Nilifuma SMS za mapenzi kwenye simu ya mke siku yetu ya ndoa, bado nikamuoa lakini sasa nahisi kuchanganyikiwa sielewi nifanyeje?

Kwema Wadau?

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu,Nilikutana na Ex wangu ambaye aliniacha way back akaolewa but hakudumu ndoani alikaa 5 months only then after sometime akaolewa tena lakini hakudumu pia.Sababu ya ndoa zote kutodumu ilikuwa kutopata Mimba kiasi kwamba akasema hawezi kuolewa tena hadi abebe mimba,ajifungue ndio ataolewa.

Nilikutana nae Last Year kwenye mwezi wa Saba na tukarudisha mawasiliano na akaibuka Maghetoni nakumbuka ilikuwa tarehe 30/07/2023 akastay home kwangu kama three days akaondoka then after 2 days akarudi tena ikawa ndo kamchezo yaani anakuja week anaondoka then anarudi mwisho tukaanza kuishi pamoja.

Mwezi wa 9 hivi akanambia hajaona siku zake anahisi ana Mimba maana alivyokuja First Time alikuwa kwenye siku za hatari lakini hawezi kushangilia maana alishakutana na hizo mbanga mara nyingi lakini mwisho wa siku bila bila so tuvute subira hadi kitumbo kitoke ndo tukapime tuthibitishe kitu ambacho baadae tulikifanya na ikaonekana kweli mjamzito na kwa uwezo wake MUNGU akajifungua tarehe 19/04/2024.

She was so Happy kufanikiwa kupata mtoto na tukakubaliana tufanye kuhalalisha tu kwa ndoa simple tu maana yeye alishaolewa mara 2 so hataki tena mbwembwe.Kwahiyo Ijumaa ya tarehe 10/5/2024 tulifunga ndoa.Lakini kabla ya kufunga ndoa hiyo,asubuhi ya siku hiyo ya harusi/Ndoa nilichukua simu yake nitumie kumpigia mshenga wangu ili kupanga ratiba vizuri ya shughuli ndo nilipokutana na jambo ambalo limefanya niombe USHAURI HUU....

Nilikuta SMS anachati na jamaa anaomba Hela ya Matumizi akimwambia jamaa kuwa mtoto hana Pampers na pia Kodi yake alipopanga Imeisha.Tena anamuita mume wake kabisa "TUNAOWAAMINI NDO WANAOTUUMIZA" Kiukweli niliumia sana maana hata nilipomuuliza alianza kwa kukana kuwa hizo SMS za zamani lakini nilipombana zaidi akakiri kwamba jamaa ni Ex wake na alikuwa anamdanganya tu na wala jamaa hakutuma hela na pia wameishablokiana.Kiufupi ndoa tumefunga Fresh lakini mie sina IMANI wala AMANI kabisa yaani nawaza mengi hadi nahisi kuchanganyikiwa so guys please naomba ushauri wenu.....

WENU KATIKA
 
Endelea tu na maisha bro !
Bora ya wewe umeona, sisi wengine hatuoni yanayoendelea ila tunajipa moyo ingawa nyuma ya pazia kuna mengi mno.
Hata kama usingeona siku ya harusi ipo siku ungeona na pengine ingekuwa mbaya zaidi kuliko siku hio.

Vinginevyo wewe ni mwanaume wa shoka, uanaume haupimwi kwa maumbile kana ndevu sauti nzito nk bali uwezo wa kubeba swala nzito huku ukiendelea na mambo mengine bila wengine kuhisi au kujua, ni wachache mno wa aina yako, hata wazee wetu walikuwa wanafuka 100% lakini walikaza na kuhitimisha kitanda hakizai haramu.

Ila ijuikane mwanamke ni mtu mwenye tamaa ya asili hivyo kama unajihusisha na mwanamke juwa namna ya kukabilia na aina hio ya udhaifu wake.
Mchango wangu ni kupeleka tangazo lako la msiba radio one
 
Mwanamke siku zote ndiye mwenye power ya kusema baba wa mtoto ni nani.

Siku hizi wengine wana kadi 2 hadi tatu za clinic zenye baba tofauti lengo likiwa ni kujipatia fedha za kujikimu.

Kutokana na aliyopatia, jaribu kumsikiliza vizuri na kwa utulivu ili ujue uhalisia alitaka kufanya nini.

Hata kama ulikuwa hujamfuma na hizo sms, bado ukweli unabaki kwamba mwanamke ndiye anayejua baba halisi ni nani.

Siku zote mwanaume ni mlezi kwa hali yeyote ile.

Usikatishwe tamaa na watoto wa 2000 humu.

Msikilize vizuri ukimwelewa baki naye ila usipomwelewa achana naye!
Acha ujinga,kama Mwanamke ana power DNA zilivumbuliwa za nini?
Kama mwanamke amelala na wanaume 2 kwenye siku zake za hatari atajuaje mimba ni ya A na sio B.
 
Red flag ilikuwa kukamata sms ulivyomuuliza akakana, Mimi habari ingeishia hapo kwenye kukana sms, hakuna mtu mjinga duniani, once mtu akikuconfront kwa kitu fulani jua kabisa kuna kitu anajua....

Binafsi nisingemuelewa labda serikali ingeingilia kati.

I can't go along with liers, hivi mnawezaje kuishi na watu waongo?

Haya ngoja waje wailaumu ndoa wakati ndoa ilikuwa imekaa zake pembeni imetulia.
 
Mwanamke siku zote ndiye mwenye power ya kusema baba wa mtoto ni nani.

Siku hizi wengine wana kadi 2 hadi tatu za clinic zenye baba tofauti lengo likiwa ni kujipatia fedha za kujikimu.

Kutokana na aliyopatia, jaribu kumsikiliza vizuri na kwa utulivu ili ujue uhalisia alitaka kufanya nini.

Hata kama ulikuwa hujamfuma na hizo sms, bado ukweli unabaki kwamba mwanamke ndiye anayejua baba halisi ni nani.

Siku zote mwanaume ni mlezi kwa hali yeyote ile.

Usikatishwe tamaa na watoto wa 2000 humu.

Msikilize vizuri ukimwelewa baki naye ila usipomwelewa achana naye!
nimekuelewa kaka
 
Kwema Wadau?

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu,Nilikutana na Ex wangu ambaye aliniacha way back akaolewa but hakudumu ndoani alikaa 5 months only then after sometime akaolewa tena lakini hakudumu pia.Sababu ya ndoa zote kutodumu ilikuwa kutopata Mimba kiasi kwamba akasema hawezi kuolewa tena hadi abebe mimba,ajifungue ndio ataolewa.

Nilikutana nae Last Year kwenye mwezi wa Saba na tukarudisha mawasiliano na akaibuka Maghetoni nakumbuka ilikuwa tarehe 30/07/2023 akastay home kwangu kama three days akaondoka then after 2 days akarudi tena ikawa ndo kamchezo yaani anakuja week anaondoka then anarudi mwisho tukaanza kuishi pamoja.

Mwezi wa 9 hivi akanambia hajaona siku zake anahisi ana Mimba maana alivyokuja First Time alikuwa kwenye siku za hatari lakini hawezi kushangilia maana alishakutana na hizo mbanga mara nyingi lakini mwisho wa siku bila bila so tuvute subira hadi kitumbo kitoke ndo tukapime tuthibitishe kitu ambacho baadae tulikifanya na ikaonekana kweli mjamzito na kwa uwezo wake MUNGU akajifungua tarehe 19/04/2024.

She was so Happy kufanikiwa kupata mtoto na tukakubaliana tufanye kuhalalisha tu kwa ndoa simple tu maana yeye alishaolewa mara 2 so hataki tena mbwembwe.Kwahiyo Ijumaa ya tarehe 10/5/2024 tulifunga ndoa.Lakini kabla ya kufunga ndoa hiyo,asubuhi ya siku hiyo ya harusi/Ndoa nilichukua simu yake nitumie kumpigia mshenga wangu ili kupanga ratiba vizuri ya shughuli ndo nilipokutana na jambo ambalo limefanya niombe USHAURI HUU....

Nilikuta SMS anachati na jamaa anaomba Hela ya Matumizi akimwambia jamaa kuwa mtoto hana Pampers na pia Kodi yake alipopanga Imeisha.Tena anamuita mume wake kabisa "TUNAOWAAMINI NDO WANAOTUUMIZA" Kiukweli niliumia sana maana hata nilipomuuliza alianza kwa kukana kuwa hizo SMS za zamani lakini nilipombana zaidi akakiri kwamba jamaa ni Ex wake na alikuwa anamdanganya tu na wala jamaa hakutuma hela na pia wameishablokiana.Kiufupi ndoa tumefunga Fresh lakini mie sina IMANI wala AMANI kabisa yaani nawaza mengi hadi nahisi kuchanganyikiwa so guys please naomba ushauri wenu.....

WENU KATIKA MTIHANI MZITO
Mtu aliolewa twice huko aliko akaachika na wewe ukamuamini kirahisi? Man jitafakari kwanza. Umeoa a walking red flag
 
Back
Top Bottom