Mrs Thabo Bester
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 3,145
- 7,921
Oh kumbe kasema hakuheshimu ndoa yake?Pole. Napata somo kwamba, ukiwa kwenye ndoa, heshimu ndoa yako.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Oh kumbe kasema hakuheshimu ndoa yake?Pole. Napata somo kwamba, ukiwa kwenye ndoa, heshimu ndoa yako.
Dada wanaume wanabembelza sana usiseme hvyo,, na vp kuhusu mahusiano mapya unamtu?Mimi sina tatizo na yeye, nilisha yaacha yapite ndio maana sijihangaishi hata kutaka chochote kutoka kwake wala kujua anakoishi. Na kuhusu watoto wake wala sijawaambia ubaya wowote na wala hawaulizi chochote. Ila mimi kumsikiliza kwa namna ya kuyajenga haitakaa itokee chini ya jua hili hata kwa bahati mbaya.
Sio Mimi mkuu. Sii mjinga. Wadada kama huyu wengi saana. Na wanaliwa Sana Kwa sababu ya shida ya maisha.Nikiwa kama katibu wa watoa pole TZ nasema pole sana bibie. Mungu yu pamoja nawe. Komaa tu na wanao ipo siku moja ya hao watoto atatokea Dimond Platnumz na utasahau yote. Sisi wanaume huwa tunazuzuka sana na mbususu mpya, jinga sana sisi.
TechnicalHajaomba msaada mkuu. Kaja tu kushusha nzigo apate relief
Sio Mimi mkuu. Sii mjinga. Wadada kama huyu wengi saana. Na wanaliwa Sana Kwa sababu ya shida ya maisha.
1. Inakuaje hujui unalipa sh ngapi Kodi na mwez ni wangapi.
2. Vipi hauwi mnyenyekevu kwa kiongozi wa familia yaani mumewe.
3. Kwa nini unalea watoto pekeako. Maana mumeo asingekuacha nao.
Kuna vitu vingine ni sensless kabisa humu tunatumia fake IDs hatujuani Kwa lolote alafu ujizushie habari ya uongo Kwa watu wasiokujua Wala usiowajua ili iweje ? Mtu kashusha mzigo wake angalau apumue halafu wanatokea judges with no honorHapa naona bondia ni ww mwenyewe,refa ww mwenyewe,shabiki ni ww mwenyewe na uwanja ni WA kwako..umeamua kujipa ushindi na kumwonesha uyo mwanaume ndio shida.
Tunasubir upande wa pili nao uje.
Pole sana dada!
Ninaomba kukushauri. Kama mume wako amekutafuta na ametaka mzungumze, msikilize.
Kwa uelewa wangu, kukataa kumsikiliza unafanya kosa, kosa zaidi. Kwa kusema hauwezi kuonana nae unaharibu akili yako; unajiadhibu mwenyewe.
Kwa hiyo, kwa msimamo huu, kama ndio dhamira yako, unashiriki kwenye makosa yaleyale; nawe unakuwa mkosaji hata kama haukuwa na kosa.
Msamaha sio kusema nimekusamehe au nimesahau nilitendewa au kutenda, bali hali hiyo ni lazima uifanye iwe vitendo au matendo.
Dada, msamaha ni mlango wa mema yote, ni nguvu ya kupata chochote; ni pia uponyaji.
Anae samehe anamkaribisha Mungu ndani yake.
Kwenye kumsikiliza siafikiani na nyie aisee.POLE sanaa lakini yule bwana alikosea sana pia nadhani ni hasira tokana na yale maneno shukuru Mungu aliondoka tu maana wengine wanafikia hatua ya kuwaua watoto. Aliporudi ungemsikiliza anachotaka kusema maana kitendo cha kuondoka mpaka na vitu ina maana aliamini kabisa HAO WATOTO SIO WAKE maana wanaume huwa tunaondoka na nguo tu kama mtu unaona umeshindwana nae mali watatumia watoto may angekupa support ya maishaa maana kama miaka 5 imepita bado una changamoto hata ya kodi jishushe ila kama akileta story za kifala na sio support achana nae jumlaa. pole sana
Thibitisha jinsia yakoAsante, ila sidhani kama kuna sehemu nimeomba mchango. Japo kama unataka kusaidia na kujua kama mimi ni ke na nayosema ni kweli naweza kukuthibitishia.
Eeeh!SIKUZOTE USIMUAMINI MWANAMKE hasa anapojieleza kuhusiana na misukosuko ya ndoa yake au mahusiano au na mume/mpenz wake... Ni waongo wanafki watafuta huruma tu...
Nimeomba stahiki? Kisa cha kuachana ni kirefu sana na sitaweza kukiweka hapa, umri wangu ni zaidi ya miaka 30Kisa Cha kupewa RED CARD na aliekua mumeo hujaeleza, maelezo ya mumeo umeeleza kidogo kwa kificho sana, scenarios zimefichwa fichwa, nini chanzo cha mgogoro umesema mtoto Ila mbele unasema mumeo anasema anawapenda watoto wake Ila anaishi na mchepuko wa mda mrefu, dini yako hujasema umri pia umeficha umri wa mumeo umeficha, mumeo alikimbilia wapi umeficha, Sasa sisi maafisa ustawi wa jamii, mahakimu, majaji, mawakili na wanasheria wa JF tunakusaidiaje kupata sitahiki zako ?
Pole kwa majangaNiliachana na aliyekuwa mume wangu miaka 5 imepita, kuachana kwetu kulikuwa kubaya sana kwa mambo mabaya yaliyopita katikati yetu. Sipendi kuyaeleza maana ni mabaya ila nilishayasahau na kuyaacha yapite.
Baada ya kuachana (aliondoka bila kuniaga na kodi ikiwa tunadaiwa miezi 5 bila kulipa) nilibaki na watoto huku nikiwa sina pa kuishi kwani mwezi 1 baadaye mwenye nyumba alinitaka kumuachia vyumba vyake, sina kazi, sina hata kitu kimoja kwa kuwa aliondoka na kila kitu hadi nguo zangu na za watoto na kwenda kusikojulikana alihama nikiwa sipo.
Kabla ya yeye kuondoka nilikuwa sijui kama tunadaiwa kodi, kwa kuwa kodi ya mwanzo ilipoisha alinambia kuwa kodi imeisha na yeye hana pesa kwa kuwa kazini kwake wamepata hasara analipwa nusu ya mshahara ambao ndio tunatumia kujikimu nyumbani.
Tukashauriana nikope pesa kwa ndugu yangu ambaye amekuwa akitusaidia kutukopesha pale tunapokwama na tunamlipa kidogokidogo, nikamtafuta na akatukopesha, nikamkabidhi 1,200,000 ambayo ndio ilikuwa kodi ya miezi 6 nikajua kalipa kumbe kampa mwenye nyumba kodi ya mwezi 1 tu na nyingine sijui alikopeleka hadi leo.
Sasa alipoondoka ndio mwenye nyumba kunitafuta kuwa nadaiwa miezi 5 hadi siku ile na nimeshaanza mwezi wa 6 ivyo ananipa wiki 1 nimuachie nyumba yake, kumbuka hapo nalala chini mimi na watoto kwa kuwa kila kitu kilishaondoka na yeye. Na nafanya kazi ndogondogo kupata chakula cha watoto.
Nikawaza kurudi nyumbani, Kilichonishangaza ni kuona ndugu zangu wote hawapokei simu zangu na wakipokea wananilaumu tu kuwa nimeyatafuta mwenyewe na nisiwasumbue na wanakata simu. Nikawaza nimeyataka yapi? Nimekosea nini? Mbona changamoto zangu pande zote wanazijua kulikoni nalaumiwa leo, nikajaribu upande wa aliyekuwa mume wangu ndio balaa zito.
Mtu 1 akaniambia unajua kuwa Unatuhumiwa kuzaa nje ya ndoa? Nikahamaki, akaendelea kusema baba fulani amewaambia ndugu zako na zake kuwa mtoto huyo mdogo sio wa kwake na ndio maana kaondoka. Nikamwambia hapana haiwezi kuwa kweli kwa kuwa sijawahi kutoka nje ya ndoa hata siku moja. Na kama kasema hayo basi ana lake jambo huenda kaamua kuficha mambo yake kwa kunitwisha mzigo maana tayari alikuwa hana pa kukwepea kutokana na mambo yake.
Basi nikatuma ujumbe mfupi kwa ndugu zangu kuwa, nashukuru kwa kuwa nimejua sababu ya nyie kunichukia ila nawaambia siyo kweli na sijawahi kufanya uchafu huo ila nipo tayari wakapime DNA nchi yoyote na ikibainika ni kweli basi wanihukumu nikazima simu ili nipate muda wa kuwa peke yangu kuwaza nini cha kufanya, nikaanza kuwaza cha kufanya nalia peke yangu.
Nikaanza safari ya kutafuta chumba japo sijui nalipa nini, nikapata mama mmoja nikamweleza hali yangu akanambia nakupa chumba ila utakuwa unanilipa mwezi mmoja mmoja sh. 60000 na mwezi huu nakupa ukae bure utaanza kunilipa mwezi ujao, nikaona chumba ni gharama ila kwangu ilikuwa ahueni maana nina mwezi mmoja wa kuanza maisha kutafuta kodi ya watu.
Nikahamia hapo, na wanangu tukaanza maisha, mwezi mmoja baadae nikapata kazi japo haina mshahara mzuri ila inaniwezesha kupata chakula na kulipa kodi ya 60000 kila mwezi, nikaanza kujibana na kununua vyombo, godoro, kitanda, nguo za watoto nk.
Miezi 7 baadaye nikaja kujua alikokwenda yule mwanaume, na kwamba alipohama alihama na mwanamke mmoja ambaye alikuwa mchepuko wake wa siku nyingi wakaanza maisha yao, nilikutana na ndugu wa huyo mwanamke ndiye aliyenipa taarifa hizo.
Baada ya miaka 2, mwanaume huyo alinipigia simu, akidai anataka kuniona kanikumbuka, nikamwambia huwezi kuniona na wala hutakaa ujue naishi wapi, kwa kuwa sikutaka hata waliokuwa wanatufahamu wajue naishi wapi pia, baada ya kumjibu ivyo akasema kwa kuwa hutaki nikuone basi nilichotaka kusema sitasema, japo nilikuwa na lengo la kuonana na wewe ili nianze kukupa hela ya matumizi ya watoto kwa kuwa umekataa na mimi sihudumii hao watoto, nikamwambia kama wameishi miaka 2 bila huduma yako, basi wataishi tu.
Akawa anaendelea kunitafuta kwa namba mbalimbali huku akifoka na kuniita nina kiburi, jeuri, sina adabu kwake, nitakuwa nimepata mwanaume ananipa kiburi nk, mara aseme nitakuwa nimewalisha watoto sumu kuwa yeye mbaya ila yeye sio mbaya anataka kuwatunza ila mimi ndio nazuia. Mwisho alikata tamaa na sasa imepita miaka 5 nikiwa naishi na wanangu.
Inaniuma sana kuishi na wanangu wakubwa sasa ndani ya chumba 1 kikiwa ndio chumba na ndio sebule kwa kuwa sina uwezo wa kulipia zaidi ya chumba 1 ukizingatia ni wa kiume ila sina jinsi najipa moyo kuna siku nitapata nafasi ya kupata walau vyumba 2 wanangu wakalala tofauti na mimi mama yao.
Nimejitahidi kuandika matukio machache kwa kuyakata sana ili nisiwacoshe
Msamehe huyo mme wako mkaribishe mulee Watoto no body is perfectNimeomba stahiki? Kisa cha kuachana ni kirefu sana na sitaweza kukiweka hapa, umri wangu ni zaidi ya miaka 30
Sasa story inakua haijatimia km haina kisa, maana hasingeondoka na kukutelekeza bila chanzo na chanzo hutaki kukisema au ulifumwa na mwanaume mwingine ? Maana kwenye maelezo yako umesema alipokupugia simu alisema una kiburi sababu ya Mwanaume mwingine hapo hapo unasema ndugu zako na ndugu zake aliwaambia umezaa mtoto na mwanaume mwingine kwa hio Ina maana alifuma kitu kinachohusu watoto kutoka kwako uligawa penzi kwa mwanaume mwingine ?Nimeomba stahiki? Kisa cha kuachana ni kirefu sana na sitaweza kukiweka hapa, umri wangu ni zaidi ya miaka 30
Acha zako wewe 5 years zishapita past is gone unaweza kurejesha jeraha kua ngozi ya awali bila kufanya upasuaji ?Msamehe huyo mme wako mkaribishe mulee Watoto no body is perfect