Nilikuwa mfuasi wa Trump Kwa Muda Mrefu sana Ila Kwa Hili la Kusitisha Misaada na Ruzuku upande wa Afya Sikubaliani nalo, amekosea sana

Nilikuwa mfuasi wa Trump Kwa Muda Mrefu sana Ila Kwa Hili la Kusitisha Misaada na Ruzuku upande wa Afya Sikubaliani nalo, amekosea sana

Jambo muhimu: utawala ni nini.
Unafikiri hawataki kujitawala?

Utawala kwa muktadha wa hapa ni uwezo wa kujiendeshea mambo yao wenyewe.

Kwa maneno Waafrika wengi watasema wanapenda kujitawala.

Lakini, kusema unapenda kujitawala si kupenda kujitawala.

Kupenda kujitawala kunaendana na kupenda kufanya kazi inayopelekea kujitawala.

Hapo kwenye kufanya kazi inayopelekea kujitawala Waafrika hawajaonesha kuwa wanapenda kujitawala.

Waafrika wengi, sio wote, wengi, wanapenda kutawaliwa, wanapenda mtu mwingine awafanyie mambo, wao wapate urahisi wa kuishi bila kufanya kazi kubwa.

Hili ni suala la kiutamaduni, si la kibaiolojia.
 
Utakula ulikopeleka mboga.

Sicheki na wowote.
downloadfile-25.jpg
 
Utawala kwa muktadha wa hapa ni uwezo wa kujiendeshea mambo yao wenyewe.
Utakubali kuwa Serikali za kiafrika haziwezi kujiendesha zenyewe.

Kwanini zimeshindwa kujitegemea?

Sababu sio za kibalojia. Sababu ni za kitamaduni kama ulivyosema.

Lakini swali, kwa nini tamaduni za waafrika?
 
Utakubali kuwa Serikali za kiafrika haziwezi kujiendesha zenyewe.

Kwanini zimeshindwa kujitegemea?

Sababu sio za kibalojia. Sababu ni za kitamaduni kama ulivyosema.

Lakini swali, kwa nini tamaduni za waafrika?
Africa, hususan kusini mwa jangwa la Sahara, ni bara lililokuwa isolated zaidi. Wakati wenzetu wa Ulaya na Asia wanaingiliana kibiashara na kubadilishana uzoefu, Africa iliachwa ikiwa haina muingiliano sana na dunia. Kwa sababu za Kijiografia.

Pia, Africa sehemu nyingi ina neema ya asili. Neema hii imepelekea watu kubweteka. Neema hii kama vile hali nzuri ya hewa, imepelekea balaa la magonjwa mengi, yaliyofanya ukuaji wa idadi ya watu kuwa mdogo, na hili lilipelekea ujengaji wa miji mikubwa kuwa mdogo. Miji mkubwa ndiyo injini inayosukuma uchumi na tamaduni kukua kwa kasi.

Waafrika wengi walikuwa insular, hawakupenda kusambaa duniani kutafuta maarifa ya nje. Mfano mmoja ni wa Mansa Aboubakar II wa Mali, ambaye tunapata habari zake kutika Mansa Musa aliyemfuatia. Mansa Musa alivyokuwa Cairo July 1324 anakwenda kuhiji Mecca, aliulizwa na watu wa Cairo, amepata vipi kuwa Mfalme wa Mali? Akajibu kuwa aliyemtangulia alikwenda safari za nchi za mbali baharini akamuacha awe Mfalme. Aboubakar II. Lakini, Aboubakar II badala ya kuwa celebrated kama explorer, akafutwa kwenye vitabu vya Wafalme wa Mali.

Sababu ni nyingi, kwa sasa niweke kituo hapa.
 
Nchi za Afrika Zote haziwezi kutoboa kwa Disease Burden Iliyopo Ngoja Twende statistically..

  • Riport ya mwaka jana Tanzania Kwa sasa Ina WAVIU- 1.7Milion na waviu wanaotumia ARV ni 1.4 Milion
  • Waliokuwa wana Ugonjwa wa Malaria walikuwa ni zaidi ya Milion 1
  • Watoto waliopatiwa Chanjo ni zaidi ya Milion 1
  • Watu waliotumia Njia za Uzazi wa Mpango ni zaidi ya Milions
  • Wagonjwa wa TB kwa mwaka Jana walikuwa zaidi ya Laki mbili
Hakuna Nchi narudia tena Hakuna nchi wala Chama Kinachoweza Kubeba Hiyo burden Bila Kuhitaji Msaada..
unajua Chanjo moja ni Bei gani? Unajua ARV Drugs Ni Tsh ngapi Kopo Moja? Unajua Uzazi wa Mpango Hata Kidonge tu Circle mpja Ni Tsh ngapi??
Mbona tunaweza nunua ma V8 kila mwaka na kufadhili mwenge!! Hata iwe 50 B tuna uwezo wa kugharamia tatizo ni vipaumbele tu. Kupunguza tu posho za wabunge zinaweza fidia hiyo deficit
 
Mbona tunaweza nunua ma V8 kila mwaka na kufadhili mwenge!! Hata iwe 50 B tuna uwezo wa kugharamia tatizo ni vipaumbele tu. Kupunguza tu posho za wabunge zinaweza fidia hiyo deficit
Shida Inakuja waliopo Katika Maamuzi hayo Sifa yao Kubwa Ni wajue Kusoma Na Kuandika Tu..
Unahisi Ni sahihi ,Kujua Kusoma Na Kuandika Kufanya Maamuzi ya Kisomi kama Hayo??
 
Back
Top Bottom