Nilikamatwa Morogoro stesheni ya SGR nikituhumiwa kusafirisha chupa ya mil.500 ya maji ya kunywa!

Mkuu, hizo ni sheria kwenye biashara, hata kwenye ndege hupandi na maji, uwe ulaya au bongo,
Na huko ni CCM ?
Unajua sababu ya kutokupanda na maji kwenye ndege?. Hizi treni ziko ulaya kitambo sana na hawana huu ujinga.
 
Muda wote maji ni dawa tosha na haihitaji kumuuliza mtu kama anakunywa maji au la, siku ikikutokea dharula ya kuishiwa maji mwilini ndipo utakapojua kuwa ni lazima muda wote uwe na chupa ya maji.
Ndani ya treni yapo yakutosha sana gentleman 🤣

kuna wanaoingia na visungura 🐒
 
Afadhali hayo maji. Kuna mtu alinunua asali lita moja aende nayo Dar. Kwenye kupitisha kwenye scanner wakaiona. Eti wakamwambia aiache au ainywe yote lakini hakuna kuingia nayo kwenye train!!!! Hapo ndipo niliona hawa wafanyakazi wa SGR ni mataahira!!!! Sasa walitegemea huyo mtu angekuwa analamba hiyo asali ndani ya train? Hata common sense hawana.
 
Ukitaka ujue Watanzania bado kiza ukipita Mtera dam utasikia msipige picha hapa na wanaopiga picha wanawasumbua wakati Dunia imezungukwa na satellite ambayo inaweza kuchukua picha hata ya sisimizi popote pale juu ya uso wa Dunia..
Moja ya dalili ya ujinga ni kutojua nini cha kuzuia na nini cha kutozuia. Nini hatari na nini siyo hatari. Mwishowe unaona bora uzuie vyote ili usiumize kichwa. Hapo Mtera hata wangeweka utalii watu wapige picha walipe hata 3,000. Wangepata chochote kitu.
 
Hivi hii imeletwa kama luxury au usafiri wa UMMA ili kusaidia walipa kodi ? Sababu naanza kuona badala ya Serikali kutoa huduma imegeuka kuwa Mfanyabiashara
 
Zipo damu kubwa kuliko Mtera kama Livingstone ya Zambia au ile ya Mozambique watu tuna Enjoy hayo maeneo bila kikwazo chochote Wabongo sasa kwa uongo usipige picha hapa eti Mtera unabaki kushangaa tu.
 
Zipo damu kubwa kuliko Mtera kama Livingstone ya Zambia au ile ya Mozambique watu tuna Enjoy hayo maeneo bila kikwazo chochote Wabongo sasa kwa uongo usipige picha hapa eti Mtera unabaki kushangaa tu.
Mbona hata daraja la Salenda Dar. nalo ni marufuku kupiga picha!
 
Mkuu, hizo ni sheria kwenye biashara, hata kwenye ndege hupandi na maji, uwe ulaya au bongo,
Na huko ni CCM ?
Exposure ni muhimu sana,sidhani kama watakuelewa hawa wajuaji..
 
Mbona hata daraja la Salenda Dar. nalo ni marufuku kupiga picha!
Mimi sijui mkuu hapa dzonga napiga picha popote hata Ikulu ya Ramaphosa ukitaka ukapige picha unapiga tu enzi za Mbeki ilikua unaenda mpaka juu kule kwenye ofisi zao sema baada ya September 11 wakasitisha hizo mambo..Walinzi hauwaoni ila ni sehemu ambayo unakanyaga camera bila kujijua..
 
Inashangaza. Mtu "kayaficha" maji yake kwenye begi, labda hana mpango wa kuyatumia ndani ya treni. Lengo lake akayatumie mbele ya safari, ameathiri vipi biashara ya vinywaji/vyakula vyao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…