Nilikopa milioni 10, siku naona salary slip yanipasa kulipa 24m jicho la upande wa kushoto lilijifunga kama dakika 40 hivi. Nilijua limeparalyse!

Nilikopa milioni 10, siku naona salary slip yanipasa kulipa 24m jicho la upande wa kushoto lilijifunga kama dakika 40 hivi. Nilijua limeparalyse!

Mkopo wa miaka 8 ni uwendawazimu aisee. Huwa najiuliza watu huwa hawapigi hesabu kabla ya kuchukua mikopo? Inatia hasira sana kuona mtu anachukua 5m na kulipa kwa miaka mingi bila kujali analipa Tsh ngapi
Kama unaizungushia kwenye biashara unajikuta unatengeneza pesa nzuri kuliko hio unayo warudishia
 
Nyumba nyingi za Wafanyakazi wa Serikali zina gharama kubwa sababu ya mkopo wa muda mrefu japo nyumba husika akisema aiuze atauza kwa bei ndogo kuliko mkopo.

Unakuta nyumba ya milioni 30 anachukua mkopo ambao analipa jumla 68
 
Ukikopa 10m kwa riba ya 17% kwa muda wa 6 years, utatakiwa kulipa Jumla ya 25+m. Mikopo inatumika hesabu za future value of money. Yaani thamani ya 10m ya leo kwa miaka sita itakuwaje?
Kwani hiyo miaka 6 ijayo bado itakuwa mil 10 deni?
 
Hesabu za benki haziko hivyo. Ni kweli riba inategemea muda ila calculations siyo hizo za simple interest, ukiambiwa benki riba ni 17% unaweza kukuta ni 9.5% kwa hesabu za kawaida.
Benki nyingi zinatumia Non Reducing Calculator na makanuni mengine ya kiuchumi.

Kwa mfano mimi nilikopa nmb 6,100,000 kwa riba ya 17%, kwa miaka 3 ningetakiwa nilipe 9.2M ila nlilipa 7.8M, sasa piga hesabu uone.
Kwa hesabu za fasta umelipa riba 28% na sio 17 % kama unavyosema , hapo zinaongezeka vipi ,kwa nini kwenye mkataba wa mkopo hawaelezi haya ??
 
Bado haingii akilini ulipe mara mbili ya deni.
Muda wa mkopo ndiyo uhamua gharama ya mkopo kwa u Jumla wake. Kadri muda unavukua mrefu na marejesho uwa makubwa (riba haibadiliki)
 
Hii ni chai hakuna riba ya bank unaweza chukua 10 ukalipa 24 m kama riba haipo mkuu...riba ni 13% kwa bank nyingi...hiyo milion 12 imezidi saana haiwezi zidi 5m kama riba..ambapo riba plus interest unaweza kulipa milion 17 hapo umedanganya umma

Ila kama ulichukua kwenye sacoss ni kweli saccos riba zao ni kwa mwezi..ila bank riba zao ni annualy
Ipo mkuu sema hujui

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Acha kabisa aisee!

Nikiwa nimepagawa na changamoto iliyokuwa inanikabili bila kujua la kufanya, nikakimbilia benki moja kuomba mkopo. Kufika pale nikamuambia afisa mikopo kuwa nahitaji m15, akaniambia m10 ni utapata lakini si hizo ulizotaka. Nikaona kheri tu itaokoa kitu tena kwa kiasi kikubwa sana tu.

Wakati huo, simu inapigwa kila baada ya sekunde 20 kutoka huko kwenye changamoto iliyonifanya niende kukopa, nilipagawa sana. Wakati afisa mikopo ananieleza habari za makato n.k mimi hata sikuwa nasikia chochote.

Akili ilikuwa kwenye kupata pesa tu nikamalize tatizo. Siku kadhaa mbele nikafanikiwa na tatizo likaisha na akili ikarudi katika utulivu wa kawaida.

Siku zinavyoenda haraka, mwisho wa mwezi ukafika bwana! Aisee, ile naiangalia salary slip sikuamini nilichokiona. Milioni 24 nahitajika kulipa. 24M!!

Kwanza nilihisi baridi, halafu ganzi; baadae nikahisi uono wangu kama hauko sawa. Nikajiuliza imekuaje mbona sioni vizuri? Kwakuwa nilikuwa chumbani, nikasogea kwenye kioo kujiangalia. Dah, si ndo nakuta jicho moja la upande wa kushoto limejifunga, kope haitaki kupanda juu ('kukupila' watu wa pwani ya kusini wanasema).

Nikajaribu kulifunua kwa mkono, wapi! Nikiliacha linajifunga tena. Hali iliendelea hivyo kama dakika 40 au saa moja hivi. Baadae sana ndo likarejea katika hali ya kawaida. Nilishapagawa, nilijua limeparalyse!

Mikopo!!!! Ukiweza kuachana nayo iache ndg'angu!
Duuh,pole sana.
 
Kwa hesabu za fasta umelipa riba 28% na sio 17 % kama unavyosema , hapo zinaongezeka vipi ,kwa nini kwenye mkataba wa mkopo hawaelezi haya ??
Hapana, hesabu za benki riba huwa ni kwa mwaka, kwenye mkopo wangu ilionyesha hiyo 17%, ambapo kwa hesabu za kawaida ningelipa 51% kwa hiyo miaka 3. Hiyo 28% ni kwa miaka 3 so kwa mwaka ni 9.5%.
 
Wala siyo kweli. Ina maana hukujaza Mkataba mpaka usubirie slip? Maana mkataba huainisha kiasi chote unachopaswa kulipa.

Na hakuna benki Tanzania inayotoza riba ya zaidi ya asilimia 100. Hakuna.

Hii ni Chai.
UMBA YASIKUKUTEEE...OMBA SANA NDUGU[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] sio asilimia 100 tu bali 200...
 
Back
Top Bottom