Nilijikuta naishi maisha ambayo sikuyategemea ila sina jinsi

Nilijikuta naishi maisha ambayo sikuyategemea ila sina jinsi

Sijaja kuhukumu mtu, ila nimeeleza kipande kidogo cha mapito yangu, kama unahisi nimekuja kujisafisha au kuchafua mtu pole.
achana nao hao siku zote huwa na neno la kukebehi. Wewe endelea kupambana na si muda Mungu atakufungulia mpaka utashangaa.

Huyo mwanamme anasubiri watoto wamekuwa halafu ndiyo anajifanya yeye ni baba wa kimataifa.

Wanaume wa aina hiyo ndiyo wazungumzaji wakubwa humu.
 
Msamehe huyo mme wako mkaribishe mulee Watoto no body is perfect

Ukipenda kuhukumu , utazidi kuhudumiwa kwa umri wako wa 30+ yrs ndo umri sahihi wa kuishi bila kinyongo Kama unakubali mtumie chumba kimoja wewe na Watoto Wakati mme wako kasema yupo tiyari kutoa support kwa Watoto then wewe unamfungia vioo ndo Nini Sasa?
Nimetangulia kusema kuwa nimeandika kipande kidogo sana cha mkasa wangu kuna mengi makubwa ambayo sijasema na sijasema kwa sababu maalum, ungejua mkasa mzima natumai usingesema habari za kumsamehe,

Nilishamsamehe wala simhukumu, na yeye hana nia ya kutoa support mpaka akutane na mimi labda kwa kuwa sikueleza bayana kukutana kwake ni kwa namna gani si kuonana tu bali tukutane tukiwa wawili nadhani umeelewa maana yake. Kitu ambacho siwezi ruhusu hata siku moja kitokee.
 
Pole sana lakini wakati mwingine kusikiliza habari hatuwezi balance mzani japo wakati mwingine nyie wanawake aisee! tunaishi kwa kuwavumilia sana hasa hasa mwanamke akianza kiburi aaah! Huwa inakata stimu sana, any way pole sana
Niliachana na aliyekuwa mume wangu miaka 5 imepita, kuachana kwetu kulikuwa kubaya sana kwa mambo mabaya yaliyopita katikati yetu. Sipendi kuyaeleza maana ni mabaya ila nilishayasahau na kuyaacha yapite.

Baada ya kuachana (aliondoka bila kuniaga na kodi ikiwa tunadaiwa miezi 5 bila kulipa) nilibaki na watoto huku nikiwa sina pa kuishi kwani mwezi 1 baadaye mwenye nyumba alinitaka kumuachia vyumba vyake, sina kazi, sina hata kitu kimoja kwa kuwa aliondoka na kila kitu hadi nguo zangu na za watoto na kwenda kusikojulikana alihama nikiwa sipo.

Kabla ya yeye kuondoka nilikuwa sijui kama tunadaiwa kodi, kwa kuwa kodi ya mwanzo ilipoisha alinambia kuwa kodi imeisha na yeye hana pesa kwa kuwa kazini kwake wamepata hasara analipwa nusu ya mshahara ambao ndio tunatumia kujikimu nyumbani.

Tukashauriana nikope pesa kwa ndugu yangu ambaye amekuwa akitusaidia kutukopesha pale tunapokwama na tunamlipa kidogokidogo, nikamtafuta na akatukopesha, nikamkabidhi 1,200,000 ambayo ndio ilikuwa kodi ya miezi 6 nikajua kalipa kumbe kampa mwenye nyumba kodi ya mwezi 1 tu na nyingine sijui alikopeleka hadi leo.

Sasa alipoondoka ndio mwenye nyumba kunitafuta kuwa nadaiwa miezi 5 hadi siku ile na nimeshaanza mwezi wa 6 ivyo ananipa wiki 1 nimuachie nyumba yake, kumbuka hapo nalala chini mimi na watoto kwa kuwa kila kitu kilishaondoka na yeye. Na nafanya kazi ndogondogo kupata chakula cha watoto.

Nikawaza kurudi nyumbani, Kilichonishangaza ni kuona ndugu zangu wote hawapokei simu zangu na wakipokea wananilaumu tu kuwa nimeyatafuta mwenyewe na nisiwasumbue na wanakata simu. Nikawaza nimeyataka yapi? Nimekosea nini? Mbona changamoto zangu pande zote wanazijua kulikoni nalaumiwa leo, nikajaribu upande wa aliyekuwa mume wangu ndio balaa zito.

Mtu 1 akaniambia unajua kuwa Unatuhumiwa kuzaa nje ya ndoa? Nikahamaki, akaendelea kusema baba fulani amewaambia ndugu zako na zake kuwa mtoto huyo mdogo sio wa kwake na ndio maana kaondoka. Nikamwambia hapana haiwezi kuwa kweli kwa kuwa sijawahi kutoka nje ya ndoa hata siku moja. Na kama kasema hayo basi ana lake jambo huenda kaamua kuficha mambo yake kwa kunitwisha mzigo maana tayari alikuwa hana pa kukwepea kutokana na mambo yake.

Basi nikatuma ujumbe mfupi kwa ndugu zangu kuwa, nashukuru kwa kuwa nimejua sababu ya nyie kunichukia ila nawaambia siyo kweli na sijawahi kufanya uchafu huo ila nipo tayari wakapime DNA nchi yoyote na ikibainika ni kweli basi wanihukumu nikazima simu ili nipate muda wa kuwa peke yangu kuwaza nini cha kufanya, nikaanza kuwaza cha kufanya nalia peke yangu.

Nikaanza safari ya kutafuta chumba japo sijui nalipa nini, nikapata mama mmoja nikamweleza hali yangu akanambia nakupa chumba ila utakuwa unanilipa mwezi mmoja mmoja sh. 60000 na mwezi huu nakupa ukae bure utaanza kunilipa mwezi ujao, nikaona chumba ni gharama ila kwangu ilikuwa ahueni maana nina mwezi mmoja wa kuanza maisha kutafuta kodi ya watu.

Nikahamia hapo, na wanangu tukaanza maisha, mwezi mmoja baadae nikapata kazi japo haina mshahara mzuri ila inaniwezesha kupata chakula na kulipa kodi ya 60000 kila mwezi, nikaanza kujibana na kununua vyombo, godoro, kitanda, nguo za watoto nk.

Miezi 7 baadaye nikaja kujua alikokwenda yule mwanaume, na kwamba alipohama alihama na mwanamke mmoja ambaye alikuwa mchepuko wake wa siku nyingi wakaanza maisha yao, nilikutana na ndugu wa huyo mwanamke ndiye aliyenipa taarifa hizo.

Baada ya miaka 2, mwanaume huyo alinipigia simu, akidai anataka kuniona kanikumbuka, nikamwambia huwezi kuniona na wala hutakaa ujue naishi wapi, kwa kuwa sikutaka hata waliokuwa wanatufahamu wajue naishi wapi pia, baada ya kumjibu ivyo akasema kwa kuwa hutaki nikuone basi nilichotaka kusema sitasema, japo nilikuwa na lengo la kuonana na wewe ili nianze kukupa hela ya matumizi ya watoto kwa kuwa umekataa na mimi sihudumii hao watoto, nikamwambia kama wameishi miaka 2 bila huduma yako, basi wataishi tu.

Akawa anaendelea kunitafuta kwa namba mbalimbali huku akifoka na kuniita nina kiburi, jeuri, sina adabu kwake, nitakuwa nimepata mwanaume ananipa kiburi nk, mara aseme nitakuwa nimewalisha watoto sumu kuwa yeye mbaya ila yeye sio mbaya anataka kuwatunza ila mimi ndio nazuia. Mwisho alikata tamaa na sasa imepita miaka 5 nikiwa naishi na wanangu.

Inaniuma sana kuishi na wanangu wakubwa sasa ndani ya chumba 1 kikiwa ndio chumba na ndio sebule kwa kuwa sina uwezo wa kulipia zaidi ya chumba 1 ukizingatia ni wa kiume ila sina jinsi najipa moyo kuna siku nitapata nafasi ya kupata walau vyumba 2 wanangu wakalala tofauti na mimi mama yao.

Nimejitahidi kuandika matukio machache kwa kuyakata sana ili nisiwacoshe
 
Nimetangulia kusema kuwa nimeandika kipande kidogo sana cha mkasa wangu kuna mengi makubwa ambayo sijasema na sijasema kwa sababu maalum, ungejua mkasa mzima natumai usingesema habari za kumsamehe,

Nilishamsamehe wala simhukumu, na yeye hana nia ya kutoa support mpaka akutane na mimi labda kwa kuwa sikueleza bayana kukutana kwake ni kwa namna gani si kuonana tu bali tukutane tukiwa wawili nadhani umeelewa maana yake. Kitu ambacho siwezi ruhusu hata siku moja kitokee.
Mkuu kaeni chini mmalize tofauti zenu , unawatesa watoto bure na usitegemee kufanikiwa haya maisha bila kuwa na ushirikiano na watu
 
Inawezekana Unamshauri ujinga mtupu mtoa Mada Kama anajiona matakatifu Mwambie aendelee hivyo Wakati mme wake kasema anaweza saidia Watoto wake so sioni tatizo hapo.
Kashasema ana mwanamke mwingine na anaishi nae, aliwasiliana akihitahi kuhudumia watoto sio kumhudumia mwanamke, elewa scenario kwanza ndio umwage maelezo, kwa kuangalia kwa kina Cha ndani kiini Cha mgogoro ni watoto, huyu mama anataka watoto awalee mwenyewe bila msaada wa mwanaume wake sababu ni machungu ya kukimbiwa kwa hio leo hii hauwezi ukamwambia aishi na mtu ambae aliwahi kumkimbia anachoona ni kukimbiwa mara ya pili
 
Sasa story inakua haijatimia km haina kisa, maana hasingeondoka na kukutelekeza bila chanzo na chanzo hutaki kukisema au ulifumwa na mwanaume mwingine ? Maana kwenye maelezo yako umesema alipokupugia simu alisema una kiburi sababu ya Mwanaume mwingine hapo hapo unasema ndugu zako na ndugu zake aliwaambia umezaa mtoto na mwanaume mwingine kwa hio Ina maana alifuma kitu kinachohusu watoto kutoka kwako uligawa penzi kwa mwanaume mwingine ?
Hongera kwa hukumu yako, hajawahi kufuma chochote, na sina tabia chafu kama unazonihukumu nazo. Pole kwa kuwaza mawazo hasi.
 
Ndio maana Kila siku nasema, Tuanzisheni Kapu la JF , ambalo Ndani yake tutadumbukiza Mia mia tu .

Kwa ajili ya watu kama hawa, Mtoa Mada ni Mama mpambanaji sana ,mwenye uchungu na wanawe .

Niwaombe sana WanaJF wanaume Kwa Wanawake wenye Fursa nyingine za Kazi, mmfikirie , mtoa Mada alipata kazi, Kwa Uwezo mkubwa wa akili na uthubutu Alonao, Hatokaa kuomba Kodi.
 
Anataka aonewe huruma sio
Ndiou
achana nao hao siku zote huwa na neno la kukebehi. Wewe endelea kupambana na si muda Mungu atakufungulia mpaka utashangaa.

Huyo mwanamme anasubiri watoto wamekuwa halafu ndiyo anajifanya yeye ni baba wa kimataifa.

Wanaume wa aina hiyo ndiyo wazungumzaji wakubwa hum

Kashasema ana mwanamke mwingine na anaishi nae, aliwasiliana akihitahi kuhudumia watoto sio kumhudumia mwanamke, elewa scenario kwanza ndio umwage maelezo, kwa kuangalia kwa kina Cha ndani kiini Cha mgogoro ni watoto, huyu mama anataka watoto awalee mwenyewe bila msaada wa mwanaume wake sababu ni machungu ya kukimbiwa kwa hio leo hii hauwezi ukamwambia aishi na mtu ambae aliwahi kumkimbia anachoona ni kukimbiwa mara ya pili
Mnamponza tu huyo Mwambie amruhusu mme wake alee watoto wake Sasa hataki sapport then analalamika ..
 
Hongera kwa hukumu yako, hajawahi kufuma chochote, na sina tabia chafu kama unazonihukumu nazo. Pole kwa kuwaza mawazo hasi.
Huko nimefika ili kujaribu kufumua mafaili lakini unakataa kua sio kisa au chanzo cha mgogoro wenu, Sasa wewe unahisi chanzo cha yeye kukukimbia ni nini ikiwa kwamba unaamini yeye sio kichaa na ni mtu ulimchagua mpaka ukifika uamuzi wa kumzalia watoto Ina maana yupo timamu sio chizi, chanzo cha yeye kukuacha na kukukimbia ni nini, kiburi, majivuno, kujiona, majisifu, kutokumsikiliza au nini ?
 
Sijaja kuhukumu mtu, ila nimeeleza kipande kidogo cha mapito yangu, kama unahisi nimekuja kujisafisha au kuchafua mtu pole.
Kama mzazi mwenzio kaonyesha nia ya kiwasaidia watoto wake kwanini unamzuia? Huoni kama unawanyima haki yao ya msingi
 
I
Hongera kwa hukumu yako, hajawahi kufuma chochote, na sina tabia chafu kama unazonihukumu nazo. Pole kwa kuwaza mawazo hasi.

Anasema hajaleta kulalamika au kuomba msaada ameleta tu km story fupi ya maisha yake, hataki msaada wako wowote hata wa ushauri wewe soma toa pole pia kushoto
Aaah sawa Basi hatuwez kuamini hiz habar
 
Back
Top Bottom