Nilijikuta naishi maisha ambayo sikuyategemea ila sina jinsi

Nikiwa kama katibu wa watoa pole TZ nasema pole sana bibie. Mungu yu pamoja nawe. Komaa tu na wanao ipo siku moja ya hao watoto atatokea Dimond Platnumz na utasahau yote. Sisi wanaume huwa tunazuzuka sana na mbususu mpya, jinga sana sisi.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamiiforum wangeweka utaratibu wa wao kudhibitisha identify ya mtu, kisha wanaoguswa wakaweza kumsaport mtu kwa account ya jamiiforum, wengi wanapitia magumu ambayo kwa kidogo mtu alichonacho kingeleta relief.

All in all pole sana dada angu.
Wazo zuri sana mkuu
 
Ila wakati mwingine bila kutumia data za nje ambazo hatuna. Umeacha mtoto miaka miwili hujui kala nini au kanywa nini unarudia baada ya miaka miwili unataka kutoa huduma huo ni ujambazi. Miaka miwili walikufa kwa njaa utawakutia wapi?. Tuache kumlaumu mtu aliyeachiwa watoto miaka miwili bila kujua kama wanakula au wanakunywa nini. Mimi nina mfano tofauti kidogo ila unafanana. Kuna mtu alimpa mimba dada yangu miaka nane iliyopita. Amefika muda wa kwenda kujifungua akamleta nyumbani mwenyewe kwa miguu yake na kuomba wazazi ajifungue halafu atawafuata. Leo ni miaka 9 toka aache binti mjamzito na hajawahi kurudi kufuatilia kama walifia hospitalini au lah. Alienda akaoa sasa ana watoto wawili. Huyu mtu kunasiku atakuja kutulaumu tumemuibia mtoto wakati hajui anakula nini, anakunywa nini wala anafananaje? Huwa namuwaza namuona ni moumbavu. Umegombana na mama wa mtoto njoo ona kilichozaliwa. Ulimuacha kwa wazazi so inabidi ukamuone huko huko ulikomuacha. Simlaumu huyu dada. Muacheni tu maana hamjapitia bado. Miaka miwili watoto walikufa kwa njaa full stop.
 
Pole sana.

Dada msamehe mmeo maisha yaendelee..binadamu hufanya makosa ili tunasamehe tu na wala hatusahau kama ulivyosema wewe..kusahau mambo mabaya huwa haiwezekani ila huwa tunasemehe na kuachilia maisha yaendelee..hao watoto wakikua ipo siku watamtafuta baba yao so ni bora uruhusu tu baba yao aanze kuwatunza..

Pia kama upo Dar jaribu kuhamia maeneo ya pembezoni mwa mji kama Chamazi,Gongolamboto,Bunju,Mbagala,Kibamba n.k huko kwa elfu 60 utapata angalau vyumba viwili vya 30 30..utatumia kimoja na watoto watatumia kimoja.


Pole sana kwa yote
 
I second you....

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Hii hadithi yako umeimaliza haraka bila kuihitimisha! Unataka tukusaidie nini? Inaelekea kwasasa tatizo lako ni kipato kidogo kisichokuwezesha kuwa na vyumba viwili ili wanao wapate chumba chao si ndio? Kaza buti mama ongeza kipato mradi isiwe kwenye vikoba!
 
Maisha ni safari ndefu dada. Mshukuru Mungu kwa kila jambo, ingawa ninyi wanawake mlio wengi huwa hamjitambui. Naamini kuna mwanaume anaweza kuja kwako tena ukahisi umepata tulizo kumbe unaingizwa chaka.

Nakuomba uwe makini sana, usijefanya kosa jingine tena.
 
[emoji253][emoji253][emoji253][emoji257][emoji257][emoji257][emoji257][emoji1651][emoji255]

Maua yako hayo hapo

Haya malizia story

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…