Nilikopa milioni 10, siku naona salary slip yanipasa kulipa 24m jicho la upande wa kushoto lilijifunga kama dakika 40 hivi. Nilijua limeparalyse!

Kwa mkopo wa miaka 8 yaani Ile mikopo ya unafunga ndoa unazaa mtoto yupo darasa la tatu ndo mkopo unaisha riba hio ni sawa.
Mkopo ni laana Kama sio lazima ya ugonjwa au kusoma acha na kukopa bora ujenge taratibu taratibu.
Mkopo usizidi miaka 3
Mkopo wa miaka 8 ni uwendawazimu aisee. Huwa najiuliza watu huwa hawapigi hesabu kabla ya kuchukua mikopo? Inatia hasira sana kuona mtu anachukua 5m na kulipa kwa miaka mingi bila kujali analipa Tsh ngapi
 
Siyo asilimia 100 tu.Ni asilimia 140!Na hapo bado haujakutana na akina Faimbweka, Bayofpigs, Platedamnit nk. Huko mikopo ukisha kopa huwa haiishi. Watakukata maisha yako yoooteeee. Damnit!😂😂😂😂
Wale ndo nyonyadamu wenyewe kuna kina tujiezeke wacha kabisa hawana huruma ndoa ya kikristo life time makato
 
Tusitishane jamani interest rate kwa mwaka ni Kati ya 16% mpaka 18% kwa mwaka kwa mabenki haya tunayoyafahamu. Ukizidisha hiyo Rate na let say miaka mitano ya kulipia bado haifiki hata 100%. Ukute mtoa Mada alitaka arudishe pesa ndani ya miaka kumi.
Hakuna marejesho ya miaka 10..
Huyu jamaa muongo
 
Mkopo wa miaka 8 ni uwendawazimu aisee. Huwa najiuliza watu huwa hawapigi hesabu kabla ya kuchukua mikopo? Inatia hasira sana kuona mtu anachukua 5m na kulipa kwa miaka mingi bila kujali analipa Tsh ngapi
Inakuwa Kama Wanapofika Kukopa Wanapoteza Network Wanakuwa Mjumbe Ndiyo Kwa Kila Kitu. Sehemu Nyingine Wanaweka ATM Card Kabisa
 
Eneo hill la mikopo linaumiza watu wengi sana kwasababu shida ikikutinga mambo mengi huyazingatii pia inakuwa siri lakini ukweli upo palepale Bank zinaendeshwa Kinyonyaji na unyonyaji umejificha kwenye masharti yaliyoandikwa kwa herufi ndogo.

Tunauenzi Ubebari tulioupiga vita Sikh nyingi mfano ukiambiwa mkopo wako ni asilima 10 ya pesa unazodaiwa hata ukilipa pesa ikapungua bado wao wanakata hata pesa uliyokwisha lipia.

Mfano ukikopa 10 mil. Makato ya liba ya 10 mil yataendelea hata kama deni limebakia lakini moja.
 
Q😆😆😆hiyo ilikuwa Stroke
 
Kumbe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…