Nilijitoa kufanya naye maisha ila ameniachia wakati mgumu nikiwa na mimba yake

Nilijitoa kufanya naye maisha ila ameniachia wakati mgumu nikiwa na mimba yake

Haya mambo haya tuyaskie tu kwa wengine, omba usikutane nayo. Pole saana Dada yetu
 
Pole sana Mfalme Daudi kwa kutelekezwa na ujauzito..
 
Wanaume hizi siku tumekosa msimamo kimaisha , maisha tunayoishi ni tupo kimwili ila kiakili na kiroho mara nyingi tunaishi mbali na tulipo.

Na hii ni kwa sababu tunamatarajio makubwa sana tunapoanza kufanya maisha

Wengi ni kama ndoto zetu hazijatimia lakini kwa sababu umekwama mahali fulani unaona uishi hapo siku mambo yakikaa sawa unatembea.
 
POLE SANA,,,,,(Binafsi huwa siamini sana Stori ikiwa upande wa Mwanamke,,,hasa hawa wenye kipato chao,,huwa kuna mengi wanaficha kupata huruma ya Jamii....)..

BUT huyo King'ast Marioo amezingua sana kuuza kiwanja,,,,Kapata madusco kidogo ameanza kushoboka na kabichi za mpito...Vijana wa siku hizi ulimbukeni ni mwingi sana,,,na huyo alikuwa anatafuta Maisha kwako,,hakuwa amekupenda tokea awali....

Jikaze,,,,Kubali Matokeo,,na itunze mimba ili ujifungue Salama...,,Jamaa amedharau Nazi,,,akisahau Embe ni tunda la Msimu tu..

..POLE SANA MKUU..,,,Ni Ngumu sana ila Jipe Moyo utashinda.....
 
Yani hii stori ni kama ya jirani yangu kabisa sema tofauti yy kakimbiwa mtt yuko darasa la kwanza, lakini kusema kweli wanaume tunafeli sana unapopata mtu mwenye akili ya maisha shikilia apoapo ata kama ana mapungufu mengine vumilia kikubwa tu ana akili ya maisha mengine mtarekebishana kuliko kukimbilia tamaa za mda mfupi mwisho wa siku unaambulia majuto.
 
Nothing to comment , but believe in God atatokea malaika wa kukubeba,

JF ni taifa lenye watu wakarimu, watakushika mkono.

Mfalme Daud amini kuwa taa yako haitazima,
 
Hiyo laana itamtafuna milele sisi aged kidogo tumeona wengi wa hivyo Huwa Hawa settle kabisa anaweza akashika Hela nyingi tu na still akawa maskini na kuhisi analogwa kumbe wap
 
Tumesikia only one side of the story. Siwezi kuhukumu. I only smell something fishy there [emoji848]. Sijui kwanini...
Ulicho smell mi kinanukia hadi huku. Harufu yake ni kwamba wakati huyu dada anampambania jamaa aligawa uroda kufanikisha mipango kati ya hiyo. Kijana akavuta subra. Mwanaume akiwa kapuku ni mvumilivu sana. Mwanamke akiwa na kipato kuzid mwenzie risk ya mahusiano inakuwa juu maana mwanaume anahisi nguvu zake za asili zinakuwa undermined! Atapima kila kauli, kila tendo, kila kitu kujua kama woman loyalty ipo? Kumbuka matendo mil 72 mema kw mmeo yanafutwa na tendo moja kasorobo la kutokuwa mwaminifu au mtiifu!

Bahat mbaya wanawake hawajui kuchuja kauli zao katika hali hii. Mikakat ya kupigwa tukio huanzia hapo.
Kumbuka mwanaume hawez kuacha mwanamke kisa kimada, mana naturally hajawai kumilikiwa na mwanamke mmoja! Ni rahis kuchepuka na mkaishi salama!

Ushaur wangu ni jipongeze kwa kufanya part yako ya utu wema na songa mbele. Hakuna uwekezaj kwa binadam! Muhim pumzi
 
Mahusiano ya saivi dada ni kuwa na exit plan mapema sana, asikudanganye mwanamme sijui umzalie ndio akuoe, utapigwa na lifatuma kichwani. Mbaya zaidi uko ndani ya mkenge huu ushauri wangu hauwezi kukusaidia.

Cha kufanya ni kupambana tu, jikung'ute vumbi simama songa mbele... Trust me atakuja siku moja akutafute kama anapajua kwenu ipo siku atakuja kukulilia na kusingizia ni shetani alimpitia.

Mimba sio kilema kama wazazi wako wapo wazima wambie hio scenario, wao wameyaona mengi kama hayo watakusaidia tu.

WANAUME TUSIUMIZE WADADA KAMA HAWA WANAOJITOA KWETU NI NADRA KUWAPATA[emoji24]

“WANAUME TUSIWAUMIZE WADADA KAMA HAWA
WANAOJITOA KWETU NI NADRA KUWAPATA.”
 
Daaa pole sister mwenye bahat habahtiki mwanaume mwenzetu katuangusha Sana unapata mpambanaji anaejua nin maana ya maisha unamfayia hivi kweli
 
Back
Top Bottom