Kwema Wadau?
Naombeni ushauri wenu ndugu zangu,Nilikutana na Ex wangu ambaye aliniacha way back akaolewa but hakudumu ndoani alikaa 5 months only then after sometime akaolewa tena lakini hakudumu pia.Sababu ya ndoa zote kutodumu ilikuwa kutopata Mimba kiasi kwamba akasema hawezi kuolewa tena hadi abebe mimba,ajifungue ndio ataolewa.
Nilikutana nae Last Year kwenye mwezi wa Saba na tukarudisha mawasiliano na akaibuka Maghetoni nakumbuka ilikuwa tarehe 30/07/2023 akastay home kwangu kama three days akaondoka then after 2 days akarudi tena ikawa ndo kamchezo yaani anakuja week anaondoka then anarudi mwisho tukaanza kuishi pamoja.
Mwezi wa 9 hivi akanambia hajaona siku zake anahisi ana Mimba maana alivyokuja First Time alikuwa kwenye siku za hatari lakini hawezi kushangilia maana alishakutana na hizo mbanga mara nyingi lakini mwisho wa siku bila bila so tuvute subira hadi kitumbo kitoke ndo tukapime tuthibitishe kitu ambacho baadae tulikifanya na ikaonekana kweli mjamzito na kwa uwezo wake MUNGU akajifungua tarehe 19/04/2024.
She was so Happy kufanikiwa kupata mtoto na tukakubaliana tufanye kuhalalisha tu kwa ndoa simple tu maana yeye alishaolewa mara 2 so hataki tena mbwembwe.Kwahiyo Ijumaa ya tarehe 10/5/2024 tulifunga ndoa.Lakini kabla ya kufunga ndoa hiyo,asubuhi ya siku hiyo ya harusi/Ndoa nilichukua simu yake nitumie kumpigia mshenga wangu ili kupanga ratiba vizuri ya shughuli ndo nilipokutana na jambo ambalo limefanya niombe USHAURI HUU....
Nilikuta SMS anachati na jamaa anaomba Hela ya Matumizi akimwambia jamaa kuwa mtoto hana Pampers na pia Kodi yake alipopanga Imeisha.Tena anamuita mume wake kabisa "TUNAOWAAMINI NDO WANAOTUUMIZA" Kiukweli niliumia sana maana hata nilipomuuliza alianza kwa kukana kuwa hizo SMS za zamani lakini nilipombana zaidi akakiri kwamba jamaa ni Ex wake na alikuwa anamdanganya tu na wala jamaa hakutuma hela na pia wameishablokiana.Kiufupi ndoa tumefunga Fresh lakini mie sina IMANI wala AMANI kabisa yaani nawaza mengi hadi nahisi kuchanganyikiwa so guys please naomba ushauri wenu.....
WENU KATIKA MTIHANI MZITO
Eti wenu katika mtihani mzito,
Kwanza nikupe pole saana kaka, ila binafsi nakuomba uchukulie kawaida saana.
Binafsi Huwa nasema binadamu ni kiumbe Cha ajabu saana achana na huyo aliyefanya hayo ni mwanamke ila kiujumla binadam ni kiumbe Cha ajabu kabisa.
Unajua kwann nakuambia hivi, yaan namaanisha akili yake haina formula na uncontrolled ya sio kama mnyama kwamba unaweza ukamfuga na kumtreat unavotaka wewe na asibadilike.
Binadam hubadilika mda wwt ule na yanaweza kuwa ni mabadiliko ya ajabu Sanaa kuwahi kutokea.
Baada ya hapo nije kwenye kesi Yako, kiongozi angalia kama moyo unakuambia kuwa huyo mtoto ni wako, naomba hayo mengine achana nayo Anza naye upya.
Ila kama moyo unakupa mashaka juu ya mtoto tafuta njia ya kujiridhisha ili uwe na amani moyoni.
Mimi binafsi kaka naweza kukaa hata mwaka sijashika simu ya mke wangu maana sitaki shida.
Siku nikija kugundua Hilo hata tu kwa sms nikawa na uhakika kuwa wameshafanya, huo ndo utakuwa mwisho na mpk wangu baina yangu nayeye