Nilikopa milioni 10, siku naona salary slip yanipasa kulipa 24m jicho la upande wa kushoto lilijifunga kama dakika 40 hivi. Nilijua limeparalyse!

 
Wala siyo kweli. Ina maana hukujaza Mkataba mpaka usubirie slip? Maana mkataba huainisha kiasi chote unachopaswa kulipa.

Na hakuna benki Tanzania inayotoza riba ya zaidi ya asilimia 100. Hakuna.

Hii ni Chai.
Mkuu hizo taasisi za hovyo hawatozi 100/% kwa maneno kuwa unalipa 100/% hapana

Wanakuambia riba ni 20% unaona yes milioni 1 kwa milioni na laki 2 mkopo ni wa mwaka huu nauweza

Sasa dadeki ukishachukua mkopo baade sana unaona deni haliishi kuuliza vizuri ndo unagundua RIBA ni 20% ukizidisha mara miezi 12 ya mkopo unajikuta umekopa mkopo kwa jumla ya riba ya 240/%

mtindo wao riba za asilimia zinakatwa kila mwez
Kuna hawa wa mitaani sijui kausha damu
Ao mamazae kwa hawa dadazetu hawajaenda shure wanakatwa riba kila siku
Ni ile unasema unasema mm narudisha mkopo wenu wote kwa pamoja Qumam@e zao hawataki wanataka umenyeke
Ukiona waalimu wanachukuliwa ATM zao usiwaone wajinga hapana ni kama hayo yalomkuta jamaa
 
Hii itakuwa ni bayport ingekuwa bank Kama Nmb au crdb ingekuja kwenye 17
CRDB ipi unaizungumzia, kuna mtu alikopa 24M baada ya mwaka aka-update mkopo na kupata 12M kwa muda wa miezi 72. Marejesho mpaka akamilishe hiyo miezi 72 ni 68M. Biblia ilishalaani mambo ya mikopo ndiyo maana wenzetu waislam wana Islamic banking ambapo hakuna riba. Akopaye humtumikia bwanake.
 
Wakopaji wengi huanza kulalamika baada ua kutatua changamoto zilizokuwa zinakabili mkumbuke hiyo ni kama biashara zinginge na mbaya zaidi hii hiashara i atolewa macho na wengi
Kimahesabu iko hivi
24,000,000 -10,000,000=14,000,000faida ikijumlishwa na garama za bima na uendeshaji wa biashara yenyewe
14,000,000 itakuwa imepatikana baada ya miezi 96 (ambayo ni miaka 8)
Ukiigawa hiyo kwa namna unalipa wewe
14,000,000÷96 miezi =145,800 hii ni kila mwezi unachangia ndipo ufikishe hiyo 14m kwahiyo kazi ya mkopeshaji ni kujuombea usifukweze kazi na usife ili asije poteza hela yake
Kwenye hiyo 145800 ndipo anatakiwa kulipia garama zote za uendeshaji kwa mwezi kinachobaki ndio kinaitwa faida na sio 14m yote anaipata kama faida kwa kukusanya kwa hiyo miezi yote 96 kuna mambo mengi katika kukopesha
Wengi wenu mnaona kuwa hii biashara ina faida sana ukiingia kukopesha utapigwa chap wanakukalisha pembeni
Hata mabenki mengi yanafilisika au kuteteleka kwakupitia mikopo zaidi
 
Wajinga sana hawa mabenki. Wakati unakopa waakataa kukupa mchanganuo wa hela yote utakayolipa, na kwa kuwa una haraka na shida ya hela inabidi uchukue tu bila kujua utalipa nini. Siku salary slip imetoka ndio utaipatapata.
 
Karibuni betting
Jana nimetengeneza 40k
Leo mapema kabisa 50k
Mtaji 10k
Faida 80k


Sasa wewe mtumishi unalalamika unadaiwa million 24 na umepata pressure

Mimi nadaiwa million 56 na Nina mpango wa kuilipa mwishoni mwa mwaka huu ili mwakani nikope million 400
 
Mkuu ushauri wako hauna maana,mfumo wa kiuchumi (maendeleo) wa Dunia upo katika mfumo wa Mikopo,without loan hakuna Uchumi,hakuna maendeleo.

Wewe sema ulienda chaka kutokana na uelewa finyu ulionao katika mikopo, na sio kwamba mikopo ni mibaya
 
Ila ndo 10M kwa 24M ? riba 100%+ huu ni wizi aisee
fuatilia hili suala mkuu, itakuwa ulislid chap terms and condition hadi kwenye "I agree"
 
Enzi za ubora wangu kuna jamaa alikuwa ananidai 11m na mambo yalikuwa yamenikaba hatari sina pa kutokea. Huyo jamaa nae alikuwa mtata balaa. Siku moja kuna roho ya ajabu ikanijia na kuniambia nimpigie jamaa nimkope tena.. kweli nikampigia simu na kumwambia nataka tuonane tuongelee deni. Tumekutana na jamaa akadhani nataka nilipe nikamwambia aniongezee 5m ili nirekebishe makosa ya kwenye biashara ili mambo yaende na ile 11m nitalipa kirahisi. Alipaniki hatari ila baada ya kumpa facts za kutosha akanipatia 4m. Nilikuja kumlipa baada ya mwaka mmoja hela zake zote. Muhimu anayekudai usimkimbie wala kukatisha mawasiliano naye.
 
Benki gani hiyo... Mbona hakuna riba ka hiyo...!??

Labda kama walinunua mkopo mwingine..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…