Wakili wa shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2022
- 1,726
- 3,391
Siku moja milimtembelea jamaa yangu kwenye ofisi yake ya kuuza tisheti za mtumba. Yeye huwa anafungua mabelo. Sasa anachofanya, anatoa nguo nzuri anatundika pale ofisini. Zingine zinazobaki anaweka mezani watu wachague kwa bei moja. Labda bukubuku au buku mbilimbili. Ni nguo nzuri nazo, nilikuwa napata form six nzuri tu kwa buku.
Sasa zile za mezani wanakuja mahustlers. Wanajuana na mwenye ofisi. Wanachagua nguo kadhaa labda kumi na kuondoka bila kutoa hata mia. Wanazunguka huko, jioni wakati wa kufunga wanarudi. Anahesabiwa. Labda kauza tano, basi tano zilizobaki anarudisha mezani na kumpa bosi elfu tano au elfu kumi ya alizouza.
Hapo yeye unakuta kila nguo kauza hata 5000. So unakuta ana elfu tano au kumi yake kaingiza. Mtaji mwendo.