Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,746
ha haaa, nimelipenda hili jibu lako rafiki.......umechoka kwani huwaga anakupa nyumba ubebe kichwani??
hivi unavyoona wenzio tunahesabu tu miaka ya kuwa ndoani usifikiri humo ndani ni asali tu, kuna muarobaini pia..... ila kwa vile tunapokutana nazo tunakunywa kama dawa tunapata uponyaji. asali tunakunywa huku tunatabasamu na kumshukuru Mungu kuwa daktari wa leo kaniandikia dawa ya asali.... muarobaini tunakunywa huku tunamwomba Mungu atusaidie kuweza kumeza maana unaihitaji ili upate uponyaji.Nawashukuru sana mlionipa ushauri humu mbarikiwe, nimesikia moyo wangu umepata dawa na uso wangu sasa umenyooka kwa tabasamu ninayopata, mbarikiwe nawaahidi kuyafanyia kazi na ile ya kuondoka nimeiweka miguuni maana nimeikanyaga nikipiga hatua moja mbele naiacha hapo. Pamoja sana MMU Mkunde anawapenda sana.
Nilihisi maana hiyo kwa sababu kuna lugha ingine maana yake hiyo hiyo..Maana yake MPENDE AU MPENDWA inategemea ni kabila gani limetokea ila kwa mimi kwa kabila lililotoka maana yake MPENDE.
hivi unavyoona wenzio tunahesabu tu miaka ya kuwa ndoani usifikiri humo ndani ni asali tu, kuna muarobaini pia..... ila kwa vile tunapokutana nazo tunakunywa kama dawa tunapata uponyaji. asali tunakunywa huku tunatabasamu na kumshukuru Mungu kuwa daktari wa leo kaniandikia dawa ya asali.... muarobaini tunakunywa huku tunamwomba Mungu atusaidie kuweza kumeza maana unaihitaji ili upate uponyaji.
Mungu anahusika sana kwenye raha na shida. kaza buti, songa mbele..... hakuna kurudi nyuma, na hasa ukizingatia kuwa bado unampenda, hiyo ni silaha yako kubwa sana....
Kila la heri
Mmmmmh dada maneno yako yameniingia ila ........................
Kiufupi sina mpango wa kumfanyia uhalifu wowote nabeba nguo zangu tuu na za mtoto. Tatizo pia hanipi hiyo nafasi ya kumuaga nimejaribu njia zote anazofanya mwanamke mwenye boma kutunza boma lake nimeshindwa sijajua nakosea wapi kwangu naona kama naishi bure nikiendelea kukaa humu, nilishawahi kuondoka mwaka mzima nilikuwa kwa wifi yangu wala hakunitafuta mimi wala mtoto wala kuulizia kama hata nimepata ajali au la . Kweli ni mume wa ujana wangu lakini.............!!!???
umekusanya mtaji wa kutosha au ndo unarudi kijijini kwa wazee,kama hujachukua endelea kumvumilia kama mwezi hivi ujichotee rasilimali mwaya.....kitaa ni pagumu thana.
Kwako baba mtoto,
Samahani nimekuja huku maana najua unashinda humu kuliko kushinda nyumbani, nimeamua kuvuja kwenye pakacha lako iwe nafuu kwako kulibeba, baki salama.
Nilikupenda sana mfano wa keki/chokoleti (napenda sana keki na chokoleti)
Lakini hukupendeka......., nimechoka hakika sijiwezi, kuishi tena mi na wewe
Ingawa nakupenda, lakini sitoweza.....
Ingawa rohoni nimekwisha, namwomba mola anisaidie, niweze kukusahau kabisa, nipate mwingine kushinda wewe.
Najua unausoma ujumbe huu muhusika ila leo ukirudi nyumbani hutanikuta, nitapotea kwenye taswira ya uso wako na maisha yako kabisa, hutaniona tena.
Naenda kuanza upya.
Aliyekuwa mkeo, mama mtoto wako na aliyekupenda daima,
Mkunde.
:disapointed::disapointed:
Snowhite, Mkunde ni jina la KICHAGA. Smile hebu njoo utowe maana ya jina la Mkunde.
Huyu atakuwa aliolewa na Mchaga mwenzake au Msukuma, sisi Wadakama huwa ni kwa nadra sana kuolea uchagani. Niko mbioni kuibadilisha kidogo hii statistic ili niwe Mdakama (Mnyamwezi) mwingine aliyeolea Uchagani.
Nikiwa Msange JKT 1989 nilipenda sana dada mmoja mwenye jina hilo. Siku moja nikamuona wamemsimamisha mnazi, nikakata tamaa maana nilishapanga niowe kabisa...... Ila kalikuwa kametulia vizuri sana kitoto cha Kichaga.
kama hakuhangaika wakati upo nyumbani,ukiondoka ndio atahangaika!!!!!!
kama ulimwambia mkiwa nyumbani,then kwa sim the Message was sent and delivered
Mkunde Original hukuwa na haja ya kuja huku,usijitese zaidi mateso aliyokupa yanatosha.....