Nilijitoa kufanya naye maisha ila ameniachia wakati mgumu nikiwa na mimba yake

Nilijitoa kufanya naye maisha ila ameniachia wakati mgumu nikiwa na mimba yake

Jina lake ndiyo hilo analotumia nenda FB waambie ndugu zake.
 
Ahahha sio poaa kaka, haya mambo mepesi ukisimuliwa tuu
Hamna wepesi kaka, tatizo kubwa sana hilo kwenye jamii yetu. Ila nina imani wanawake watachukua usukani na kuwa viongozi mambo ya kujilinda na kuzaa kwa kutegemea tu uwepo wa baba mtoto... bora wazae wakiwa tayari kwa lolote ili mtoto awe na kesho salama na uhakika zaidi.
 
Kitu ambacho siwezi kutelekeza ni damu yangu. Hata mwanamke awe yeye ndio tatizo ila mwanangu atahudumiwa! Mwamba kazingua sana!
 
Mada za wakina ROBERT HERIEL na The unpaid Seller zimenifanya niweje yaani.

Any way! Pole sana dada yetu, Mungu siku zote ni mwema, tena ni mwema mno jua tu utavuka salama kabisa.

Nitakujia Chemba ni kusupport kwa chochote kitu.
 
Kosa lako lipo sentensi ya kwanza tu.Pole
 
Hii story umeitoa kwa idd makengo au?
Umeniwahi. Ina dalili zote za TATEPA hasa kule mwishoni [emoji16][emoji16][emoji870][emoji870]
Screenshot_20220617-135524_Google.jpg
 
Mfalme Daudi natanguliza pole ikiwa usemayo ni kweli ila ikiwa kuna mengine pia pole binadamu hatujakamilika si wewe wala si huyo ndugu yetu.

Dada rejea comment katika post yako , kuna mtu ameahidi njia ya kuepukana na malipo ya hao wenye solar ili upunguze machungu ya majukumu yanayokuandama , mtafute tafadhali alafu iuze hiyo solar ikusaidie kwenye mambo mengine.

Dada ukibahatika kuuza solar , hakika deni la mkopo wako utaweza kulilipa ila bada ya hapo , jikaze umpate unayemuamini katika mgahawa wako ili uendelee kupambana , mimba miezi sita bado kwa kiasi chake hivyo mtafute msaidizi katika mgahawa wako kabla ya siku za uchovu wa mimba kuzidi.

Dada Mfalme Daudi natambua umeathirika kisaikolojia juu ya huyo mwanaume , Ndugu yangu jikaze ni wakati mgumu ila nikukumbushe kuwa muda ni mponyaji mzuri , jitahidi kuwqza ya kuwa mlikuwa wote ila sasa hayupo tena ...

Pole sana ndugu , amka simama endelea na mwendo hajakuangusha ila kakuimarisha

Ushauri tu.

TEKERI.[emoji120][emoji120]

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Pole sana. Huwa wanaondokaga. Kuwa makini, lea hio mimba usimuathiri mtoto.
 
Pole sana mpendwa, inasikitisha sana lakini usikate tamaa endelea kupambana muombe sana Mungu akuvushe katika hiyo changamoto unayopitia, Mungu akusaidie.
 
Pole sana Mfalme Daudi kwa kutelekezwa na ujauzito..



Mfalme Daudi mwanamke?

Huyu ana matatizo kwenye akili yake ndio maana jamaa amemtelekeza na mimba!

Huyu hana tofauti na yule anayejiita mfalme Zumaridi wa Mwanza.
 
Kwani alikuoa?

Au alikubaka ?

Ingekuwa mke hizo lawama ningezielewa lakini hakukuwa na commitments za kukuoa Kwanini ulijirahisisha na kujichanganya kiasi hicho?

Kwani kila mahusiano ya mapenzi ya Mwanaume na mwanamke lazima yapelekee kuzaa ?

Wengine wanapita tu , wengine urafiki tu n.k

Kalenda ya uzazi anayo nani Mwanaume au mwanamke?

Ukute mwenzio ana mke wake huko mahali wewe hukustuka
Ukatia akili ukajua umepata kumbe umepatikana.

Au hakukupenda alikuwa anapita tu!
 
Back
Top Bottom