Nilijikuta naishi maisha ambayo sikuyategemea ila sina jinsi

Jamiiforum wangeweka utaratibu wa wao kudhibitisha identify ya mtu, kisha wanaoguswa wakaweza kumsaport mtu kwa account ya jamiiforum, wengi wanapitia magumu ambayo kwa kidogo mtu alichonacho kingeleta relief.

All in all pole sana dada angu.
 
Mimi sina tatizo na yeye, nilisha yaacha yapite ndio maana sijihangaishi hata kutaka chochote kutoka kwake wala kujua anakoishi. Na kuhusu watoto wake wala sijawaambia ubaya wowote na wala hawaulizi chochote. Ila mimi kumsikiliza kwa namna ya kuyajenga haitakaa itokee chini ya jua hili hata kwa bahati mbaya.
 
Dah pole sana kama umeweza kupambana miaka yote hiyo bila yeye.... Naamini Uta survive tu. Jipe moyo na subira naamini utavuka hiyo hatua.
 
Yaani kwa hiyo pesa unayolipa kodi hapo (60,000). Huwezi kupata vyumba viwili maeneo mengine tofauti hapo ili uepuke hiyo kadhia ya kulala na watoto wa kiume chumba kimoja, mwisho uwaachie laana.
Tatizo linakuja wenye nyumba wanataka kodi ya miezi 6 kwa mkukupuo, hata nikipata vya 30000 sitaweza kulipa pesa yote kwa mkupuo hapa nalipa mwezi mmoja mmoja tu
 
Pole sana mpenzi! nilichogundua ukiwa kwenye hali ngumu na yenye majonzi watu uliowategemea hukukimbia,

Ila Mungu anatokeza mtu mmoja tofauti na wao ili kukupa faraja.
Jiombee mwenyewe, ombea kazi yako, ombea watoto wako.

Mungu wa faraja atakupa faraja na kukusaidia zaidi.
 
Pole sana dada!

Ninaomba kukushauri. Kama mume wako amekutafuta na ametaka mzungumze, msikilize.

Kwa uelewa wangu, kukataa kumsikiliza unafanya kosa, kosa zaidi. Kwa kusema hauwezi kuonana nae unaharibu akili yako; unajiadhibu mwenyewe.

Kwa hiyo, kwa msimamo huu, kama ndio dhamira yako, unashiriki kwenye makosa yaleyale; nawe unakuwa mkosaji hata kama haukuwa na kosa.

Msamaha sio kusema nimekusamehe au nimesahau nilitendewa au kutenda, bali hali hiyo ni lazima uifanye iwe vitendo au matendo.

Dada, msamaha ni mlango wa mema yote, ni nguvu ya kupata chochote; ni pia uponyaji.

Anae samehe anamkaribisha Mungu ndani yake.
 
POLE sanaa lakini yule bwana alikosea sana pia nadhani ni hasira tokana na yale maneno shukuru Mungu aliondoka tu maana wengine wanafikia hatua ya kuwaua watoto. Aliporudi ungemsikiliza anachotaka kusema maana kitendo cha kuondoka mpaka na vitu ina maana aliamini kabisa HAO WATOTO SIO WAKE maana wanaume huwa tunaondoka na nguo tu kama mtu unaona umeshindwana nae mali watatumia watoto may angekupa support ya maishaa maana kama miaka 5 imepita bado una changamoto hata ya kodi jishushe ila kama akileta story za kifala na sio support achana nae jumlaa. pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…