Pole, now I understand clearly. Ulitakiwa kuonesha umekulia katika familia gani tangu mwanzo ili wachangiaji tukuelewe wewe ni mtu wa aina gani.
Kwanza nataka ujue hili, "The truth is, everyone is going to hurt you. You just got to find the ones worth suffering for."
Usidhani kuna mwanamme utampata akawa perfect 100%, unachotakiwa kujiuliza ni je, anakupa furaha? Anatimiza majukumu yake? Ankupenda kwa dhati? Ukishajijibu maswali hapo juu, utajua kama anakufaa ama lah.
At 30, ulitakiwa kuwa mwanamke mkomavu, ngangari na mwenye kutafuta suluhisho la matatizo yake kwa njia za kiutu uzima zaidi, Hili ulilofanya hapa, ni kama binti wa miaka 17. Haliendani na umri wako kabisa.
Wakati huo huo, baada ya kujua umelelewa na bibi, uko peka yako, nimekuelewa kwa nini umetumia njia hii. Watoto wanaolelewa na bibi zao wanakuwa na deko zisizo za kiuhalisia. Unaweza kuwa ulizoea kubembelezwa bembelezwa bila sababu za msingi. Ndio maana labda hata huyu mwanamme uliyenaye anaona kero kushinda na wewe sababu unataka kila saa ubembelezwe (love sucker?')
Kwanza unatakiwa kujiuliza, kwa nini mzazi mwenzio anashinda mtandaoni? Unamkera? Na kama ndio, ni mambo yapi yanamkera?
na watu wengine husema, watoto wanaozaliwa na kulelewa peke yao huwa selfish in term ya vitu na hisia, je na wewe ukoje katika hilo?
Emotional stability yako pia unatakiwa kuichunguza, are you emotionally stable? Sio kakitu kadogo tu unaruka kama umeona simba. Kweli alichokifanya mzazi mwenzio kinastahili kuachana.
Mie nakushauri kwanza ujichunguze mapungufu yako, halafu ndio uanza kumlaumu mzazi mwenzio. Nashawishika kuamini kuwa wewe ndio chanzo cha matatizo, bila hata ya wewe kujijua. na inaweza kuwa inachangia na makuzi yako.
You can do better than this. Hii dunia sio laini kihivyo, usipokuwa imara wewe mwenyewe kutetea unalolitaka hakuna atakayekuja kukutetea. Be strong for you kid and hubby, hili linajadilika. Kaa nyumbani, pika, msubiri mmoe jioni akirudi mkalishe chini muongee. Waweza jaribu kumuuliza kama na wewe unamkwaza, usidhani wewe ni malaika.
Na pia jaribu kuangalia mmeo kakulia mazingira yapi, kama ni mtu asiye emotional sana, ujue hapo kuna 'clash' Inabidi mjadialiane mtachukulianaje hizo tabia zenu za kuhisia.
Mengi ya kuandika hapa.
Hata sijui hizo latin soap operas zinafananaje, this is not a movie jamani ni true life ambayo nimepitia, its sirias issue.
Nina miaka 30, ndugu nilionao ni wa baba mtoto tuu, mimi nilizaliwa mwenyewe nimelelewa na bibi nae alishakufa baba sikumfahamu wala ndugu zake, mama aliniacha kwa bibi wakati niko mdogo na aliolewa na mjerumani wakati nasoma primary hajarudi tena hadi leo na sina mawasiliano nae. Ndugu wa baba mtoto wangu siko karibu nao maana ni familia ambayo iko busy sana na mambo ya kazi na kutafuta hela hawana muda wa kusocialise hata ukienda mtembelea kama huna appointment humuoni na ukiweka appointment ni ten minutes anakwambia nina kikao zaidi ya hapo sina wa kuongea nae.