasi zinakusanywa najikuta sijaandika chochote - nikaja kujichunguza nikagundua kwenye maisha yangu nina maswali mengi ya utatuzi wa maisha nakosa majibu na pengine jibu ninalo ila silioni au nalionea uzito /sijiamini!
Jichunguze sio kila jambo linaanza na maombi! Maarifa umepewa kwa ajili hio ufikirie ili hata utakapoomba ujue unaomba nini!

- pia kwenye maisha kuna kupanda na kushuka ndo mana wanasema Mshukuru Mungu kwa kila jambo! Kila jambo ndo hilo sasa unadhani wale wanaoumwa mahospitali sio watu? Ama yule mama aliefiwa na binti zake wawili kariakoo anajiskiaje? Magumu yapo na kukata tamaa kupo na maumivu yapo huo ndo ubinadamu kwenye maisha kuna majira kama iwavyo asubuhi mchana na jioni.
Mvua na jua nk
Kikubwa tulia kama mtu mzima chekecha akili kubali kuwa umeanguka! Hata katika maombi yako Muombe Mungu usikose ridhiki yako ya kila siku na umshukuru yeye anajua anakupitisha kipindi gani na lini atakuweka sawa kila unachoona kinatokea Mungu karuhusu! Na iko siku atakiachilia!
Shukuru hata una hao watoto wakula mawe kuna watu hawana hata hao watoto na mawe wanakula mwanzo mwisho
 
Back
Top Bottom