Nilifuma SMS za mapenzi kwenye simu ya mke siku yetu ya ndoa, bado nikamuoa lakini sasa nahisi kuchanganyikiwa sielewi nifanyeje?

Nilifuma SMS za mapenzi kwenye simu ya mke siku yetu ya ndoa, bado nikamuoa lakini sasa nahisi kuchanganyikiwa sielewi nifanyeje?

Huna akili. Ni mpumbavu. Na unastahili kila linalokupata. Ulishindwaje ku call it off? Ulitaka kufurahisha watu. Pita hivi.
 
Huna akili. Ni mpumbavu. Na unastahili kila linalokupata. Ulishindwaje ku call it off? Ulitaka kufurahisha watu. Pita hivi.
 
Kwema Wadau?

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu,Nilikutana na Ex wangu ambaye aliniacha way back akaolewa but hakudumu ndoani alikaa 5 months only then after sometime akaolewa tena lakini hakudumu pia.Sababu ya ndoa zote kutodumu ilikuwa kutopata Mimba kiasi kwamba akasema hawezi kuolewa tena hadi abebe mimba,ajifungue ndio ataolewa.

Nilikutana nae Last Year kwenye mwezi wa Saba na tukarudisha mawasiliano na akaibuka Maghetoni nakumbuka ilikuwa tarehe 30/07/2023 akastay home kwangu kama three days akaondoka then after 2 days akarudi tena ikawa ndo kamchezo yaani anakuja week anaondoka then anarudi mwisho tukaanza kuishi pamoja.

Mwezi wa 9 hivi akanambia hajaona siku zake anahisi ana Mimba maana alivyokuja First Time alikuwa kwenye siku za hatari lakini hawezi kushangilia maana alishakutana na hizo mbanga mara nyingi lakini mwisho wa siku bila bila so tuvute subira hadi kitumbo kitoke ndo tukapime tuthibitishe kitu ambacho baadae tulikifanya na ikaonekana kweli mjamzito na kwa uwezo wake MUNGU akajifungua tarehe 19/04/2024.

She was so Happy kufanikiwa kupata mtoto na tukakubaliana tufanye kuhalalisha tu kwa ndoa simple tu maana yeye alishaolewa mara 2 so hataki tena mbwembwe.Kwahiyo Ijumaa ya tarehe 10/5/2024 tulifunga ndoa.Lakini kabla ya kufunga ndoa hiyo,asubuhi ya siku hiyo ya harusi/Ndoa nilichukua simu yake nitumie kumpigia mshenga wangu ili kupanga ratiba vizuri ya shughuli ndo nilipokutana na jambo ambalo limefanya niombe USHAURI HUU....

Nilikuta SMS anachati na jamaa anaomba Hela ya Matumizi akimwambia jamaa kuwa mtoto hana Pampers na pia Kodi yake alipopanga Imeisha.Tena anamuita mume wake kabisa "TUNAOWAAMINI NDO WANAOTUUMIZA" Kiukweli niliumia sana maana hata nilipomuuliza alianza kwa kukana kuwa hizo SMS za zamani lakini nilipombana zaidi akakiri kwamba jamaa ni Ex wake na alikuwa anamdanganya tu na wala jamaa hakutuma hela na pia wameishablokiana.Kiufupi ndoa tumefunga Fresh lakini mie sina IMANI wala AMANI kabisa yaani nawaza mengi hadi nahisi kuchanganyikiwa so guys please naomba ushauri wenu.....

WENU KATIKA MTIHANI MZITO


Mambo 2:

1. Acha huyo Mbwa.
2. DNA.

Ila huwa hamsikii....

Unatuabisha kuja kuuliza ushauri, mimi hata ndo isingefungwa.
 
Tulishawakataza kuwaonea huruma wanawake narudia tena “ mwanamke sio mtu wa kumwonea huruma” ye alikuwa hapati mtoto kwani ni tatizo laoko wewe ? Si la kwakwe yeye ? Umemwonea huruma umentia mimba amezaa ila ye hakupend wewe anampenda jamaake alichokifanya yeye ni kukuonea huruma ukamwoa na hiyo ni sababu umeweza kumjaza mimba mapenz ya kuoneana huruma ni mabaya sana hilo zigo libebe kama lilivyo umewaolea wahuni, mtoto kashapata ila bado hajampata anae mpenda ndio anamtafuta na nakuhakikishia anaempenda sio wewe mkuu, kuna jamaa mwingine atakuwa anamshindilia misumari ya moto na mapenz yatakuwa moto. When are you guys gonna learn to mind your own business ?
 
Ushauri mwingi umetolewa, wengine wakidhihaki ila isikukatishe tamaa kulisema jambo ni moja ya kutua mzigo ambao ungekutesa moyoni.

Hapo mwenye maamuzi makubwa ni wewe mwenyewe, lakini kwa upande wangu niombe mwache mtoto akue angalau miaka 2 then mwambie mkapime DNA ili kama akikataa basi achana nae mazima ila kwa sasa jifanye mjinga kwake mlee mtoto ili asiathirike na ugomvi wenu.
kwa hiyo avumilie kulea mtoto wa mwanaume mwingine.? hapo jambo la muhimu ajiridhishe kwanza kama mtoto ni wake ndo anaweza kuamua kuvumilia
 
Nilishindwa kuahirisha alinililia sana nisimdhalilishe mbele ya familia na ndugu zake
Kila siku tunapigiana kelele humu kwamba usimuoe mwanamke kwa sababu ya huruma eti atadhalilika hiyo itaku-cost lakini wewe bado umekuwa stubborn husikii!!!

Acha kuhurumia malaya hao hakuna kitu watakupa zaidi ya maradhi na headache mwanamke wa kumjali ni mama yako mzazi tu na yule anayefuata matakwa yako nje ya hapo mtoto wa kiume maisha utayaona machungu kama sifongo kwenye dunia hii.
 
Kila siku tunapigiana kelele humu kwamba usimuoe mwanamke kwa sababu ya huruma eti atadhalilika hiyo itaku-cost lakini wewe bado umekuwa stubborn husikii!!!

Acha kuhurumia malaya hao hakuna kitu watakupa zaidi ya maradhi na headache mwanamke wa kumjali ni mama yako mzazi tu na yule anayefuata matakwa yako nje ya hapo mtoto wa kiume maisha utayaona machungu kama sifongo kwenye dunia hii.
Kweli, hutuma sio malezi
 
Endelea tu na maisha bro !
Bora ya wewe umeona, sisi wengine hatuoni yanayoendelea ila tunajipa moyo ingawa nyuma ya pazia kuna mengi mno.
Hata kama usingeona siku ya harusi ipo siku ungeona na pengine ingekuwa mbaya zaidi kuliko siku hio.

Vinginevyo wewe ni mwanaume wa shoka, uanaume haupimwi kwa maumbile kana ndevu sauti nzito nk bali uwezo wa kubeba swala nzito huku ukiendelea na mambo mengine bila wengine kuhisi au kujua, ni wachache mno wa aina yako, hata wazee wetu walikuwa wanafuka 100% lakini walikaza na kuhitimisha kitanda hakizai haramu.

Ila ijuikane mwanamke ni mtu mwenye tamaa ya asili hivyo kama unajihusisha na mwanamke juwa namna ya kukabilia na aina hio ya udhaifu wake.
Mwanamke akiishinda tamaa, ameshinda sehemu kubwa ya maisha yake.
 
Ukaogopa kumdhalilisha yeye ila ukajilipua kujidhalilisha wewe. Kwahiyo waliomuoa mwanzo na kuachana mwanzo walikuwa wanaume ila wewe ukajiona kidume utaweza! Hizi shida umezitaka mwenyewe endelea kupambana nazo
NDOA NI UTAPELI
KATAA NDOA
TUNZA FURAHA YAKO
 
Daah pole sana brother.
Dunia uwanja wa vita, Dunia sio mahala salama sana na sio salama kabisa kwa good guys kama wewe.

Kama mwanaume kataa katu kua good guy, utajuta karibu maisha yako yote, utakumbana na disapointments za kutosha, utaumizwa na kufanywa daraja kwa kila wa karibu yako hasa wanawake.

Huyo mkeo kashakuzidi akili na maarifa, alikutega kidogo na wewe ukajaa, daah pole sana aisee.

Sasa wewe unaogelea kwenye maamuzi kwa kufata hisia, wakati huo yeye anatumia akili ili mwanae na yeye waishi vizuri kupitia koro mmoja ambae ni wewe.

Cha kukushauri ni kua, kwenye kila maamuzi yako utayofanya anza kujiangalia wewe kwanza, sio mkeo wala huyo chalii, anza na wewe kwanza then hao wengine wafate.
Asipokuwelewa hapa ndo basi tena, salama yake ni kukaa mbali na huyo mwanamke haijalishi mtoto ni wake au lah.
 
Kwa nini binadamu tupo judgemental sana? Mtu mwenyewe humjui?
Kaomba ushauri. Kama unalo la kumshauri do. Kama huna pita pembeni. You don't need to judge him.
You judge their thinking. Mwanamke alikuwa demu wake akamuacha kwenda kuolewa, akaachika akaolewa kwingine akaachika anarudi kwako eti unamuoa kisa huruma?
 
  • Ndio maana wazee waliwachagulia vijana wao wenza.
  • Demokrasia (uhuru wa kuchagua) ni utaratibu mzuri ila unahitaji jamii iliyostaarabika vilivyo - yenye akili na nidhamu.
 
Back
Top Bottom